ARUDI KOCHA BRAZIL: BIG PHIL kwa ajili ya 2014 World Cup!!
>> CARLOS ALBERTO PARREIRA Mkurugenzi Ufundi!!
>>MECHI ya KWANZA kuivaa England Februari 2013!!
Luiz
Felipe Scolari ameteuliwa kuwa Kocha wa Brazil ikiwa ni mara yake ya
pili baada ya Kocha huyo, aliewahi kuzifundisha Chelsea na Portugal,
kuiongoza Brazil Mwaka 2002 kutwaa Kombe la Dunia lililochezwa huko
Nchini Japan na Korea ya Kusini.
Scolari, Miaka 64, amembadili Mano Mezes
alietimuliwa Wiki iliyopita na sasa ataiongoza Nchi yake kwenye Fainali
za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 zitazochezwa Nchini Brazil.
+++++++++++++++++++++++++++
MAFANIKIO ya SCOLARI KIMATAIFA:
-2002: ATWAA Kombe la Dunia na Brazil walipoifunga Germany 2-0 Fainali.
-2004: AFIKA Fainali Euro 2004 akiwa na Portugal, wafungwa 1-0 na Greece
-2006: AIONGOZA Portugal kushika Nafasi ya 4 Kombe la Dunia
+++++++++++++++++++++++++++
Mkongwe Carlos Alberto Parreira,
aliewahi kuwa Kocha wa Brazil, ameteuliwa kumsaidia Scolari na amepewa
wadhifa wa Mkurugenzi wa Ufundi.
Scolari, akipokea uteuzi huo, alisema: “Sina presha, nina furaha! Nimemshukuru Rais wa FA mara 1000 kwa kuniteua!”
Mwaka 2001, Scolari aliinusuru Brazil
katika janga la kutofuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka
wakati walipokuwa wakifanya vibaya kwenye Mechi za Mchujo na hatimae
kuifikisha Fainali alipopewa Timu na pia kutwaa Ubingwa wa Dunia.
FIFA Ballon d’Or 2012: NI RONALDO, INIESTA & MESSI!
>>KOCHA BORA: DEL BOSQUE, GUARDIOLA & MOURINHO!
>>MAFOWADI 15 FIFA/FIFPro World XI 2012 wamo ROONEY, RVP, SUAREZ, AGUERO, BALOTELLI, DROGBA, ETO’O!!
>>GOLI BORA: NEYMAR, FALCAO & STOCH!!
Wagombea
wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2012, FIFA Ballon d’Or,
wametangazwa leo na FIFA huko Anhembi Convention Center Mjini Sao Paulo,
Brazil katika Mkutano uliohudhuriwa na Viongozi wa FIFA, akiwemo Rais
wao, Sepp Blatter na Katibu Mkuu Jerome Valcke na pia Mchezaji Nguli wa
Brazil, Ronaldo, na Wachezaji watatu waliotajwa kugombea Tuzo hiyo ni
Cristiano RONALDO, Portugal, Andres INIESTA, Spain na Lionel MESSI,
Argentina.
Kwa upande wa Kinamama, Wagombea ni MARTA, Brazil, Alex MORGAN, USA na Abby WAMBACH, USA.
Sambamba na hao, pia zilitajwa Listi za Wagombea Tuzo nyingine ambao ni:
KOCHA BORA kwa Wanaume:
-Vicente DEL BOSQUE, Spain (Spain)
-Pep GUARDIOLA, Spain (FC Barcelona)
-Jose MOURINHO, Portugal (Real Madrid)
KOCHA Bora kwa Wanawake:
-Bruno BINI, France (France)
-Norio SASAKI, Japan (Japan)
-Pia SUNDHAGE, Sweden (USA)
Wagombea hao wa Tuzo hizo walipatikana
kwa Kura za Manahodha na Makocha wa Timu za Taifa za Wanaume na Wanawake
pamoja na Wawakilishi wa Wanahabari walioteuliwa na Gazeti la France
Football ambao ni Washirika wa FIFA katika Tuzo hizi.
Pamoja na hao pia yalitangazwa Majina ya Wagombea wa Goli Bora, wanaowania Tuzo ya FIFA Puskás ambao ni:
- FALCAO (América de Cali-Atletico Madrid, 19 May 2012)
-NEYMAR (Santos-Internacional, 7 March 2012) –
-Miroslav STOCH (Fenerbahçe-Gençlerbirliği, 3 March 2012).
Pia, yalitangazwa Majina ya Fowadi 15
ambao wanaungana na Makipa watano, Mabeki 20, na Viungo 15,
waliotangazwa kabla, kufanya jumla ya Wachezaji 55 watakaowania nafasi
11 za kuwemo kwenye Listi ya Wachezaji 11 watakauonda Timu Bora Duniani,
FIFA/FIFPro World XI 2012, yenye Kipa mmoja, Mabeki wanne, Viungo
watatu na Mafowadi watatu.
LISTI HIYO ya Wachezaji 55:
WALIOTEULIWA HADI SASA:
MAKIPA 5 WALIOTEULIWA:
-Gianluigi Buffon (Italy, Juventus)
-Iker Casillas (Spain, Real Madrid)
-Petr Cech (Czech Republic, Chelsea)
-Joe Hart (England, Manchester City)
-Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich).
MABEKI 20:
-Jordi Alba (Spain, Barcelona)
-Gareth Bale (Wales, Tottenham Hotspur)
-Giorgio Chiellini (Italy, Juventus)
-Ashley Cole (England, Chelsea)-
-Dani Alves (Brazil, Barcelona)
-David Luiz (Brazil, Chelsea)
-Patrice Evra (France, Manchester United)
-Rio Ferdinand (England, Manchester United)
-Mats Hummels (Germany, Borussia Dortmund)
-Branislav Ivanovic (Serbia, Chelsea)
-Vincent Kompany (Belgium, Manchester City)
-Philipp Lahm (Germany, Bayern Munich)
-Marcelo (Brazil, Real Madrid)
-Javier Mascherano (Argentina, Barcelona)
-Pepe (Portugal, Real Madrid)
-Gerard Piqué (Spain, Barcelona)-
-Carles Puyol (Spain, Barcelona)
-Sergio Ramos (Spain, Real Madrid)
-John Terry (England, Chelsea)
-Thiago Silva (Brazil, Paris St-Germain).
