Thursday, November 1, 2012

 

Kikapu Taifa yapamba moto

Brown Msyani,Tanga
Timu ya mpira wa kikapu ya mkoa wa Arusha imeichapa timu ya mkoa wa Tanga kwa pointi 87-50 katika mfulilizo wa mashindano ya Kombe la Taifa kwenye Uwanja wa mkwakwani mjini hapa.

Katika mchezo huo, mchezaji Bariki Kilimbo wa Arusha alifunga pointi 18 peke yake na kuzuia mara 6, pasi mara 6.

Aliyemfuatia kwa kujaza pointi nyingi alikuwa Martin Ajesa aliyepata 15, huku upend wa Tanga B Sefu Semboya akifunga pointi 25 akifutiwa na Abasi Omary aliyefunga pointi 10.

Timu zote ziliingia dimbani na kucheza mchezo wa kasi uliojaa pasi za haraka haraka, huku Arusha ikiongoza kwa pointi 16-9 robo ya kwanza.

Katika nusu ya pili, walikuwa Arusha waliendelea kuipeleka puta Tanga B iliyolazimika kuutafuta mpira kwa 'tochi' na kujikuta wakiwa nyuma kwa pointi 28-11.

Arusha walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 44-20, na robo ya mwisho, Arusha walikuwa mbele kwa 30-11.

Katika mchezo mwingine, timu ya Mkoa wa Singida iliifunga Kilimanjaro kwa point 79-58.

Mashindano hayo yaliyoanza juzi kwa wenyeji Tanga kuanza vizuri baada kuifunga Pwani pointi 64-4.

Mashindano ya mwaka jana, Dar es Salaam, Singida ndiyo walioibuka na ubingwa baada ya kuifunga Unguja katika mchezo wa fainali.

Kwa upande wa wanawake, mabingwa walikuwa timu ya mkoa wa Mbeya.

 

VPL: Stewart Hall arudi Chamazi kwa kishindo, AZAM yaishindilia Coastal 4-1!!

>>NI SALAM SPESHO kwa Yanga Jumapili!!!
VPL_LOGOWakiwa kwao Uwanja wa Azam Complex huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC leo wameitwanga Coastal Union kwa bao 4-1 katika Mechi ya Ligi Kuu Vodacom, VPL, ikiwa ni Mechi ya kwanza tu kwa Kocha Stewart Hall alierejeshwa tena Klabuni hapo baada ya kuondolewa Mwezi Agosti na nafasi yake kutwaliwa na Kocha kutoka Nchini Serbia Boris Bunjak aliefukuzwa majuzi baada ya kutwangwa na Simba.
++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za Juu:
1 Simba Mechi 11 Pointi 23 [Mabao: Kufunga: 20 Kufungwa: 8 Tofauti: 12]
2 Yanga Mechi 11 Pointi 23 [Mabao: Kufunga: 21 Kufungwa: 10 Tofauti: 11]
3 Azam FC Mechi 10 Pointi 21
4 Coastal Mechi 11 Pointi 19
++++++++++++++++++++++++++
Ushindi huu wa leo umeifanya Azam ikamate nafasi ya 3 ikiwa na Pointi 21 kwa Mechi 10 wakiwa wamecheza Mechi moja pungufu ya Timu za juu yao Simba na Yanga ambazo zote zina Pointi 23 kila mmoja.
Bao za Azam, ambao waliongoza 3-0 hadi mapumziko, zilifungwa na Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche, Khamis Mcha na Othman wa Coastal aliejifunga mwenyewe.
Bao pekee la Coastal Union lilifungwa na Jeery Santo.
Mechi inayofuata kwa Azam FC ni hapo Jumapili ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam watakapoivaa Yanga.
RATIBA:
Novemba 3
Ruvu Shooting v Toto Africans [Mabatini, Pwani]
African Lyon v Mgambo JKT [Azam Complex, Dar es Salaam]
Kagera Sugar v Tanzania Prisons  [Kaitaba, Kagera]
Novemba 4
Azam v Yanga [National Stadium, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Simba [Jamhuri, Morogoro]
Azam v JKT Oljoro [Azam Complex, Dar es Salaam]
++++++++++++++++++++++++++

 PICHA MBALI MBALI KATIKA MECHI YA AZAM NA WAGOSI WA KAYA HAPO JANA

Samir Hajji Nuhu na Khamis Mcha 'Vialli' wakimpongeza Gaudence Mwaikimba (katikati) kufunga bao la kwanza katika mchezo wa  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam dhidi ya Coastal Union ya Tanga. Azam ilishinda mabao 4-1.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen akimuelekeza jambo kuhusu mechi hiyo Kocha wa timu za vijana, Jacob Michelsen kulia 

