Thursday, November 29, 2012

ZANZIBAR YAIKALISHA RWANDA NAMBOOLE

Khamis Mcha ‘Vialli’ akiruka kushangilia baada ya kufunga bao la kwanza. Kushoto ni Jaku Juma.


MABAO mawili ya kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ usiku huu yameipa Zanzibar ushindi wa 2-1 dhidi ya Rwanda, katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
Kwa ushindi huo, Zanzibar Heroes imefufua matumaini ya kwenda Robo Fainali ya michuano hii, ikipanda kileleni mwa Kundi hilo, kwa pointi zake nne, Rwanda ikishuka nafasi ya pili kwa pointi zake tatu, sawa na Malawi, wakati Eritrea inashika mkia kwa pointi yake moja.
Vialli alifunga mabao yake moja kila kipindi, la kwanza dakika ya sita na la pili dakika ya 61, yote akionyesha yeye ni fundi na mwenye akili na maarifa ya soka kutokana na kutulia na kumtungua kipa hodari kabisa katika ukanda huu, Jean Claude Ndoli.
Rwanda ilipata bao lake kupitia kwa Dadi Birori dakika ya 79, ambaye aliingia uwanjani dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Tumaine Ntamuhanga.
Mchezo wa leo kama ulivyokuwa mchezo wa kwanza kati ya Malawi na Eritrea ulitibuliwa na mvua iliyoharibu mandhari ya Uwanja wa Mandela, hivyo haikuwa wa ufundi zaidi ya ‘butua butua’.
Nahodha wa Zanzibar, Nadir Heroub ‘Cannavaro’ alisema baada ya mechi hiyo kwamba wamefuta makosa yao ya mchezo wa kwanza na sasa Wazanzibari wasubiri Kombe, wakati Haruna Niyonzima wa Rwanda, alilalamikia Uwanja mbovu leo kuwasababisha kucheza ovyo.  
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Zanzibar kilikuwa; Mwadini Ally, Nassor Masoud ‘Cholo’, Samir Hajji Nuhu, Aggrey Morris, Nadir Haroub Ali 'Canavaro, Sabri Ali, Khamis Mcha 'Vialli', Abdulaghan Gulam, Jaku Juma, Seif Abdallah/Adeyom Saleh Ahmed dk88 na Suleiman Kassim ‘Selembe’.
Rwanda; Jean Claude Ndoli, Emery Bayisenge, Hamdani Bariyanga, Ismail Nshutiyamagara, Mwemere Ngirishuti/Jean Claude Iranzi dk46, Jean Baptiste Mugiraneza, Haruna Niyonzima, Jimmy Mbagara, Jerome Sina, Jean D’Amour Uwimana/Fabrice Twagizimana dk24 na Tumaine Ntamuhanga/Dadi Birori dk66.


MSIMAMO KUNDI C:
                     P   W  D   L    GF GA GD Pts
Zanzibar        2    1    1    0    2    1    1    4
Rwanda         2    1    0    1    3    2    1    3
Malawi           2    1    0    1    3    4    -1  3
Eritrea           2    0    1    1    2    3    -1  1

Beki wa Zanzibar, Nassor Masoud 'Chollo' akiondoka na mpira mbele ya kiungo wa Rwanda, Haruna Niyonzima

Kikosi cha Rwanda leo

Kikosi cha Uganda leo

Vialli kushoto akishangilia bao lake la pili, kulia ni Suleiman Kassim 'Selembe' 

Wachezaji wa Zanzibar wakishangilia bao la pili kwa staili ya kupiga kasia

 

BUNDESLIGA: TAJI la Dortmund hatihati!!