VIUNGO 15:
-Xabi Alonso (Spain / Real Madrid),
-Sergio Busquets (Spain / FC Barcelona),
-Cesc Fabregas (Spain / FC Barcelona),-
-Steven Gerrard (England / Liverpool)
-Eden Hazard (Belgium / Chelsea)
-Andres Iniesta (Spain / FC Barcelona)
-Frank Lampard (England / Chelsea)
-Luka Modric (Croatia / Real Madrid)
-Mesut Özil (Germany / Real Madrid)
-Andrea Pirlo (Italy / Juventus)
-Franck Ribery (France / Bayern Munich)
-David Silva (Spain / Manchester City)
-Bastian Schweinsteiger (Germany / Bayern Munich)
-Yaya Touré (Ivory Coast / Manchester City)
-Xavi Hernandez (Spain / FC Barcelona)
MAFOWADI 15:
-Sergio Agüero (Argentina, Manchester City)
-Mario Balotelli (Italy, Manchester City)
-Karim Benzema (France, Real Madrid)
-Edinson Cavani (Uruguay, AS Napoli)
-Didier Drogba (Ivory Coast, Shanghai Shenhua)
-Samuel Eto’o (Cameroon, Anzhi Makhachkala)
-Radamel Falcao (Colombia, Atletico Madrid)
-Mario Gomez (Germany, Bayern Munich)
-Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Paris Saint-Germain)
-Lionel Messi (Argentina, Barcelona)
-Neymar (Brazil, Santos)
-Robin van Persie (The Netherlands, Manchester United)
-Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid)
-Wayne Rooney (England, Manchester United)
-Luis Suarez (Uruguay, Liverpool)
Washindi wote wa Tuzo hizi watatangazwa huko Kongresshaus Mjini Zurich, Uswsisi hapo 7 January 2013.
TAIFA QUEENS YAPAA LEO KWENDA SINGAPORE KUSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA YA MABARA
TIMU ya Taifa ya Netiboli ‘Taifa Queens’ imeondoka nchini leo saa tisa kuelekea nchini Singapore kwenye michezo ya kimataifa inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho kutwa na kumalizika Disemba 8 mwaka huu nchini humo.
Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 12 pamoja na viongozi wawili kimeagwa leo na kukabidhiwa bendera na Naibu Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo Juliana Yasoda.
Akizungumza na jijini mara baada ya kuagwa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Rose Mkisi alisema kuwa timu hiyo imeongozana na Mwenyekiti wa CHANETA na Daktari katika safari hiyo.
Mkisi alisema timu ikitua itaendelea na mazoezi baada ya mapumziko ya siku moja.
Kikosi hicho kinachoundwa na wachezaji kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kilipata maandalizi ya kutosha baada ya kukaa kambini mjini Morogoro kujiandaa na michuano hiyo.
Mkisi aliongeza kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kufanya vizuri katika michuano zinazoshiriki timu kutoka kwenye shirikisho la Kimataifa la Netiboli (IFNA) kwa nchi itakayofanya vizuri ambapo Tanzania ipo nafasi ya tatu kwa Kanda ya Afrika.
PETER TINO "THE STRIKER" AKABIDHI SERENGETI BOYS BENDERA NA UJUMBE MZITO WA KWENDA KUIVAA CONGO BRAZAVILLE
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa Taifa Stars Peter Tino jana usiku aliwakabidhi timu ya Taifa ya vijana waliochini ya miaka 17 "Serengeti boys" bendera na ujumbe mzito.
Tino ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye halfa hiyo aliwaasa wachezaji kucheza kwa kujituma wakijua kuwa nyuma yao kuna watanzania wanawafatilia na ndio maana wamepewa bendera ya taifa kwa sababu wanaiwakilisha nchi.
"Nyie ni jeshi la Tanzania mnakwenda kupigana mkiwa tayari mmeshashinda nyumbani hivyo vyovyote mnatakavyofanyiwa nyie fikirie mchezo tu", alisema Tino.
Pia aliwaambia kwenye mchezo kuna mbinu chafu ambazo zinaweza kutumika ili kuwadhoofisha kisaikolojia ila wasilitilie maanani bali wafikirie mchezo.
"Mchezo wenu ni sawa na mchezo wetu tuliocheza 1980 dhidi ya Zambia na dakika ya 89 mimi niliwanyamazisha Wazambia mbele ya Rais Mugabe baada ya kufunga bao na kufanikiwa kufuzu mataifa ya Afrika, alisema Tino.
Akizungumza na wachezaji Rais wa Shirikisho la Soka nchini Leodgar Chilla Tenga aliwaasa wachezaji wakazingatie kile tu walichofundishwa na kocha kwani anajua mchezo huu utakuwa mgumu
Timu iliondoka na ndege ya shirika la ndege la Kenya na msafara wa watu 27, wachezaji 18 na viongozi tisa huku wakiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele baada ya mchezo wa awali uliochezwa nchini kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Kocha wa timu hiyo, Jacob Michelsen alisema kuwa anajua nakwenda kucheza natimu bora ila wao ni bora pia kwani wana faida ya bao la nyumbani.
"Wachezaji wapo kamili na wana ari ya kushinda mchezo huo na kwa sababu nyumbani tulishinda tunaamini tutashinda pia", alisema Jacob
Serengeti boys ambayo imeundwa na wachezaji chipukizi waliopatokana kutokana na mashindano ya Copa Cocacola wanatamani kushinda mchezo ili waweze kuandika historia ambayo haijawahi kuandikwa hapa nchini.
