Friday, September 28, 2012

Aguero ndani, Tevez bado NJE Argentina!

Ijumaa, 28 Septemba 2012 16:08
Chapisha Toleo la kuchapisha
>> PABLO ZABALETA YUMO! 

>> ARGENTINA kucheza na URUGUAY nyumbani Oktoba 12

BRAZIL_2014_BESTWachezaji wa Manchester City Sergio Agüero na Pablo Zabaleta wameitwa kuichezea Timu ya Taifa ya Argentina itakapocheza Mechi Mwezi ujao ya kuwania kucheza Fainali ya Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil lakini mwenzao wa Klabu moja Carlos Tevez bado hana nafasi kwa Timu hiyo.
Aguero hakucheza Mechi za Argentina za Raundi iliyopita za Kombe la Dunia dhidi ya Paraguay na Peru zilizochezwa mapema Mwezi huu kwa vile alikuwa ameumia goti lakini kutoitwa kwa Tevez sasa kumekuwa kitu cha kawaida toka kwa Kocha wa Timu ya Taifa Alejandro Sabella na badala yake Kocha huyo amemchukua Straika wa Palmeiras Hernan Barcos.
Wachezaji wengine mashuhuri walioachwa ni Beki wa Newcastle Fabricio Coloccini, Kiungo wa Anderlecht Lucas Biglia na Fowadi Internazionale Rodrigo Palacio.
Katika Mechi za Kanda ya Marekani ya Kusini kuwania kucheza Fainali ya Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil, Argentina itacheza nyumbani na Uruguay Oktoba 12 na ugenini na Chile Oktoba 16.
KIKOSI KILICHOITWA:
Mariano Andujar (Catania), Sergio Romero (Sampdoria); Hugo Campagnaro (Napoli), Federico Fernandez (Napoli), Pablo Zabaleta (Manchester City), Ezequiel Garay (Benfica), Marcos Rojo (Sporting Lisbon); Javier Mascherano (Barcelona), Angel Di Maria (Real Madrid), Fernando Gago (Valencia), Enzo Perez (Benfica), Jose Sosa (Metalist Kharkiv), Pablo Guinazu (Internacional); Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Real Madrid), Sergio Agüero (Manchester City), Ezequiel Lavezzi (Paris St Germain), Hernán Barcos (Palmeiras).
========================
MSIMAMO KANDA ya NCHI za MAREKANI ya KUSINI:
1 Argentina Mechi 7 Pointi 14
5 Colombia Mechi 7 Pointi 13
3 Ecuador Mechi 7 Pointi 13
4 Uruguay Mechi 7 Pointi 12
2 Chile Mechi 7 Pointi 12
6 Venezuela Mechi 8 Pointi 11
7 Peru Mechi 7 Pointi 7
8 Bolivia Mechi 7 Pointi 4
9 Paraguay Mechi 7 Pointi 4
FAHAMU: Timu 4 za juu zinatinga Fainali Brazil moja kwa moja na ile ya 5 itaenda Mechi ya Mchujo.
 

Eto’o Kundini Cameroun!

Ijumaa, 28 Septemba 2012 15:50
Chapisha Toleo la kuchapisha
Baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Cameroun Mwezi Novemba Mwaka jana kwa kuongoza mgomo wa Wachezaji kudai malipo yao na baada ya kumaliza kifungo, Nahodha wa zamani wa Cameroun, Samuel Eto’o, aligoma kurudi kuichezea Nchi yake lakini hivi sasa Staa huyo amebadili uamuzi na kukubali kurejea kuichezea tena Cameroun.
Mwezi uliopita Eto’o aliitwa kuichezea Cameroun Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mwisho ya Mtoano kuwania nafasi 15 za kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, dhidi ya Cape Verde lakini aligoma na Cameroun ikapigwa 2-0 huko Visiwani Cape Verde.
Timu hizi zinatarajiwa kurudiana hapo Oktoba 14.
Kurudi kwa Eto’o  kunafuatia mazungumzo pamoja na Waziri Mkuu Yang, Waziri wa Michezo Adoum Garoua, Meneja wa Timu Song Bahang na Kocha Jean Paul Akon.
Eto’o alitoa tamko kwenye Tovuti yake: “Baada ya kuombwa na uongozi wa juu wa Nchi yetu nimekubali kuichezea Nchi yangu.”
Eto'o ameifungia Cameroun Mabao 53 katika Mechi 109.
SHIRIKI