Kim na Jacob wakifuatilia mechi

Meneja wa Taifa Stars, Leopold Tasso Mukebezi kushoto akiwa na Ofisa wa TFF, Saad Kawemba

Kocha wa timu za vijana wa Azam, Vivek Nagul akinukuu mambo muhimu kuhusu mchezo huo, na baada ya hapo anakutana na Kocha Mkuu, Stewart kumpa ripoti ili mapungufu yafanyiwe kazi

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu' akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Coastal kulia

Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Wakili Imani Madega alikuwepo Chamazi leo

Makocha wa Yanga, Ernie Brandts kulia na Msaidizi wake, Freddy Felix Minziro walikuwepo kuifanyia ushushushu Azam Chamazi leo

Bado Yanga; Gaudence akishangilia bao lake, ambalo ni tamu kwa kweli

Hajji Nuhu na Gau Mwaikimba

Gau baada hya kufunga

Kama yupo mtu leo alikuwa anatia huruma, basi ni M kurugenzi wa Ufundi wa Coastal, Nassor Bin Slum...hapa anatuliza mawazo kwa sigara yake

Bosi leo alikuwa anatia huruma

Kama vile amtukane TANO JUMA  baada ya kumshitukia anampiga picha...lakini busara ikamzuia

Samir Hajji Nuhu anaambaa kulia

Kipre Balou anamtoka Othman Tamim

Kipre Tcheche anamtoka Juma Jabu

Daniel Lyanga kulia na Said Mourad kushoto

Lyanga na Mourad

Balou na Othman

Tcheche na Jabu kulia

Mwadini Ali akiwa amedaka moja ya michomo iliyoelekezwa langoni mwake leo

Cheki pande la Salum Abubakr linavyopasua msitu kuelekea kwa Mwaikimba (hayupo pichani)

Stewart kazini

Mwaikimba katikati ya msitu wa mabeki wa Coastal        

 Gor Mahia yatangaza jihad

Hiki ni kikosi cha timu ya Footprints inayoshiriki Ligi ya Kikapu ya Nairobi. Chipukizi hawa wameonyesha mchezo wa kuvutia msimu huu. Picha na John Kimwere

KOCHA wa Gor Mahia, Zdravko Logarusic, ambaye sasa vijana wake wameishika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Kenya, amesema wameshainusa harufu ya ubingwa hivyo hakuna kulala tena, bali ni mwendo wa dozi tu katika mechi nne zilizosalia.

Jumatano usiku wana K'Ogalo walitwaa nafasi hiyo hivyo kuishusha AFC Leopards kwa nafasi moja ilipoilaza Rangers mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Nyayo.

Kwa kufanya hivyo imekuwa kama mchezo wa vigogo hivyo kubadilisha nafasi hiyo iliyo nyuma ya vinara, Tusker FC.

Lakini Logarusic alisema: "Hakuna kurudi nyuma tena, ni lazima tuhakikishe tunazishinda Karuturi Sports, Tusker, Muhoroni Youth na Thika United ili kutimiza ndoto zetu za ubingwa."

Gor ina kazi kubwa kwani Leopards nayo inaonekana bado kuwa na kiu ya ubingwa huku Tusker iliyo kileleni kwa pointi 51 nayo ikiwa macho mbele. Gor kwa sasa ina pointi 49, moja mbele ya Leopards.

"Tumeshainusa harufu ya ubingwa, huu sasa ni wakati wa kazi nzito. Ni lazima tujitume kwa nguvu zetu zote ili kufanikisha azma, upinzani ni mkali lakini ninaamini tuna uwezo," alisema kocha huyo.

Kwa sasa Logarusic ana wiki mbili za kukiimarisha zaidi kikosi chake kwani ligi hiyo imesimama kupisha mechi za Kombe la FKF 'President Cup' na maandalizi ya timu ya taifa, Harambee Stars, inayojiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi Afrika Kusini.

WENGER: “Hatumuongelei RVP, hamna kisasi! Nataka Mashabiki wamuheshimu!”


