FAINALI za shindano la
kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kipekee ‘Unique Model’ kwa mwaka 2012
zinatarajiwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa New Maisha Club uliopo Oyesterbay
jijini Dar es Salaam ambapo warembo 12
watachuana kuwania taji hilo.
Mkurugenzi wa Unique Entertainment inayoandaa shindano hilo,
Methuselah Magese alisema kwamba maandalizi ya shindano hilo yamekamilika,
hivyo amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia fainali hizo.
Alisema shindano hili linatarajiwa kuwa na ushi ndani
mkubwa kutokana na washiriki wake kuwa na viwango vya hali ya juu hali
itakayowapa mtihani mkubwa majaji katika maamuzi yao.
Magese aliwataja washiriki
hao ni Janecy Maluli,Judith Sangu,Vestina Charles,Catherine Masumbigana,Darling
Godfrey,Amina Ayoub,Elizabeth Pertty,Lulu Mramba ,Sadory Kendra,Elizabeth
Borniface na Zeenarth Habib ambao walikuwa kambini kwenye hoteli ya Lamada kwa
wiki mbili chini ukufunzi wa Wancy Nells kwa upande wa miondoko na Denis Lucas kwa
upande wa shoo.
Aidha, Magesa alisema tayari Baraza
la sanaa la Taifa (BASATA) limeteuwa majina matatu ya majaji watakaoshiriki katika kumchagua mshindi wa
taji hilo linoloshikiliwa na Asia Dachi kuwa ni wabunifu Asia
Idarous Khamsini,Gymkhana Hilall
‘paka wear’ na Martin Kadinda ‘Singo Button’.
Shindano hilo limedhaminiwa
na Giraffe Ocean view Totel,Kitwe General Traders,Sophanaa Investment ltd,Dtv,88.4
clouds fm,Magazeti ya Tanzania Daima na Kiu,Mashujaa
Investment Ltd,Blogu za Michuzi,jiachie,Mtaa kwa Mtaa, Unique Entertainment,, Lamada
Apartments & Hotel, Fabak fashions,Genessis Health Center na Yung don
Records,Paka Wear na Mtoko Design litapambwa na burudani toka bendi ya mashujaa
ikiongozwa na rapa maarufu Chalz Baba, msanii wa ngoma za asili toka kwa Costa
Siboka na msanii wa bongo flava B-shop.
No comments:
Post a Comment