Kaka Kundini Brazil

Alhamisi, 27 Septemba 2012 23:50
Chapisha Toleo la kuchapisha
NEYMAR_v_MESSIKaka ameitwa kuichezea Brazil kwa ajili ya Mechi za Kimataifa za Kirafiki dhidi ya Iraq na Japan Mwezi ujao baada ya kutochukuliwa tangu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 zilizochezwa huko Afrika Kusini.
Tangu atue Real Madrid, Kaka, Miaka 30, amekuwa na wakati mgumu lakini hivi karibuni nyota yake imeanza kung’ara tena na Jumatano aliifungia Real hetitriki walipocheza Mechi ya Kirafiki na Klabu ya Colombia Millonarios.
Kocha wa Brazil, Mano Menezes, ameamua kumchukua Kaka ili kumpima uwezo wake katika Mechi hizo mbili ambazo zote zitachezwa Ulaya.
Mechi ya Brazil na Iraq itachezwa huko Malmo, Sweden hapo Oktoba 11 na ile ya Japan itachezwa Wroclaw, Poland hapo Oktoba 16.
Kikosi hicho cha Brazil kina Wachezaji wanne ambao wanachezea Klabu za Ligi Kuu England ambao ni watatu kutoka Chelsea, David Luiz, Oscar na Ramires, na Kiungo wa Tottenham Sandro.
Kikosi kamili:
Makipa: Diego Alves (Valencia ), Jefferson (Botafogo), Victor (Atletico-MG)
Mabeki: Daniel Alves (Barcelona ), Marcelo (Real Madrid), Adriano (Barcelona), Alex Sandro (Porto), Thiago Silva (PSG), David Luiz (Chelsea), Dede (Vasco), Leandro Castan (Roma)
Viungo: Sandro (Tottenham), Paulinho (Corinthians), Fernando (Gremio), Giuliano (Dnipro), Lucas Moura (Sao Paulo), Oscar (Chelsea), Ramires (Chelsea), Thiago Neves (Fluminense), Kaka (Real Madrid)
Mastraika: Neymar (Santos), Leandro Damiao (Internacional), Hulk (Zenit)
 

JOEY BARTON aikejeli FA kumfungia Terry Mechi 4 tu!

Alhamisi, 27 Septemba 2012 21:22
Chapisha Toleo la kuchapisha
>>YEYE Kifungo chake 12 kwa VURUGU, ahoji UBAGUZI 4 tu??
>>AHOJI: “Mechi 4? Mwaka mzima uchunguzi, Siku 4 Kesi, ni Mechi 4 tu?”
JOEY_BARTON_n_KOMPANYMchezaji makeke Joey Barton amesema FA inatia aibu sana kwa kumfungia John Terry Mechi 4 kwa Ubaguzi wakati Luis Suarez alipigwa Mechi 8 kwa kosa kama hilo na yeye kwa ugomvi Uwanjani wakati wa Mechi na Manchester City Msimu uliopita alitwangwa Mechi 12.
Joey Barton, ambae alikuwa Nahodha wa QPR, Timu ambayo Beki wake Anton Ferdinand ndie aliekashifiwa kibaguzi na John Terry Oktoba Mwaka jana, kwa sasa yupo Ufaransa akicheza kwa mkopo na Timu ya Marseille na amehoji kupitia Mtandao wa Twitter.
Barton ameandika: “Mechi 4? Mwaka mzima uchunguzi, Siku 4 Kesi na ni Mechi 4 tu? Suarez alipewa 8 sio??”
Aliongeza: “Hii inathibitisha mengi. Ni takataka hii. Mechi 12 kwa ugomvi na 4 kwa hilo. FA lazima wanatia aibu.”
Barton pia alihoji uhalali wa yeye kufungiwa Mechi 12 kwa kuburuzana na Wachezaji wa Manchester City wakati Mbaguzi anapewa Mechi 4 tu.
Alimalizia: “Jana Usiku niliota kuhusu Terry, Watu wanapiga kelele na Kikosi cha Mauaji kipo! Lakini hili sio nilotegemea!”
Wakati huo huo, Kambi ya John Terry imetoa tamko kuwa inasubiri kupewa Ripoti yote ya Kesi iliyomfungia na kisha watatoa uamuzi kama watakata Rufaa au la.
John Terry anao muda wa Siku 14 kukubali makosa au kukata Rufaa akipenda.
SHIRIKI
 

BRAZIL 2014: FIFA yapitisha Saa za Mechi Kuanza FAINALI KOMBE la DUNIA!