>>OLD TRAFFORD Jumamosi: Man United v Arsenal!
>>MECHI ya kwanza Robin van Persie kukutana na Ze Ganaz tangu ahame!!
>>WENGER aungama: “RVP ni Denja!!”
ARSENE_WENGER-13Arsene Wenger amepoza maneno ya Mashabiki wa Arsenal kutaka kisasi kwa Robin van Persie kwa RVP_in_RED2kuihama Timu hiyo na kwenda Manchester United wakati Timu hizo zitakapokutana Jumamosi Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na hiyo ikiwa mara ya kwanza kwa Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal kukutana na Timu yake ya zamani tangu ahame.
Wenger amewataka Mashabiki wa Arsenal watakaokuwepo Old Trafford kumwonyeshea heshima Robin van Persie na si kumkashifu na kumtukana.
Wenger alitamka: “Kwetu, muhimu ni matokeo na uchezaji wetu. Hatumzunguzii kabisa Van Persie. Natumaini Mashabiki watamuheshimu kwani kachezea kwetu Miaka minane na alifanya vizuri sana!”
Alihoji: “Tunapiga vita Ubaguzi, Wiki iliyopita ilikuwa hivyo na kwa nini isiwe sasa?”
Akiichezea Arsenal, Robin van Persie, mwenye Miaka 29, aliifungia Arsenal jumla ya Mabao 132, 37 yakiwa Msimu uliopita na kuwawezesha kushika nafasi ya 3 kwenye Ligi.
Wenger amesema: “Daima unataka uongoze Watu vizuri wawe na maisha mazuri! Wakifanikiwa unaridhika, sidhani kwake nilifanya vibaya!”
Hadi sasa, kwa Kipindi kifupi, Van Persie ameifungia Man United Bao 7 kwenye Ligi na yeye na Demba Ba wa Newcastle ndio wanaongoza kwenye Ufungaji.
Hilo halikumshangaza Wenger ambae ametamka: “Sishangazwi na yeye kufanya vizuri. Man United ina Wachezaji wazuri sana, na Robin ni mjanja kwenye boksi, mwenye kasi na kujua nafasi huashangaza! Wapo Wachezaji wazuri na Robin atanufaika tu. Robin ni Straika hatari sana!”


LIGI ULAYA: Juve kuivaa Inter, wawania kutofungwa Mechi 50!