Serengeti boys wamefika hatua hii baada ya kufuzu hatua ya kwanza baada ya Kenya kujiondoa na hatua pili Misri kujitoa pia
LENZI YA MICHEZO tunawatakia kila la heri mfanikiwe kufuzu fainali za vijana zinazotarajiwa kuchezwa nchini Morocco, Machi mwakani
Ronaldo, Iniesta na Messi WAMETANGAZWA KUWANIA TUZO YA FIFA Ballon d’Or 2012
Watakao wania tuzo ya mwanasoka Bora wa
Dunia ya FIFA Ballon d’Or kwa mwaka 2012 na kwa wanawake wametangazwa
leo hii huko Anhembi Sao Paulo.
Ambapo Rais wa FIFA Joseph S. Blatter,
Katibu mkuu wa fifa Jérôme Valcke, Mkuu wa jarida la L’Equipe na mkuu
wa soka la ufaransa François Morinière, na mchezaji mahiri raia wa
Brazil Ronaldo Luiz Antonio Nazalia De Lima na Marta, ambaye aliwahi
kushinda tuzo hiyo walihudhuria .
Wakiwatajwa kiherufi na kimpangillio watakao wania tuzo hiyo ya FIFA Ballon d’Or Ni Cristiano RONALDO, Ureno (Real Madrid ) , Andres INIESTA, Uispania na Lionel MESSI, Argentina, wakati MARTA, Kutoka Brazil, Alex MORGAN, Kutoka USA na Abby WAMBACH, kutoka USA wao watashindania kwa upande wa wanawake .
kwa upande wa Makocha wanaume ni : Vicente DEL BOSQUE, Uispania, Pep GUARDIOLA, Uispania (FC Barcelona) na Jose MOURINHO, Kutoka Ureno (Real Madrid) kwa upande wa wanawake Bruno BINI, Ufaransa , Norio SASAKI, Japan (Japan) na , Pia SUNDHAGE, raia wa Sweden akifundisha (USA) .
Wachezaji wengine watatu wanaowania goli zuri zaidi kwa maana ya tuzo ya FIFA Puskás : FALCAO alifunga goli katika mechi kati ya (América de Cali-Atletico Madrid, 19 May 2012), NEYMAR kati ya (Santos dhidi -Internacional, 7 March 2012) na Miroslav STOCH kati ya (Fenerbahçe dhidi -Gençlerbirliği, 3 March 2012).
Washindi watapewa zawadi zao katika makao makuu ya FIFA Ballon d’Or Gala huko Kongresshaus Zurich Tarehe 7 January 2013 zawadi nyingine ni Uuungwana Michezoni FAIR PLAY na Tuzo ya Heshima rais wa fifa
Wakiwatajwa kiherufi na kimpangillio watakao wania tuzo hiyo ya FIFA Ballon d’Or Ni Cristiano RONALDO, Ureno (Real Madrid ) , Andres INIESTA, Uispania na Lionel MESSI, Argentina, wakati MARTA, Kutoka Brazil, Alex MORGAN, Kutoka USA na Abby WAMBACH, kutoka USA wao watashindania kwa upande wa wanawake .
kwa upande wa Makocha wanaume ni : Vicente DEL BOSQUE, Uispania, Pep GUARDIOLA, Uispania (FC Barcelona) na Jose MOURINHO, Kutoka Ureno (Real Madrid) kwa upande wa wanawake Bruno BINI, Ufaransa , Norio SASAKI, Japan (Japan) na , Pia SUNDHAGE, raia wa Sweden akifundisha (USA) .
Wachezaji wengine watatu wanaowania goli zuri zaidi kwa maana ya tuzo ya FIFA Puskás : FALCAO alifunga goli katika mechi kati ya (América de Cali-Atletico Madrid, 19 May 2012), NEYMAR kati ya (Santos dhidi -Internacional, 7 March 2012) na Miroslav STOCH kati ya (Fenerbahçe dhidi -Gençlerbirliği, 3 March 2012).
Washindi watapewa zawadi zao katika makao makuu ya FIFA Ballon d’Or Gala huko Kongresshaus Zurich Tarehe 7 January 2013 zawadi nyingine ni Uuungwana Michezoni FAIR PLAY na Tuzo ya Heshima rais wa fifa
LIGI YA PREMIER YA UINGEREZA JANA USIKU
Man Utd. 1 vs 0 West Ham
November 28, 2012 8:00 PM UTC
Old Trafford — Manchester
Referee: M. Jones
Attendance: 75572
November 28, 2012 8:00 PM UTC
Old Trafford — Manchester
Referee: M. Jones
Attendance: 75572
Tottenham 2 vs 1 Liverpool
November 28, 2012 7:45 PM UTC
White Hart Lane — London
Referee: P. Dowd
Attendance: 36162
November 28, 2012 7:45 PM UTC
White Hart Lane — London
Referee: P. Dowd
Attendance: 36162
Everton 1Arsenal 1
Chelsea 0Fulham 0
Wigan Athletic 0Manchester City 2
Man Utd 1West Ham United 0
Chelsea 0Fulham 0
Wigan Athletic 0Manchester City 2
Man Utd 1West Ham United 0
KASHFA YA MACHANGUDOA KATIKA KAMBI YA HARAMBEE STARS, YAWAREJESHA NAIROBI WACHEZAJI NYOTA PAUL WERE NA KELVIN OMONDI.
Paul Were na Kevin Omondi. |
Kocha James Nandwi. |
KOCHA wa
timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars James Nandwa amewatimua wachezaji wake
wawili tegemeo katika kikosi chake kufuatia kutoroka kambi ya timu yao hapo
jana usiku.