Alhamisi, 27 Septemba 2012 20:12
Chapisha Toleo la kuchapisha
>>MECHI ya UFUNGUZI 12 Juni 2014 SAA 5 Usiku Bongo Taimu!
>>FAINALI 13 Julai 2014 SAA 4 Usiku Maracana Stadium!
BRAZIL_2014_BESTLEO Kamati Kuu ya FIFA iliyoketi huko kwenye ‘Nyumba ya FIFA’ Mjini Zurich, Uswisi imepitisha rasmi Saa za kuanza kwa Mechi za Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa huko Brazil Mwaka 2014.
Mechi ya ufunguzi itachezwa Mjini Sao Paulo kuanzia Saa 5 Usiku Bongo Taimu ikiwa ni Saa 11 Jioni huko Brazil.
Tofauti ya Masaa kati ya Brazil na Tanzania ni Masaa 6 na Tanzania iko mbele kwa Masaa hayo.
Lakini, kwa Mechi ambazo zitachezwa huko Miji ya Cuiaba na Manaus tofauti ya Masaa ni 7.
Mechi za Makundi zitakuwa zikichezwa, kwa Saa za Bongo, Saa 1 Usiku, Saa 4 Usiku, Saa 5 Usiku, Saa 6 Usiku, Saa 7 Usiku na Saa 9 Usiku.
Hatua za Mtoano Mechi zitaanza Saa 1 Usiku na Saa 5 Usiku.
Nusu Fainali zitachezwa Saa 5 Usiku na Fainali, hapo Julai 13, 2014, ni Saa 4 Usiku.
Vile vile, FIFA imethibitisha kuwa Droo kamili ya Ratiba ya Fainali za Kombe la Dunia itafanyika Ijumaa Desemba 6, 2013 huko Costa do Sauipe, Bahia, Brazil.
HABARI ZA AWALI:
FIFA, Ronaldo wamwanua Armadillo, Kinyago maalum kwa Kombe la Dunia 2014!!
KUBATIZWA: MIJUBI au FULECO au ZUZECO!!
FIFA na Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 Brazil, kupitia Nguli wao, Ronaldo, wameanua ‘Kinyago’ , au, tuite ‘Katuni maalum’, kwa ajili ya Mashindao hayo ambae ni Mnyama aitwae Armadillo ambae yupo hatarini kuangamizwa na ambae ifikapo Mwezi Novemba atapewa Jina lake maalum.
Kinyago hicho kitabatizwa ama Amijubi, Fuleco au Zuzeco Jina ambalo litachaguliwa na Wabrazil kwa kura.
Tayari Fainali hizo za Mwaka 2014 zimeshapata Mpira maalum uliotengenezwa na Kampuni ya Adidas, uliopewa Jina maalum, "Brazuca" ambalo ni neno la mtaani na la utani likimaanisha Wazalendo wa Brazil na hili limewekwa ili kuonyesha msisitizo wa asili ya Raia wa Brazil.
Armadillo ni Mnyama anaepatikana Kaskazini Mashariki ya Brazil na ni mithili ya Kakakuona ambae ana gamba gumu mgongoni na hujiviringisha kjitetea wakati akitaka kushambuliwa.
Wakati akimwanua Armadillo, Ronaldo alisema: “Nina furaha kumkaribisha Mwanachama mpya muhimu wa Timu yetu ya Mwaka 2014.”
Kinyago hicho kina Rangi za Bendera za Brazil na maandishi ‘Brazil 2014.’
FIFA, kupitia Katibu Mkuu wake Jerome Valcke imesema: “Kwa vile Mnyama huyo ni Kiumbe kinachotishiwa kuangamia kukitumia katika Kombe la Dunia ni kutangaza umuhimu wake katika mazingara na uhai wa Viumbe na Mimea.”
Pia FIFA imesema Majina matatu yaliyotolewa ili kupigiwa Kura kumbatiza Armadillo yana maana zake muhimu.
Amijubi huwakilisha urafiki na furaha wakati Fuleco na Zuzeco yanahusishwa na ujumbe wa uhai wa Viumbe na Mimea.
Katika Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 huko Afrika Kusini Kinyago alietumiwa alikuwa ni Chui alieitwa ‘Zakumi’, Fainali za 2006 huko Germany walikuwa na Simba aliepewa Jina la Goleo.
Kinyago wa kwanza kabisa kutumika katika Kombe la Dunia ni katika zile Fainali za Mwaka 1966 huko England na alikuwa ni Simba alievalishwa Bendera ya Uingereza na kuitwa ‘Willie.’
Vinyago vingine vilivyowahi kutumika ni Mtoto alieitwa ‘Juanito’ huko Mexico 1970, Chungwa lililoitwa ‘Naranjito’ huko Spain Mwaka 1982, Mbwa alieitwa ‘Striker’ huko USA 1994 na Jogoo mwenye Jina la ‘Footix’ huko Ufaransa Mwaka 1998.

No comments:

Post a Comment