EL_SHAARAWY-AC_MILAN>>BUNDESLIGA: Baada kichapo, vinara Bayern wataka faraja!
>>LA LIGA: Barca na Atletico zafukuzana, Real yajivuta!!
ZIFUATAZO ni Taarifa fupi kuhusu Ratiba na hali ya Ligi za Serie A, Bundesliga na La Liga:
SERIE A: Juve yawania kutofungwa Mechi ya 50 ikicheza na Inter Jumamosi!
RATIBA:
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
[SAA za BONGO]
Alhamisi Novemba 1
Genoa v Fiorentina [Comunale Luigi Ferraris]
Jumamosi Novemba 3
2000 AC Milan v Chievo Verona [Stadio Giuseppe Meazza]
2245 Juventus v Inter Milan [Juventus Stadium]
Jumapili Novemba 4
US Pescara v Parma [Adriatico]
Bologna v Udinese [Stadio Renato Della`Ara]
Catania v Lazio [Stadio Angelo Massimino]
Fiorentina v Cagliari [Stadio Artemio Franchi]
Napoli v Torino [Stadio San Paolo]
Sampdoria v Atalanta [Comunale Luigi Ferraris]
Siena v Genoa [Artemio Franchi]
AS Roma v Palermo [Stadio Olimpico]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Juventus wanaweza kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika Mechi 50 za Ligi ya Serie A Jumamosi watakapocheza na Inter Milan ambao wako nafasi ya pili nyuma ya Juventus kwa Pointi 4.
Baada ya Mechi 10, Juventus wana Pointi 28 kwa kushinda Mechi zote kasoro sare katika Mechi moja tu lakini Inter Milan wanakuja na moto baada ya kushinda Mechi zao 9 zilizopita, za Ligi na Mashindano mengine, na hilo linaifanya Mechi hiyo kuwa ni tamu.
Juventus, ambao ndio Mabingwa watetezi, walitwaa Taji Msimu uliopita bila kufungwa hata Mechi moja na mara ya mwisho kufungwa kwenye Ligi ilikuwa ni katika Msimu wa 2010/11 walipofungwa na Parma Mechi moja kabla Ligi kwisha.
Rekodi ya kutofungwa katika Mechi nyingi inashikiliwa na AC Milan waliyoiweka katika Miaka ya 1990 kwa kutofungwa Mechi 58.
BUNDESLIGA
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Ijumaa Novemba 2
Eintracht Frankfurt v SpVgg Greuther Fürth [Commerzbank-Arena]
Jumamosi Novemba 3
Borussia Dortmund v VfB Stuttgart [Signal-Iduna-Park]
Borussia Monchengladbach v SC Freiburg [Borussia-Park]
Hannover 96 v FC Augsburg [AWD-Arena]
Nurnberg v  VfL Wolfsburg [EasyCredit-Stadion]
TSG Hoffenheim v Schalke 04 [Rhein-Neckar-Arena]
Hamburg SV v Bayern Munich [HSH Nordbank Arena]
Jumapili Novemba 4
Bayer Leverkusen v Fortuna Düsseldorf [BayArena]
Werder Bremen v Mainz [Weserstadion]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Vinara wa Bundesliga Bayern Munich Jumamosi wanatinga kwenye Dabi watakapocheza ugenini na Hamburg kwenye Mechi ya Ligi ya Bundesliga lakini ndio kwanza wanatoka kwenye kipigo chao cha kwanza cha Ligi hiyo walipofungwa Wiki iliyopita 2-1 na Bayer Leverkusen.
Hata hivyo, Bayern, Jumatano, waliichapa Kaiserslautern bao 4-0 katika Mechi ya kugombea German Cup.
Bayern wapo kileleni wakiwa na Pointi 24 wako Pointi 4 mbele ya Schalke na Hamburg wapo nafasi ya 7 wakiwa na Poniti 13.
Schalke watakuwa ugenini kucheza na Timu ya chini Hoffenheim.
Mabingwa watetezi Borussia Dortmund, ambao wapo nafasi ya 4, watacheza Jumamosi na Stuttgart.
LA LIGA
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Jumamosi Novemba 3
Málaga v Rayo Vallecano [Estadio La Rosaleda]
2000 Barcelona v Celta Vigo [Estadio Camp Nou]
2200 Real Madrid v Real Zaragoza [Estadio Santiago Bernabéu]
Jumapili Novemba 4
Deportivo La Coruña v Mallorca [Estadio Riazor]
Granada v Athletic Bilbao [Estadio Los Cármenes]
Osasuna v Valladolid [Estadio El Sadar]
Real Sociedad v Espanyol [Estadio Anoeta]
Sevilla FC v Levante [Estadio Ramon Sanchez Pizjuan]
Valencia v Atlético Madrid [Estadio Mestalla]
Jumatatu Novemba 5
Getafe v Real Betis [Coliseum Alfonso Perez]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Baada ya kushinda kwenye Mechi zao za Copa del Rey katikati ya Wiki vinara Barcelona, Timu ya pili Atletico Madrid na Mabingwa watetezi Real Madrid wote wapo dimbani Wikiendi hii kucheza Mechi za La Liga.
Barcelona ambao waliwafunga  Alaves 3-0 kwenye Mechi ya Copa del Rey na kuwapumzisha Mastaa wao, Kipa Victor Valdes, Xavi Hernandez, Lionel Messi na Pedro Rodriguez, wanatarajiwa kuwarudisha wote hao watakapocheza na Celta Vigo Uwanjani Nou Camp.
Atletico Madrid, ambao nao waliipiga Jaen 3-0 kwenye Copa del Rey, wataenda ugenini kucheza na Valencia.
Nao Mabingwa Real Madrid, ambao pia walishinda kwenye Copa del Rey kwa kuichapa Alcoyano bao 4-1, watakuwa nyumbani Estadio Santiago Bernabeu kucheza na Real Zaragoza huku wakijijua wako Pointi 8 nyuma ya Barca na ni lazima wapate matokeo mazuri.
 

BPL: Wikiendi kuanza mapema kwa moto wa Man United v Arsenal!