Wachezaji hao
ni winga Paul Were na kiungo Kevin Omondi ambapo wachezaji hao waliondoka na
kuelekea kwenye starehe baada ya kupewa pesa zao za posho au Bonas ya mchezo
wao dhidi ya Sudani Kusini ambao walichomoza na ushindi wa mabao 2-0.
Taarifa zinasema
wachezaji hao walitoweka katika kambi yao iliyoko katika hoteli ya Sky Sports iliyoko
Kireka na kwenda kustarehe usiku mzima wakichanganywa na posho walizopewa
kufuatia ushindi.
Mbaya zaidi
wachezaji hao walirejea hotelini na machangudoa jambo ambalo kocha James Nandwa
amekielezea kitendo hicho kuwa ni cha aibu na kisichokubalika.
Kevin Omondi
alikuwa katika kiwango kizuri katika mchezo wao dhidi ya Sudani Kusini hapo
jana ambapo alitoa pasi za mwisho zilizo zaa magoli yote mawili ya Harambe ukiwa
ni ushindi wa kwanza kwa Harambee Stars.
Wachezaji hao
wanatarajiwa kurejea Nairobi huku adhabu zaidi zikiwasubiri kutoka shirikisho
la soka la Kenya (FKF) alivyo nukuliwa Francis Nyamweya.
WESLEY SNEIJDER AIFUNGULIA MILANGO MANCHESTER CITY
MILAN, Italia
Nyota huyo wa
kimataifa wa Uholanzi, kwa sasa amezuiwa kujumuika na kikosi cha kwanza cha
Inter, hadi atakapokubali kusaini mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo,
utakaoambatana na punguzo la mshahara wake
KIUNGO Wesley Sneijder amefungua milango ya kuhamia klabu ya
Manchester City
kwa kutoa kauli kuwa hana uhakika kama anataka kuendelea kubaki San Siro yaliko
makazi ya Inter Milan,
zaidi ya kipindi cha usajili wa majira ya baridi.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi, kwa sasa amezuiwa
kujumuika na kikosi cha kwanza cha Inter, hadi atakapokubali kusaini mkataba
mpya wa kuichezea klabu hiyo, utakaoambatana na punguzo la mshahara wake.
Kwa hasira Sneijder akakataa katakata kukubali masharti hayo
ya Inter na kuamua kuchagua kuihama klabu hiyo pindi dirisha la usajili wa
majira ya baridi litakapofunguliwa Januari mwakani.
Klabu za Manchester United, Schalke 04 na Anzhi Makhachkala,
ni miongoni mwa zinazomuwinda mkali huyo mwenye miaka 28, hali inayozalisha
vita kali ya kufuatilia kujua hatima yake.
‘Nina furaha kuwa hapa, lakini sijui nini kitatokea
baadaye,’ alijibu Mholanzi huyo alipoilzwa na mashabiki kuhusu uwezekano wa
kutimka klabuni hapo Januari mwakani.
Maelezo hayo ya Sneijder bila shaka yanafungua milango kwa
klabu zinazosaka saini yakena bosi wa Manchester City,
Mtaliano Roberto Mancini ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa kiungo huyo mahiri.
Inafahamika namna Mancini alivyojaribu mara mbili bila
mafanikio kusaka saini ya Sneijder kutua Man City,
na taarifa kutoka hapa zinapasha kuwa nyota huyo anaweza kupatikana kwa
dau pauni milioni 15.
VILLAS-BOAS AMKATIA TAMAA GARETH BALE
Gareth Bale (mwenye mpira) wa Tottenham Hotspur akimtoka beki wa Southampton wakati wa mechi kati ya timu hizo
LONDON, England
ANDRE Villas-Boas amekiri kuwa, Tottenham ina kibarua kigumu
cha kuhakikisha inaendelea kumbakisha Gareth Bale, baada ya kumshuhudia
akifanya vitu adimu kuhitimisha mechi nane bila kichapo Liverpool
na kuichapa mabao 2-1 jana usiku.
Bale alikimbia na mpira kwa mita 50 huku akichambua mabeki
wanne wa Liverpool, kabla ya kumtengea Aaron Lennon
kuipa Spurs bao la kwanza na kisha kumtungua mlinda mlango Pepe Reina kwa bao
la umbali wa mita 30.
Bale alisaini mkataba wa kubaki Spurs kiangazi kilichopita,
lakini hiyo haijazuia harakati za Barcelona na
Real Madrid kusaka saini ya mkali huyo mwenye miaka 23, na Villas-Boas amekiri
kuwa yeye kama kocha hana nguvu ya kumzuia
winga huyo kuondoka.
'Kwa sasa yeye yuko katika kiwango cha juu, akifanya mambo
makubwa kwa Spurs na kimsingi sisi kama timu
tunavutiwa mno na afanyacho kwa ajili yetu. Yuko katika levo ya juu
kulinganisha na wakati wowote,' Villas-Boas alisema.
'Ni wazi kwamba Tottenham kama klabu ya soka ingependa
kumbakisha yeye hapa kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo, lakini tunatambua
kwamba wachezaji bora na wazuri kama hawa
wanakuwa na thamani kubwa sokoni, ambalo ndio asili ya mchezo.'
FERGUSON AITOA CHELSEA MBIO ZA UBINGWA WA ENGLAND
MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amekenulia
meno mwanzo mbaya wa kocha wa Chelsea, Rafa Benitez klabuni Stamford Bridge,
na kutabiri ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu ni kinyang’anyiro cha timu za jiji la
Manchester.
Chelsea inayoshikilia ubingwa
wa soka barani Ulaya, iko nyuma kwa pointi saba nyuma ya vinara Man United na
sita, nyuma ya mabingwa watetezi Man
City.
Fergie bosi wa Man United, alisema: “Matokeo ya leo usiku
yanatuweka sisi mbali kidogo na Chelsea
katika mbio za ubingwa wa ligi.
“Sisi bado tuko mbele tukiongoza msimamo wa ligi, lakini Man City
wako karibu yetu na msimu bado ni mrefu.
