BAADA YA KUPANDIKIZIWA INNI JINGINE ABIDAL ASEMA YUPO FITI
BEKI wa Barcelona Eric
Abidal amesema anajisikia vyema na yuko tayari kurejea tena uwanjani
ikiwa ni miezi nane imepita toka afanyiwe upasuaji wa kupandikizwa ini
jingine. Akihojiwa
Abidal mwenye umri wa miaka amesema ni muda mwingi umepita toka
afanyiwe upasuaji na amekuwa akipambana ili aweze kurejea katika hali
yake kawaida. Abidal
alifanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini jingine April 10 ikiwa ni mwaka
mmoja toka alipoondolewa uvimbe wa kansa katika ini lake Machi 2011. Beki
huyo alianza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake Desemba 19 siku
ambayo ndiyo taarifa za kocha wa klabu Tito Vilanova kurudiwa na tatizo
la kansa ya koo zilipotangazwa. Vilanova
naye alifanyiwa upasuaji mwingine wa kuondoa uvimbe huo wa kansa na
baadae kuruhusiwa kutoka hospitali ambapo kwasasa anaendelea na matibabu
ya mionzi kwa kipindi cha wiki sita.
No comments:
Post a Comment