BPL_LOGO>>REFA CLATTENBURG hakupangiwa Mechi Wikiendi hii kupisha uchunguzi wa malalamiko ya Chelsea!
Ligi Kuu England, BPL [Barclays Premier League], inaingia kwenye Raundi yake ya 10, isipokuwa kwa Sunderland na Reading ambazo zina kiporo cha Mechi kati yao, na baada ya Wikiendi iliyopita vinara Chelsea kunyukwa bao 3-2 wakiwa kwao Stamford Bridge na Manchester United, lile pengo kati ya Chelsea na Timu za nyuma yake, Man United na Mabingwa Man City, limebaki Pointi 1 tu.
Mbali ya Man United ambao wako nyumbani kupambana na Arsenal katika Mechi ya kwanza kabisa hapo Jumamosi, Chelsea na Man City zote zipo ugenini kwa Chelsea kucheza na Swansea City na Man City kukipiga na West Ham huko Upton Park, Jijini London.
Kufuatia Chelsea kuwasilisha malalamiko kwa FA, Chama cha Soka England, kuhusu Refa Mark Clattenburg kutumia lugha isiyofaa katika Mechi Chelsea waliyofungwa 3-2 na Manchester United Jumapili iliyopita dhidi ya Wachezaji wake John Mikel Obi na Juan Mata na pia kuwepo kwa uchunguzi wa Polisi baada ya Kikundi cha Wanasheria Weusi kulalamika kuhusu tukio hilo, Refa huyo ameondolewa kuchezesha Mechi za Wikiendi hii.
ZIFUATAZO NI RATIBA, MSIMAMO, MAREFA waliopangwa Mechi zote za Wikiendi na WAFUNGAJI BORA:
RATIBA:
Jumamosi, Novemba 3, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Manchester United v Arsenal
[SAA 12 Jioni]
Fulham v Everton
Norwich City v Stoke City
Sunderland v Aston Villa
Swansea City v Chelsea
Tottenham Hotspur v Wigan Athletic
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Ham United v Manchester City
Jumapili, Novemba 4, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Queens Park Rangers v Reading
[SAA 1 Usiku]
Liverpool v Newcastle United
Jumatatu, Novemba 5, 2012
[SAA 5 Usiku]
West Bromwich Albion v Southampton
MAREFA wa MECHI za WIKIENDI:
Jumamosi Novemba 3
Manchester United v Arsenal
Refa: M Dean
Wasaidizi: S Ledger, A Garratt
Refa wa Akiba: P Dowd
Fulham v Everton
Refa: N Swarbrick
Wasaidizi: D Bryan, M Wilkes
Refa wa Akiba: M Oliver
Norwich City v Stoke City
Refa: A Marriner
Wasaidizi: G Beswick, A Holmes
Refa wa Akiba: P Tierney
Sunderland v Aston Villa
Refa: M Jones
Wasaidizi: D C Richards, J Brooks
Refa wa Akiba: C Foy
Swansea City v Chelsea
Refa: K Friend
Wasaidizi: C Breakspear, M Scholes
Refa wa Akiba: J Moss
Tottenham Hotspur v Wigan Athletic
Refa: M Atkinson
Wasaidizi: S Child, M McDonough
Refa wa Akiba: C Pawson
West Ham United v Manchester City
Refa: H Webb
Wasaidizi: D Cann, P Bankes
Refa wa Akiba: L Mason
Jumapili Novemba 4
Queens Park Rangers v Reading
Refa: M Oliver
Wasaidizi: S Long, D England
Refa wa Akiba: M Atkinson
Liverpool v Newcastle United
Refa: A Taylor
Wasaidizi: S Burt, A Halliday
Refa wa Akiba: M Jones
Jumatatu Novemba 5
West Bromwich Albion v Southampton
Refa: M Halsey
Wasaidizi: R Ganfield, J Flynn
Refa wa Akiba: M Dean
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 9 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea Pointi 22
2 Man Utd  21
3 Man City  21
4 Tottenham 17
5 Everton 16
6 Arsenal 15
7 Fulham 14
8 West Brom 14
9 West Ham 14
10 Newcastle 13
11 Swansea 11
12 Liverpool 10
13 Stoke  9
14 Sunderland Mechi 8 Pointi 9
15 Wigan 8
16 Norwich 7
17 Aston Villa 6
18 Reading Mechi 8 Pointi 4
19 Southampton 4
20 QPR 3
WAFUNGAJI BORA:
Demba Ba [Newcastle] Mabao 7
Van Persie [Man United] 7
Michu  [Swansea] 6
Suarez [Liverpool] 6
Defoe [Tottenham] 5
Dzeko [Man City]5
Fletcher [Sunderland] 5
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi, Novemba 10, 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Fulham
Everton v Sunderland
Reading v Norwich City
Southampton v Swansea City
Stoke City v Queens Park Rangers
Wigan Athletic v West Bromwich Albion
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Manchester United
Jumapili, Novemba 11, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Manchester City v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Ham United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Liverpool
 

MVUA ya MAGOLI Jumamosi Man United v Arsenal Old Trafford??

