KIPA NAMBA MOJA WA ZAMANI WA URUGUAY AFARIKI DUNIA.
GOLIKIPA wa zamani wa
kimataifa wa Uruguay, Ladislao Mazurkiewicz amefariki dunia akiwa na
umri wa miaka 67 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Golikipa
huyo alikimbizwa hospitalini wiki iliyopita kutokana na matatizo ya
kushindwa kupumua vizuri lakini hali yake ilishindwa kutengemaa na kuaga
dunia. Mazurkiewicz
anachukuliwa kama mmoja wa makipa bora kuwahi kutokea duniani huku
akikumbukwa zaidi kwa kiwango cha hali ya juu alichokionyesha katika
michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Mexico mwaka 1970. Nyota
huyo enzi zake alijikusanyia mataji mengi akiwa ameshinda mataji matatu
ya ya Ligi Kuu nchini Brazil, Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini
na Kombe la Intercontinental mwaka 1966 pamoja na Kombe la Ligi akiwa na
klabu ya Atletico Mineiro ambayo kwasasa nyota wa Brazil Ronaldinho
ndipo anapocheza.
No comments:
Post a Comment