>>FA YAWAANDIKIA BARUA REDKNAPP & MANCINI KUJIELEZA!!
>>FERGIE AMPANDISHIA PARDEW!!
WAKATI
FA, Chama cha Soka England, kimethibitisha kuwaandikia Barua za
kuwataka kujieleza, Mameneja wa Man City na QPR, Roberto Mancini na
Harry Redknapp, kufuatia kauli zao baada ya Mechi zao za kulalamika
kuhusu Marefa na kudokeza uchezeshaji usio wa haki, Mameneja wa Arsenal,
Arsene Wenger, na wa Newcastle, Alan Pardew, wamesema Sir Alex Ferguson
alistahili Kadi Nyekundu kwa kubishana na Marefa kwenye Mechi kati ya
Manchester United na Newcastle iliyochezwa Boxing Dei.
Akijiingiza kwenye mzozo huo, Arsene
Wenger amesema Sir Alex Ferguson alipaswa kuadhibiwa na Refa Mike Dean
kwa kitendo chake cha kabla Kipindi cha Pili kuanza kwenye Mechi kati ya
Manchester United na Newcastle cha kumvaa Refa Mike Dean na
kumlalamikia kisha kumkabili Refa wa Akiba Neil Swarbrick na pia Refa
Msaidizi Jake Collin.
Katika Mechi hiyo ambayo Man United
walishinda Bao 4-3, Ferguson alikuwa amekasirishwa na Refa Mike Dean
kufuta Ofsaidi iliyotolewa ishara na Msaidizi wake Jake Collin na kuamua
ni Bao kwa vile Jonny Evans alijifunga mwenyewe.
Wakati Kipindi cha Pili kinataka kuanza,
Ferguson alimvaa Refa Mike Dean na kumlalamikia kisha akamvaa Refa wa
Akiba Neil Swarbrick na pia Refa Msaidizi Jake Collin.
Lakini FA ilithibitisha jana kuwa Sir
Alex Ferguson hatachukuliwa hatua yeyote kwa vile Refa Mike Dean
hakutaja lolote kwenye Ripoti yake ya Mechi.
Wenger amesema Sheria ni msumeno na Refa Mike Dean alipaswa kumwadhibu Ferguson.
Arsene Wenger ashawahi kukumbana na Kadi
Nyekundu toka kwa Refa Mike Dean Agosti 2009 alipotolewa Uwanjani kwa
kuipiga teke chupa ya maji wakati Arsenal inachapwa 2-1 na Man United
Uwanjani Old Trafford.
WAKATI HUO HUO, Sir
Alex Ferguson amemshambulia Meneja wa Newcastle, Alan Pardew kwa kutamka
kuwa alipaswa kupewa Kadi Nyekundu kwa kubishana na Refa Mike Dean na
Wasaidizi wake wakati Newcastle ilipochapwa 4-3 na Man United Uwanjani
Old Trafford.
Ferguson amejibu mapigo kwa kusema:
“Alan Pardew amejitokeza na kuniponda mimi. Yeye ndio mbaya zaidi kwa
kuvamia Marefa, anadiriki hata kuwasukuma na kisha analeta mzaha kuhusu
hilo! Ameshasahau msaada niliompa!”
Ferguson ameongeza: “Sikufanya kosa!
Sikutoa kashfa yeyote! Nlikuwa nikiongea na Refa tu! Tatizo ni kuwa tupo
Klabu kubwa na mimi ni Meneja wa Klabu kubwa Duniani hivyo kila kitu
kinakuzwa! Sio Newcastle Klabu ndogo iliyo huko Kaskazini Mashariki!”
Pardew aliwahi kufungiwa Mechi mbili na
kudundwa Faini ya £20,000 kwa kumsukuma Refa Msaidizi wakati Newcastle
inaifunga 2-1 Tottenham Hotspur hapo Tarehe 18 Agosti.
HIVI PUNDE TU, FA,
Chama cha Soka England, kimethibitisha kuwaandikia Barua za kuwataka
kujieleza, Mameneja wa Man City na QPR, Roberto Mancini na Harry
Redknapp, kufuatia kauli zao baada ya Mechi zao za kulalamika kuhusu
Marefa na kudokeza uchezeshaji usio wa haki, kitendo ambacho ni kinyume
cha Kanuni za FA.
Mancini, Meneja wa Man City, alilalamika
kuhusu Refa Kevin Friend baada kufungwa 1-0 na Sunderland kwenye Mechi
ya Ligi Kuu England iliyochezwa Desemba 26 kwa Refa huyo kutopiga
Filimbi ya Faulo aliyochezewa Mchezaj wake Pablo Zabaleta na badala yake
kuachia mpira uchezwe na kuzaa Goli la Adam Johnson, Winga wa zamani wa
Man City, lililowaua City 1-0.
Mancini alidai: “Pengine Refa alivimbiwa na Mlo wa Krismasi! Haiwezekani Waamuzi wawili wasione tukio hilo! [Akimaanisha Refa Na Msaidizi wake]”
Nae Harry Redknapp, Bosi wa QPR, yuko
matatani baada ya kuhamaki na maamuzi ya Refa Chris Foy ambayo alidai ni
‘Skandali!’ wakati walipofungwa 2-1 na West Brom na kutupwa mkiani mwa
Ligi Kuu England Siku ya Boxing Dei.
Refa Chris Foy alilikubali Goli la
kujifunga mwenyewe Kipa Robert Green ambae alionekana akibanwa waziwazi
na Mchezaji wa WBA, Marc-Antoine Fortune, na pia aliwayima Penati ya
wazi mwishoni baada ya Beki Liam Ridgewell kuunawa mpira.
Redknapp amewaka: "Ile ni Faulo ya wazi kwa Kipa wetu na ile ni Penati ya wazi! Hii ni kashfa!”
Msimamo wa FA kwa Mameneja ni kwamba
hawatakiwi kuwalaumu Marefa kuhusu maamuzi yao na wakifanya hivyo
wanaandikiwa Barua kutaka maelezo yao na kama hayaridhishi hufunguliwa
Mashitaka.
No comments:
Post a Comment