Wednesday, January 30, 2013

KIGWA ALL STARZ FC WAFANYA UCHAGUZI WAO JANA JAN.29,2013 KULE WILAYANI UYUI.


Timu ya kigwa all starz jana january 29,2013 ilifanya uchaguzi w aviongozi ndani ya klabu hiyo wilayani uyui  tayari kwa kushiriki ligi daraja la nne mkoani tabora ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia mwezi wa pili mpaka mwezi wa tatu.

Uchaguzi huo jana ulihudhuriwa na wajumbe 20 wakiongozwa na katibu wa chama cha FAU wilayani humo na mjumbe wa kamati tendaji mkoani tabora TAREFA BW.James erick kabepele ,viongozi waliochaguliwa hiyo jana katika nafasi ya mwenyekiti alichaguliwa masinde jonas,na nafasi ya makamu mwenyekiti alichaguliwa mrisho sinundo,kalangu magayu alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa klabu hiyo na katika nafasi ya katibu msaidizi alichaguliwa swalehe bilali.

Viongozi wengine waliochaguliwa ni pamoja na hamis mpuma mtunza pesa za klabu na anania lameck alichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu,na katika nafasi ya kamati ya utendaji walichaguliwa abeid hassan,salum kaswiza,pamoja na minazi rashid.na katika nafasi ya mwakilishi wa klabu kwa upande wa kinamama alichaguliwa ndugu farida ismail.

Katika uchaguzi huo wanachama wa klabu waliadhimia kuwachagua wazee wa timu ili iweze kuwa na taswira ya kisoka nao ni pamoja na sheikh sadala,donard nhwale,,zyagi mmanywa,karenga,msemo,mussa mrisho na wilbert kayanda.

Na makocha wa timu hiyo walichaguliwa akina mnazi rashidy,na kocha na msaidizi ni hussein kitala na makapteni w atimu hiyo ni kulwa jarufu na rashidy majaliwa.

No comments:

Post a Comment