>>MTANANGE Jumamosi ALLIANZ ARENA: Bayern v Dortmund!!
BORUSSIA_DORTMUND_JUKWAAMabingwa watetezi Borussia Dortmund wanasafiri kwenda Munich Wikiendi hii kuwavaa vinara wa Bundesliga Bayern Munich wakiwa Pointi 11 nyuma yao na wanajua wazi matokeo mengine yeyote bila ya ushindi ni kuwa Taji lao ‘kwishnei!’
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 14]
1 Bayern Munich Pointi 37
2 Bayer Leverkusen 27
3 Borussia Dortmund 26
4 Schalke 24
5 Eintracht Frankfurt 24
6 Hannover 20
7 Mainz 20
+++++++++++++++++++++++
Ingawa kuna Mechi nyingi tu zimebaki na wao wakiwa nafasi ya 3, Kocha wa Mabingwa Borussia Dortmund, Juergen Klopp, anafahamu fika Jumamosi wanahitaji ushindi kwa kila hali.
Kitu cha kutia moyo kwa Borussia Dortmund ni kuwa wameifunga Bayern Munich katika Mechi 4 kati ya 5 walizocheza nao mwisho na Mechi waliyopteza ni ile waliyocheza mwishoni ambayo Bayern walitwaa German Super Cup mwanzoni mwa Msimu huu.
Lakini Bayern ya Msimu huu ni kali na wamefungwa Bao 5 tu Msimu huu kwenye Bundesliga.
RATIBA:
Ijumaa Novemba 30
Fortuna Dusseldorf v Eintracht Frankfurt
Jumamosi Desemba 1
Bayern Munich v Borussia Dortmund
Schalke v Borussia Monchengladbach
Mainz v Hannover
SpVgg Gr. Furth v Stuttgart
Augsburg v Freiburg
Bayer Leverkusen v Nuremberg
Jumapili Desemba 2
Hoffenheim v Werder Bremen
Wolfsburg v Hamburger
+++++++++++++++++++++++
 

CECAFA CHALLENGE CUP 2012: Zenji yashinda, yashika hatamu Kundi C!!

>>IJUMAA: Lala salama Kundi A!
CECAFA_TUSKER_CUP_2012Kwenye michuano ya kusaka Nchi Bingwa ya Afrika Mashariki na ya Kati, CECAFA TUSKER CHALENJI CUP 2012 inayoendelea huko nchini Uganda, Zanzibar Heroes leo wamejiweka nafasi nzuri kutinga Robo Fainali kutoka Kundi C baada ya kuichapa Malawi Mabao 2-1 na kutwaa uongozi wa Kundi hilo.
MABAO mawili ya Zanzibar yalifungwa na Kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 6 na 61, na la Rwanda limefungwa na Dadi Birori dakika ya 79.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
MAKUNDI:
KUNDI A: Uganda, Ethiopia, Kenya, South Sudan
KUNDI B: Sudan, Tanzania, Burundi, Somalia
KUNDI C: Rwanda, Malawi, Zanzibar, Eritrea
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Katika Mechi nyingine ya Kundi C, Malawi iliifunga Eritrea Bao 3-2 kwa Bao za Chiukepo Msowoya, Miciam Mhone na Patrick Masanjala na yale ya Eritrea kufungwa na Amir Hamad Omary na Yosief Ghide kwa penalti.
Michuano hii itaendelea Ijumaa Novemba 30 kwa Mechi za mwisho za Kundi A kwa Mechi za Kenya v Ethiopia na Uganda v South Sudan.
RATIBA/MATOKEO:
KUNDI A:
Novemba 24:  Ethiopia 1 South Sudan 0, Uganda 1 Kenya 0
Novemba 27: South Sudan 0 Kenya 2, Uganda 1 Ethiopia 0
Novemba 30: Kenya v Ethiopia,  South Sudan v Uganda
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 2]
1 Uganda Pointi 6
2 Kenya 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3 Ethiopia 3 [Tofauti ya Magoli: 0]
4 South Sudan 0
KUNDI B:
Novemba 25: Burundi 5 Somalia 1, Tanzania 2 Sudan 0
Novemba 28: Somalia 0 Sudan 1, Tanzania 0 Burundi 1
Desemba 1: Sudan v Burundi, Somalia v Tanzania
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 2]
1 Burundi Pointi 6
2 Kili Stars 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3 Sudan 3 [Tofauti ya Magoli: -1]
4 Somalia 0
KUNDI C:
Novemba 26: Zanzibar 0 Eritrea 0, Rwanda 2 Malawi 0
Novemba 29: Malawi 3 Eritrea 2, Rwanda 1 Zanzibar 2
Desemba 1: Malawi v Zanzibar, Eritrea v Rwanda
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 2]
1 Zanzibar Pointi 4
2 Rwanda 3 [Tofauti ya Magoli: 1]
3 Malawi 3 [Tofauti ya Magoli: -1]
3 Eritrea 1
FAHAMU: Washindi wawili wa juu wa kila Kundi pamoja na Timu mbili zitakazoshika nafasi za 3 Bora zitaingia Robo Fainali.
ROBO FAINALI: Desemba 3 & 4
NUSU FAINALI: Desemba 6
FAINALI: Desemba 8
 

FIFA KLABU BINGWA DUNIANI: Chelsea yatangaza Kikosi kwenda Japan!!