“Umuhimu wa kushinda bao 1-0 katika baadhi ya mechi,
unawaonesha wapinzani wako kiasi cha ujasiri mlichonacho.
“Kama utaangalia baadhi ya mechi muhimu za matokeo ya bao
1-0 tuliowahi kupata... rejea nyuma kabisa tulipoicaha Newcastle wakati wakiwa pointi tisa juu yetu
mwaka 1996 – ushindi wetu wa 1-0 usiku huo, ukatuwezesha kutupa ubingwa.
“Kulikuwa na umuhimu wa ushindi wa 1-0. tulifanya hivyo kwa
wengi wao.”
MALAWI YAWAFUNGA KWA MBINDE ERITREA
Kocha wa
Tanzania, Kim Poulsen akiwa na Msaidizi wake, Sylvester Marsh wakifuatilia
mchezo kati ya Rwanda na Malawi. Chini ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF).
|
WAZEE WA KUZAMIA NCHI ZA WATU WAKIPIGA MICHAKATO...
NDIKUMANA AWATEGA SIMBA SC
Ndikumana |
Ndikumana
aliyewahi pia kucheza Norway na Uturuki, jana alifunga bao la tatu katika
mashindano haya, akiichezea Burundi dhidi ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars.
Sasa
anamzidi kwa bao moja, John Bocco ‘Adebayor’ wa Kilimanjafo Stars.
Jumla ya
mabao 17 hadi sasa yamefungwa katika mechi 16 za makundi yote matatu,
zilizopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala.
Bocco anafungana
na mshambuliaji mwingine wa Burundi, Christopher Nduwarugira, wakati wachezaji
wengine ambao hadi sasa kila mmoja amefunga bao moja ni Farid Mohamed, Yussuf
Ndikumana wa Burundi, Mohamed Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey Kizito wa Uganda, Yonatal Kebede Teklemariam, Haruna
NiyonzimUganda, David Ochieng, Clifton Miheso na Jean Mugiraneza.
Kwa sasa
Bocco anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, ndiye mshambuliaji pekee kwenye
kikosi cha Bara, baada ya washambuliaji wengine, Mbwana Samatta na Thomas
Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Kongo (DRC)
kuzuiliwa na klabu yao.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
John Bocco Tanzania 2
Chris
Nduwarugira Burundi 2
Yussuf
Ndikumana Burundi 1
Mohamed
Jabril Somalia 1(penalti).
Geoffrey
Kizito Uganda 1
Brian Umony Uganda 1
Yonatal
Teklemariam Ethiopia 1
Haruna
Niyonzima Rwanda 1
Jean
Mugiraneza Rwanda 1
David
Ochieng Kenya 1
Clifton
Miheso Kenya 1
Farid
Mohamed Sudan 1
KAZIMOTO, KAPOMBE HATARINI KUWAKOSA WASOMALI JUMAMOSI
Kazimoto |
WACHEZAJI wawili
wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, beki Shomary Kapombe na kiungo Mwinyi
Kazimoto, walishindwa kumaliza mechi za jana, baada ya kuumia na sasa wako
hatarini kuikosa mechi ya mwisho ya Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika
Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Somalia, Desemba 1.
Wachezaji
hao wa klabu ya Simba, wote waliumia kipindi cha pili na kutolewa, nafasi ya
Kapombe ikichukuliwa na Issa Rashid wa Mtibwa Sugar nay a Mwinyi ikichukuliwa
na Shaaban Nditi wa Mtibwa pia.
Wote
walitoka wakichechemea, kuashiria wamepata maumivu makali kidogo na Kocha Mkuu
wa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen alisema ataangalia hali zao leo na kesho.
Kim pia
alisema kwamba sasa imetosha kuzungumzia suala la washambuliaji Mbwana Samatta
na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
kama watajiunga na timu hiyo au la.
“Kwangu sasa
lazima ifikie wakati iwe inatosha, sitaki kuwazungumzia tena wachezaji hao,
waulizeni TFF,”alisema Poulsen baada ya kuulizwa kama mawasiliano na klabu yao
kama yanaendelea juu ya kuombea ruhusa.
Mazembe
imekataa kuwaruhusu wachezaji hao kwa sababu michuano ya Challenge haimo kwenye
kalenda ya FIFA.
Kutokana na
kukosekana kwa washambuliaji hao, Stars sasa inabaki na mshambuliaji mmoja tu
kikosini, John Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC, ambaye Watanzania wanatakiwa
kumuombea dua asiumie ili aendelee kuibeba timu yao ya taifa.
POULSEN HAJAKATA TAMAA, ALIA NA BAHATI JANA
Kim Poulsen jana |
KOCHA Mkuu
wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen, raia wa Denmark,
amesema kwamba bado ana matumaini ya kutinga Robo Fainali ya michuano ya Kombe
la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge licha ya jana
kuchapwa 1-0 na Burundi.
Mbaya wa Kim
na Stars jana, alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam,
Suleiman Ndikumana aliyefunga bao hilo dakika ya 52, katika mchezo huo wa Kundi
B, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole.
Akizungumza
mara baada ya mechi ya jana, Poulsen alisema kwamba anaamini
wakishinda mechi ya mwisho dhidi ya Somalia, watasonga mbele.
Hata hivyo,
Kim alisema haidharau Somalia kwani imeonyesha mchezo mzuri katika mechi zake
zote mbili pamoja na kufungwa.
“Nina muda
mzuri kidogo wa kujiandaa na mchezo huo hadi Jumamosi, tutajiandaa vizuri na
nina matumaini ya kushinda,”alisema.
Akizungumzia
mchezo wa jana, Kim alisema walitengeneza nafasi nyingi nzuri, lakini wakashindwa
kuzitumia, mipira ikigonga mwamba na mingine ikiokolewa ikiwa inaelekea
nyavuni, hivyo hana wa kumlaumu kwa matokeo hayo, bali habati haikuwa yao jana.
