PONGEZI KWA KOCHA WA BARCA VILANOVA AANZA KAZI RASMI.
MENEJA wa klabu ya
Barcelona, Tito Vilanova amerejea mapema kuliko ilivyotegemewa na
kuonekana mazoezini jana kwa mara ya kwanza toka alipofanyiwa upasuaji
wa koo wiki mbili zilizopita. Kocha
huyo mwenye umri wa miaka 44 alihitaji upasuaji mwingine kufuatia
upasuaji aliofanyiwa mara ya kwanza kuondoa uvimbe wa kansa katika koo
lake Novemba 2011 na msaidizi wake Jordi Roura kuchukua nafasi yake
wakati akijiuguza. Vilanova
alitegemewa kurejea tena uwanjani katikati ya Januari lakini
aliwatembelea wachezaji jana asubuhi na baadae kuwasimamia wachezaji
mazoezini katika kipindi cha mchana. Wachezaji
wengi katika kikosi hicho walikuwa hawapo kwasababu ya mchezo wa
kirafiki dhidi ya Nigeria huku nyota wengine wakiwa ndege zao zikiwa
zimechelewa kufika wakati wakitoka katika mapumziko ya sikukuu za Noel
na mwaka mpya.
No comments:
Post a Comment