>>CHELSEA kucheza Desemba 13 na Mshindi Usain Hyundai v Monterrey!!
>>BARANI ASIA: MCHEZAJI BORA 2012==SHINJI KAGAWA!
CHELSEA_ULAYA_2012AWakati Chelsea inatangaza Kikosi chake cha kwenda Japan kuwania kuwa Klabu ya pili toka England, baada ya Manchester United, kutwaa Kombe la Dunia kwa Klabu, Nchi hiyo Japan na Klabu ya Manchester United imetoa Mchezaji Bora Barani Asia kwa Wachezaji wa Kimataifa, Tuzo ambayo ni mara ya kwanza kutolewa, na Mshindi huyo ni Shinji Kagawa.
CHELSEA
Kocha wa muda wa Chelsea, Rafael Benitez, ametangaza Kikosi kikali kwa ajili ya Michuano ya kuwania Taji la FIFA la Klabu Bingwa Duniani ambayo wao wataanza kucheza hatua ya Nusu Fainali dhidi ya Mshindi kati ya Bingwa wa Barani Asia, Usain Hyundai kutoka Korea na Monterrey, ambao ni Mabingwa wa Marekani ya Kati na Kaskazini.
Kikosi cha Chelsea kina Majina yote makubwa wakiwemo Nahodha wao John Terry na Frank Lampard ambao wote bado wamo kwenye Listi yao ya sasa ya Majeruhi wao.
Meneja Rafael Benitez ana uzoefu mkubwa kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Duniani kwani hii itakuwa mara yake ya 3 kushiriki ambapo aliipeleka Liverpool Mwaka 2005 na kutolewa Fainali na 2010, aliiongoza Inter Milan, iliyofikishwa huko na Jose Mourinho, kutwaa Ubingwa wa Dunia.
KIKOSI KAMILI:
Makipa: Petr Cech, Ross Turnbull, Hilario
Mabeki: Branislav Ivanovic, Ashley Cole, David Luiz, Paulo Ferreira, Gary Cahill, John Terry, Cesar Azpilicueta, Ryan Bertrand
Viungo: Oriol Romeu, Ramires, Frank Lampard, Oscar, John Obi Mikel, Eden Hazard, Marko Marin, Lucas Piazon
Mafowadi: Fernando Torres, Juan Mata, Victor Moses, Daniel Sturridge
BARANI ASIA: MCHEZAJI BORA 2012==SHINJI KAGAWA!
KAGAWA_N_GIL
Kiungo wa Japan na Manchester United Shinji Kagawa ametwaa Tuzo ya kwanza kabisa kutolewa na Shirikisho la Soka Barani Asia, AFC, ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2012 kwa Wachezaji wa Kimataifa, wale wanaocheza nje ya Asia.
Katika kutwaa Tuzo hiyo Shinji Kagawa aliwashinda Yuto Nagatomo wa Japan anaecheza Klabu ya Inter Milan na Kipa Veterani wa Australia anaechezea Fulham, Mark Schwarzer.
Washindi hao walitajwa huko Kuala Lumpur, Malaysia hii leo.
Mchezaji wa Korea ya Kusini, anaechezea Klabu Bingwa ya Asia, Lee Keun-ho, ndie Mchezaji Bora kwa Wachezaji wanaocheza ndani ya Asia.
Lee aliwashinda Kiungo wa Iran Ali Karimi na Beki wa China Zheng Zhi.
Katika Tuzo nyingine mpya anayozawadiwa Mchezaji wa kutoka nje ya Asia anaecheza Asia Mshindi ni Mbrazil Rogerio De Assis Silva Coutinho wa Klabu ya United Arab Emirates Al Jazira.
KLABU BINGWA DUNIANI 2012
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea-BINGWA ULAYA
Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI
Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI
Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA
Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia
Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika
Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI
RATIBA:
Raundi ya Mchujo - Desemba 6, Yokohama
1 Sanfrecce Hiroshima v Auckland City
ROBO FAINALI - Desembar 9, Toyota
2 Usain Hyundai  v Monterrey
3 MSHINDI Mechi Na 1 v Al Ahly
MSHINDI wa 5- Desemba 12, Toyota
Aliefungwa Robo Fainali 1 v Aliefungwa Robo Fainali 2
NUSU FAINALI
Desemba 12, Toyota
5 Mshindi Mechi Na 3 v Corinthians
Desemba 13, Yokohama
6 Mshindi Mechi Na 2  v Chelsea
MSHINDI wa 3 - Desemba 16, Yokohama
FAINALI - Desemba 16, Yokohama

No comments:

Post a Comment