Burundi
walipata bao lao kwa penalti jana Nahodha huyo wa Burundi, anayechezea Inter
Stars ya nyumbani kwao kwa sasa, akifunga baada ya yeye mwenyewe kuangushwa
kwenye eneo la hatari na Shomary Kapombe.
Hadi
mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na Burundi
walifanya mashambulizi mawili ya hatari zaidi, lakini sifa zimuendee ‘TZ One’,
Juma Kaseja aliyeokoa hatari hizo.
Stars
hawakucheza soka yao ya chini kutokana na hali mbaya ya Uwanja, kujaa matope,
kuwa wenye kuteleza kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kutwa nzima ya leo.
Kipindi cha
pili Stars walijitahidi kutaka kusawazisha mabao hilo, lakini bahati haikuwa
yao na zaidi waliishia kukosa mabao mawili ya wazi.
Kwa matokeo
hayo, Burundi imeendelea kuongoza Kundi A, kwa pointi zao sita, mabao sita ya
kufunga na moja la kufungwa, wakati Bara inabaki nafasi ya pili kwa pointi zake
tatu, Sudan ya tatu ikiwa na pointi moja sawa na Somalia.
Kikosi cha Stars
jana kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe/Issa
Rashid, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco,
Mwinyi Kazimoto/Shaaban Nditi na Simon Msuva/Amri Kiemba.
STARS WAOMBEWA VIAU VYA KUCHEZEA KWENYE MVUA KAMPALA
Mashabiki wanaoiunga mkono Stars mjini hapa |
MASHABIKI wa
Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars waliopo hapa, wameliomba Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kuwatumia wachezaji wa timu hiyo viatu vya kuchezea kwenye mvua,
kabla ya mechi ya mwisho ya Kundi B, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na
Kati, CECAFA Tusker Challenge Jumamosi.
Wakizungumza
baada ya mechi ya jana dhidi ya Burundi, ambayo Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, walichapwa 1-0 kwenye
Uwanja wa Mandela, Namboole mjini mashabiki hao walisema hali ya hewa ya mji
huu kwa sasa itaendelea kuwa ya mvua na TFF inapaswa kuchukua tahadhari baada
ya matokeo ya jana.
“Leo
tumefungwa kwa sababu Uwanja ulikuwa unateleza kutokana na mvua na wenzetu
Burundi walikuwa wana viatu vya mvua, kwa hivyo Uwanja haukuwasumbua, sasa na
sisi lazima wachezaji wetu wapatiwe viatu hivyo,”alisema Ally Abubakar aliyetoka River Side, Ubungo, Dar es Salaam kuja
kuishangilia timu ya taifa.
Mbaya wa
Stars jana, alikuwa mshambuliaji wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam,
Suleiman Ndikumana aliyefunga bao hilo dakika ya 52, katika mchezo huo wa Kundi
B, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole.
Burundi
walipata bao lao kwa penalti jana Nahodha huyo wa Burundi, anayechezea Inter
Stars ya nyumbani kwao kwa sasa, akifunga baada ya yeye mwenyewe kuangushwa
kwenye eneo la hatari na Shomary Kapombe.
Hadi
mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na Burundi
walifanya mashambulizi mawili ya hatari zaidi, lakini sifa zimuendee ‘TZ One’,
Juma Kaseja aliyeokoa hatari hizo.
Stars
hawakucheza soka yao ya chini kutokana na hali mbaya ya Uwanja, kujaa matope,
kuwa wenye kuteleza kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kutwa nzima ya leo.
Kipindi cha
pili Stars walijitahidi kutaka kusawazisha mabao hilo, lakini bahati haikuwa
yao na zaidi waliishia kukosa mabao mawili ya wazi.
Kwa matokeo
hayo, Burundi imeendelea kuongoza Kundi A, kwa pointi zao sita, mabao sita ya
kufunga na moja la kufungwa, wakati Bara inabaki nafasi ya pili kwa pointi zake
tatu, Sudan ya tatu ikiwa na pointi moja sawa na Somalia.
ZANZIBAR KUJARIBU BAHATI TENA LEO TUSKER CHALLENGE, KUKIPIGA NA RWANDA NI VITA YA NIYONZIMA NA CANNAVARO
Zanzibar Heroes |
Mchezo huo
utatanguliwa na mchezo mwingine, kati ya Malawi na Eritrea ambao utaanza saa
10:00 jioni kwenye Uwanja huo.
Zanzibar
walilazimishwa sare ya bila kufungana na Eritrea katika mchezo wa kwanza,
wakati Malawi ilifungwa mabao 2-0 na Rwanda.
Zanzibar
wanahitaji kushinda mechi ya leo, ili kuweka hai matumaini ya kuingia Robo
Fainali ya michuano hii, ingawa mbele ya Rwanda huo utakuwa mtihani mgumu kwao.
Moja kati ya
burudani zinazotarajiwa kwenye mechi hiyo ni kushuhudia wachezaji wawili wa
klabu moja, Yanga SC ya Dar es Salaam, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa
Zanzibar na kiungo Haruna Niyonzima wa Rwanda, wakichuana leo, tena wote wakiwa
manahodha wa timu zao za taifa.
Baada ya
sare katika mechi ya kwanza, Cannavaro pamoja na kuwaomba radhi Wazanzibari kwa
sare hiyo, lakini pia ameahidi watajituma na kufanya vizuri katika mechi
zijazo.