>>ARSENAL haijashinda Old Trafford katika Mechi 8 za mwisho!!
>>RVP kuivaa Timu yake ya zamani kwa MARA ya KWANZA!!
RVP_in_RED>>PATA DONDOO na REKODI za Mechi Man United v Arsenal!
Jumamosi Novemba 3, ndani ya Uwanja wa Old Trafford, Manchester United itaikaribisha Arsenal katika moja ya Mechi za Ligi Kuu England, BPL, ambayo inangojewa kwa hamu kubwa kwani inazikutanisha Timu ambazo, kati yao, zimefunga na kufungwa jumla ya Magoli 41 katika Mechi 8 kuanzia Oktoba 20 na pia mvuto upo kumuona Nahodha wa zamani wa Arsenal, Robin van Persie, akiivaa Klabu yake ya zamani kwa mara ya kwanza tangu ahamie Man United mwanzoni mwa Msimu huu.
Bila shaka, Arsenal watakuwa na wasiwasi kumvaa Straika ambae wakiwa nae Msimu uliopita aliifungia jumla ya Magoli 37 na tangu atue Man United mtambo wake wa magoli umeendelea mtindo mmoja.
Juzi Jumanne, Arsenal walitoka nyuma kwa Bao 4-0 walipocheza kwenye Kombe la Ligi na kuifunga Reading 7-5 katika Dakika 120 za Mchezo huku Theo Walcott akipiga hetitriki.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 9]
1 Chelsea Pointi 22
2 Man United 21 [Tofauti ya Magoli 11]
3 Man City 21 [Tofauti ya Magoli 9]
4 Tottenham 17
5 Everton 16
6 Arsenal 15
7 Fulham 14
8 WBA 14
9 West Ham 14
10 Newcastle 13
MAN_UNITED-ANDO_RVP_SHINJI_EVRA+++++++++++++++++++++++WALCOTT_WILSHERE_OX
Msimu uliopita, Mwezi Agosti Mwaka jana Uwanjani Old Trafford, Arsenal walichabangwa bao 8-2 kwenye Mechi ya Ligi na Msimu huu Man United wamekuwa wakiendeleza wimbi lao la kufunga Mabao mengi kila Mechi baada ya Jumapili iliyopita kushusha kipigo cha kwanza kwenye Ligi kwa vinara wa Ligi Chelsea Uwanjani Stamford Bridge walipoifunga 3-2 lakini Siku 3 baadae, Jumatano, Chelsea walilipa kisasi kwa kuifunga Man United, iliyochezesha Kikosi cha Pili,  bao 5-4, kwenye Mechi ya Kombe la Ligi iliyochukua Dakika 120 baada ya kutoka 3-3 katika Dakika 90.
Katika Mechi 8 za mwisho kucheza Old Trafford, Arsenal hawajashinda hata moja baada ya kuchapwa na Man United katika Mechi 7 kati ya hizo na sare 1 tu.
Kimsimamo kwenye Ligi, Arsenal wapo nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 15 na Man United wapo nafasi ya pili, Pointi moja nyuma ya vinara Chelsea, na wana Pointi 21.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
USO kwa USO-Man United v Arsenal:
-WAMECHEZA JUMLA MECHI: 214
-Arsenal: Ushindi: 78
-Man United: Ushindi 90
-Sare: 46
NYUMBANI kwa Arsenal: Mechi 101
-Arsenal: Ushindi: 57
-Man United: Ushindi 27
-Sare: 17
NYUMBANI kwa Man United: Mechi 102
-Man United: Ushindi 60
-Arsenal: 17
-Sare: 25
MATOKEO Misimu ya hivi karibuni:
2011/12:
Januari 22-Arsenal 1 Man United 2 [BPL]
Agosti 28-Man United 8 Arsenal 2 [BPL]
2010/11:
Mei 1-Arsenal 1 Man United 0 [BPL]
Machi 12-Man United 2 Arsenal 0 [FA Cup]
Desemba 13-Man United 1 Arsenal 0 [BPL]
2009/10
Januari 31-Arsenal 1 Man United 3 [BPL]
Agosti 29-Man United 2 Arsenal 1 [BPL]
2008/9:
Mei 16-Man United 0 Arsenal 0 [BPL]
Mei 5-Arsenal 1 Man United 3 [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Aprili 29-Man United 1 Arsenal 0 [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Novemba 8-Arsenal 2 Man United 1 [BPL]
2007/8:
Aprili 13-Man United 2 Arsenal 1 [BPL]
Februari 16-Man United 4 Arsenal 0
Novemba 3-Arsenal 2 Man United 2
REKODI-Mabao Mengi:
-2011/12: Man United 8 Arsenal 2
-1946/47: Arsenal 6 Man United 2
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments:

Post a Comment