MECHI ZILIZOSALIA:
RATIB KUNDI
A:
Novemba 30, 2012:
Kenya v Ethiopia (Saa
9:00 Alasiri)
Sudan Kusini v Uganda (Saa 12:00 jioni)
RATIBA
KUNDI B:
Desemba 1, 2012:
Sudan v Burundi (Saa
9:00 Alasiri)
Somalia v Tanzania (Saa
12:00 jioni)
RATIBA
KUNDI C:
Novemba 29, 2012:
Malawi v Eritrea (Saa
9:00 Alasiri)
Rwanda v Zanzibar (Saa
12:00 jioni)
Desemba 2, 2012:
Malawi v Zanzibar (Saa
9:00 Alasiri)
Eritrea v Rwanda (Saa
12:00 jioni)
MSIMAMO
KUNDI A:
P W D L GF GA GD Pts
Uganda 2 2 0 0 2 0 2 6
Kenya 2 1 0 1 2 1 1 3
Ethiopia 2 1 0 1 1 1 0 3
Sudan Kusini 2 0 0 2 0 3 -3 0
MSIMAMO
KUNDI B:
P W D L GF GA GD Pts
Burundi 2 2 0 0 6 1 5 6
Tanzania 2 1 0 1 2 1 1 3
Sudan 2 1 0 1 1 2 -1 3
Somalia 2 0 0 2 1 6 -5 0
MSIMAMO
KUNDI C:
P W D L GF GA GD Pts
Rwanda 1 1 0 0 2 0 2 3
Eritrea 1 0 1 0 0 0 0 1
Zanzibar 1 0 1 0 0 0 0 1
Malawi 1 0 0 1 0 2 -2 0
VIWANGO VYA
UBORA FIFA
NCHI NAFASI
Uganda 86
Malawi 101
Ethiopia 102
Sudan 102
Rwanda 122
Burundi 128
Kenya 130
Tanzania 134
Zanzibar 134
Somalia 193
Eritrea 192
Sudan Kusini 200
(Viwango hivi vimetoka mwezi huu)
BPL: Man United BADO JUU, City wapo, Chelsea yanasa tena!
>>LIVERPOOL yachapwa na Spurs, Everton na Arsenal drooo!!
Mechi
8 za Ligi Kuu England, BPL [Barclays Premier League], zilichezwa
Jumatano Usiku na Bao la Sekunde ya 31 la Robin van Persie limeendelea
kuwaweka Manchester United kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 1 mbele ya
Man City walioichapa Wigan 2-0 lakini sare ya Chelsea na Fulham
imewabakisha Chelsea nafasi ya 3 na kuwafanya wawe Pointi 7 nyuma ya
vinara Man United.
+++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumatano Novemba 28
Chelsea 0 Fulham 0
Everton 1 Arsenal 1
Southampton 1 Norwich 1
Stoke 2 Newcastle 1
Swansea 3 West Brom 1
Tottenham 2 Liverpool 1
Wigan 0 Man City 2
Man United 1 West Ham 0
+++++++++++++++++++++++++++
WIGAN 0 MAN CITY 2
Hadi Haftaimu Bao zilikuwa 0-0 lakini
Bao mbili zilizofungwa na Mario Balotelli na James Milner katika Dakika
za 69 na 72 ziliwapa ushindi Man City na kuwabakiza nafasi ya pili
Pointi 1 nyuma ya Man United.
VIKOSI:
Wigan: Al Habsi, Stam,
Boyce, Lopez, Figueroa, McCarthy, Jones, Gomez, Kone, Beausejour, Di
Santo. Subs: Pollitt, McManaman, McArthur, Boselli, Fyvie, Golobart,
Redmond.
Man City: Hart, Maicon,
Kompany, Nastasic, Zabaleta, Javi Garcia, Toure, Silva, Barry, Aguero,
Balotelli. Subs: Pantilimon, Toure, Kolarov, Milner, Sinclair, Tevez,
Dzeko.
Refa: Mark Halsey
MAN UNITED 1 WEST HAM 0
Bao la Sekunde ya 31 tangu mpira uanze
la Robin van Persie baada ya pande la Michael Carrick limewapa Man
United ushindi wa Bao 1-0 na kuwabakisha kileleni mwa Ligi.
VIKOSI:
Man United: Lindegaard, Da Silva, Smalling, Evans, Evra, Carrick, Anderson, Cleverley, Rooney, van Persie, Hernandez
Akiba: De Gea, Jones, Ferdinand, Young, Welbeck, Fletcher, Buttner.
West Ham: Jaaskelainen, Demel, Reid, Collins, O'Brien, Taylor, Diame, Tomkins, Jarvis, Nolan, Carroll
Akiba: Spiegel, Cole, Maiga, Spence, O'Neil, Moncur, Lletget.
Refa: Mike Jones
TOTTENHAM 2 LIVERPOOL 1
Uwanjani White Hart Lane, Aaron Lennon
na Gareth Bale walipachika Bao kwa Tottenham lakini pia Bale alijifunga
mwenyewe na Mechi kwisha 2-1 kwa ushindi kwa Tottenham.
VIKOSI:
Tottenham: Lloris, Walker, Gallas, Dawson, Vertonghen, Lennon, Sandro, Dembele, Bale, Dempsey, Defoe
Akiba: Friedel, Huddlestone, Naughton, Sigurdsson, Livermore, Townsend, Carroll.
Liverpool: Reina, Johnson, Agger, Skrtel, Downing, Allen, Henderson, Gerrard, Jose Enrique, Sterling, Suarez
Akiba: Jones, Sahin, Assaidi, Carragher, Fernandez Saez, Shelvey, Wisdom.
Refa: Phil Dowd
STOKE 2 NEWCASTLE 1
Newcastle walitangulia kufunga kwa Bao
la Papiss Cisse katika Dakika ya 47 lakini Bao za Walters na Jerome za
Dakika ya 81 na 85 ziliwainua kidedea Stoke City kwa Bao 2-1.
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Shotton, Huth, Shawcross, Cameron, Walters, Nzonzi, Whelan, Etherington, Adam, Crouch
Akiba: Sorensen, Palacios, Jones, Whitehead, Upson, Kightly, Jerome.
Newcastle: Krul, Simpson, Coloccini, Williamson, Santon, Anita, Perch, Tiote, Gutierrez, Ba, Cisse
Akiba: Elliot, Bigirimana, Marveaux, Sammy Ameobi, Ranger, Ferguson, Tavernier.
Refa: Howard Webb
SWANSEA 3 WEST BROM 1
Swansea wameifunga WBA Bao 3-1 kwa Bao za Michu na mbili za Routledge huku bao la WBA likifungwa na Romelu Lukaku.
VIKOSI:
Swansea: Tremmel, Rangel, Williams, Chico, Davies, Britton, Hernandez, Ki, Dyer, Routledge, Michu
Akiba: Cornell, Monk, Shechter, Moore, de Guzman, Tiendalli, Agustien.
West Brom: Myhill, McAuley, Olsson, Ridgewell, Jones, Yacob, Morrison, Mulumbu, Brunt, Odemwingie, Lukaku
Akiba: Daniels, Popov, Rosenberg, Long, Dorrans, Tamas, Fortune.
Refa: Lee Mason
CHELSEA 0 FULHAM 0
Hii ni Mechi ya pili mfululizo kwa Meneja mpya wa Chelsea Rafael Benitez kutoka 0-0.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Cole, Romeu, Ramires, Hazard, Oscar, Bertrand, Torres
Akiba: Turnbull, Mata, Mikel, Moses, Ferreira, Marin, Cahill.
Fulham: Schwarzer, Riether, Senderos, Hughes, Riise, Duff, Diarra, Sidwell, Karagounis, Rodallega, Berbatov
Akiba: Etheridge, Kelly, Baird, Kasami, Petric, Frei, Dejagah.
Refa: Anthony Taylor
EVERTON 1 ARSENAL 1
Uwanjani Goodison Park, Arsenal
walitangulia kwa bao la mapema la Theo Walcott aliefunga katika Sekunde
ya 50 tu tangu Mechi ianze lakini Marouane Fellaini akaisawazishia
Everton.
VIKOSI:
Everton: Howard, Hibbert, Jagielka, Distin, Baines, Naismith, Gibson, Osman, Pienaar, Fellaini, Jelavic
Akiba: Mucha, Heitinga, Oviedo, Hitzlsperger, Gueye, Barkley, Vellios.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Vermaelen, Walcott, Ramsey, Arteta, Wilshere, Cazorla, Girou
Akiba: Mannone, Rosicky, Oxlade-Chamberlain, Coquelin, Jenkinson, Gervinho, Gibbs.
Refa: Michael Oliver
SOUTHAMPTON V NORWICH
VIKOSI:
Southampton: Gazzaniga, Clyne, Yoshida, Fonte, Shaw, Puncheon, Schneiderlin, Cork, Lallana, Lambert, Ramirez
Akiba: Kelvin Davis, Hooiveld, Steven Davis, Rodriguez, Do Prado, Mayuka, Reeves.
Norwich: Bunn, Whittaker, Ryan Bennett, Bassong, Garrido, Snodgrass, Johnson, Tettey, Pilkington, Hoolahan, Holt
Akiba: Rudd, Martin, Howson, Jackson, Morison, Elliott Bennett, Barnett.
Refa: Mark Clattenburg
+++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 1 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Ham v Chelsea
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Swansea
Fulham v Tottenham
Liverpool v Southampton
Man City v Everton
QPR v Aston Villa
West Brom v Stoke
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Reading v Man United
Jumapili Desemba 2
[SAA 1 Usiku]
Norwich v Sunderland
Jumatatu Desemba 3
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Wigan
UFUKWENI COPACABANA: Hodgson ashuhudia umahiri wa Brazil!!
>>ASHUHUDIA, Bibi na Bwana wakipiga DANADANA!!!
Akiwa
ziarani, Rio de Janeiro, akitembea kwenye Ufukwe wa Copacabana, Roy
Hodgson, Meneja wa England, alishuhudia kitu kilichomfungua macho na
kubaini kuwa Wabrazil ni wakali kujenga vipaji vyao na kukubali kuwa
wakati umefika kwa England kuchukua hatua za makusudi ili waweze kufanya
vyema zaidi katika Ulimwengu wa Soka.
Hodgson ameeleza: “Niliwaona Watu
wawili, Mwanamke na Mwanaume, wakiwa wamesimama Mita 25 toka kila mmoja
na yule Mwanaume alikuwa akiupiga mpira kichwani kwa Mwanamke na yule
Mama anarudisha kwa Kichwa miguuni kwa yule jamaa! Nilisimama kutazama
danadana ile itachukua muda gani…iliendelea kwa Dakika 12 bila kusimama
wala mpira kudondoka chini! Nikakata tamaa nikaondoka, niliporudi tena
pale niliwakuta bado wapo, danadana inaendelea na mpira uko juu tu
haugusi chini!”
Aliongeza: “Hapa England, tunafanya
mazoezi ya kujenga ufundi wa kumiliki mpira kwa Dakika 5 au 10 tu, kisha
tunataka kucheza Gemu!”
Hodgson amesema hiyo inaonyesha tofauti
kati ya Brazil, ambao wametwaa Kombe la Dunia mara 5, na England
iliyotwaa mara moja tu na tangu Mwaka 1996, walipofika Robo Fainali ya
EURO 1996, hawajaweza kuvuka Robo Fainali yeyote ya Mashindano makubwa.
Ingawa amekiri kuwa hali ya hewa ya
Brazil, ambako ni joto, ukilinganisha na England kwenye baridi na mvua
kunawafanya wapata urahisi wa kucheza Soka mfululizo, lakini pia
amelaumu miundo mbinu ukilinganisha na Nchi nyingine za Ulaya ambazo
zina Viwanja vingi vya ndani ambavyo huweza kutumika wakati wowote wa
Mwaka hata wakati wa Winta kali ambapo Nchi hufunikwa barafu.
No comments:
Post a Comment