Wednesday, October 24, 2012

 

YANGA NA POLISI TAIFA, AZAM YAWANIA USUKANI CHAMAZI MBELE YA RUVU SHOOTING LEO

Yanga SC


LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi nne za raundi ya tisa huku Azam ikiusaka usukani wa ligi hiyo ikiwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Kipre Herman Tchetche, tegemeo la Azam
Mechi hiyo namba 60 ambayo kama Azam itashinda itafikisha pointi 20, hivyo kuwa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom itakayochezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, viingilio vyake vitakuwa ni Sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
Lakini macho na masikio ya wengi yatakuwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambao Yanga wataikaribisha Polisi Morogoro, wanaoshika mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Katika mechi hiyo ambayo viingilio vitakuwa Sh. 5,000, Sh. 8,000, Sh. 15,000 na Sh. 20,000, refa Alex Mahagi kutoka Mwanza ndiye atakayepuliza filimbi kwenye mechi hiyo namba 62, akisaidiwa na Frank Komba na Michael Mkongwa, wote kutoka Iringa wakati mwamuzi msaidizi ni Oden Mbaga anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wa Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo, Yanga itawakosa mabeki wake wa kati, Job Ibrahim, Kevin Yondan na mshambuliaji Said Bahanuzi ambao ni majeruhi.
Job, ambaye amekuwa beki wa akiba tangu mwanzoni mwa msimu, aliumia kifundo cha mguu mazoezini mwishoni mwa wiki na juzi hakufanya mazoezi kabisa, wakati Yondan na Bahanuzi wanaendelea na programu ya mazoezi mepesi, chini ya kocha Mholanzi, Ernie Brandts.
Kwa sababu hiyo, Mbuyu Twite ataendelea kucheza pamoja na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika beki ya kati, wakati Jerry Tegete ataendelea kucheza na Didier Kavumbangu katika safu ya ushambuliaji.
‘Dogo’ Simon Msuva amemaliza adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa Oktoba 3, mwaka huu katika mechi dhidi ya Simba na ilikuwa aanze kucheza tangu Jumamosi, ila kutokana na kiwango duni cha Hamisi Kiiza alichoonyesha kwenye mechi na Ruvu Shooting Jumamosi, leo kinda huyo anaweza kurudishwa uwanjani.
Kiiza aliichezea Yanga kwa mara ya kwanza siku hiyo akitokea benchi kipindi cha pili, tangu atolewe kipindi cha kwanza katika mechi dhidi ya Simba, Oktoba 3, mwaka huu. Kiiza alikuwa kwao, Uganda, alipokwenda kuichezea timu yake ya taifa, The Cranes katika mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini.
Uganda ilitolewa na Zambia kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya jumla ya 1-1, Zambia wakianza kushinda nyumbani 1-0 na Uganda wakashinda kwao 1-0 pia mwishoni mwa wiki, hivyo mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti, ambako timu ya Kiiza ilitolewa.
Yanga imeweka kambi katika hoteli ya Uplands, Changanyikeni, Dar es Salaam huku ikiendelea kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Yondan aliyeumizwa na kiungo wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ katika mechi baina ya wapinzani hao wa jadi, Oktoba 3, mwaka huu, wakati Bahanuzi ‘Spider Man’ alichanika nyama za paja la mguu wa kulia katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba Oktoba 8, mwaka huu.
Bahanuzi aliumia dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete katika mechi ambayo Yanga ililala 1-0, beo pekee la Themi Felix.
Bahanuzi ndiye tegemeo la mabao la Yanga kwa sasa, kwani tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, ameifungia mabao 12 katika mechi 13, ikiwemo ile dhidi ya Kagera aliyocheza kwa dakika 23 kabla ya kuumia na kutoka. 
Yanga kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 14, baada ya kucheza nane, kushinda nne, sare mbili na kufungwa mbili. Simba iliyocheza mechi tisa, inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 19, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 17, iliyocheza mechi saba.
Kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, wenyeji Coastal Union wataikaribisha African Lyon ya Dar es Salaam, wakati Mtibwa Sugar itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu ulioko kwenye mashamba ya miwa Turiani mkoani Morogoro.

LIGI DARAJA LA KWANZA BARA YAANZA KUTIMUA VUMBI LEO

Wachezaji wa Moro United wakimdhibiti mchezaji wa Simba (kushoto) katika mchezo wao wa kujipima nguvu kabla ya kuanza Ligi daraja la Kwanza wiki iliyopita. Moro inaanza na Villa Squad Mlandizi


LIG Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja mbalimbali nchini.
Kundi A kutakuwa na mechi tatu ambapo Burkina Faso itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati JKT Mlale itakuwa mwenyeji wa Small Kids kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.
Nayo Kurugenzi itaumana na Majimaji katika Uwanja wa Wambi ulioko Mufindi mkoani Iringa. Kundi hilo litamaliza raundi ya kwanza keshokutwa (Oktoba 25 mwaka huu) kwa mchezo kati ya Mkamba Rangers na Polisi Iringa utakaofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mechi za kundi B kwa leo ni Ndanda dhidi ya Transit Camp katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Villa Squad itakipiga na Moro United kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi. Oktoba 25 mwaka huu ni Green Warriors v Tessema (Mabatini, Mlandizi) na Polisi Dar v Ashanti United (Uwanja wa Chamazi).
Kundi C leo ni Kanembwa FC v Polisi Dodoma (Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma), Mwadui v Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi Mara (Kirumba, Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi, Tabora).

AFCON 2013: Droo ya Makundi ya Fainali kufanyika Jumatano Oktoba 24 huko Durban!!



Chansa (left) seen here celebrating a goal with Zambian team mates at AFCON 2012 finals
>>UWEZEKANO ‘KUNDI la KIFO’ la Ivory Coast, Nigeria, Algeria au Morocco, na Congo DR!!
Droo ya kupanga Makundi manne ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Afrika Kusini kuanzia Tarehe 19 Januari 2013 hadi 10 Februari 2013, itafanyika Jumatano Oktoba 24 huko Mjini Durban Afrika Kusini huku Timu 16 zilizo Fainali zimegawanywa katika Vyungu vinne ambapo kila Chungu kitatoa Timu moja kuunda Kundi moja la Timu 4 na Chungu Namba 1 kina Wenyeji Afrika Kusini, Mabingwa watetezi Zambia, Ghana na Ivory Coast.
++++++++++++++++++++++++++++++++
VYUNGU:
CHUNGU 1: South Africa, Zambia, Ghana, Ivory Coast
CHUNGU 2: Mali, Tunisia, Angola, Nigeria
CHUNGU 3: Algeria, Burkina Faso, Morocco, Niger
CHUNGU 4: Togo, Cape Verde, Congo DR, Ethiopia
FAHAMU: Kila Chungu kitatoa Timu moja ili kupata Makundi manne ya Timu 4 kila moja.
++++++++++++++++++++++++++++++++
Mgawanyo huu wa Vyungu umechukuliwa kwa kutathmini matokeo ya kila Nchi katika Mashindano matatu yaliyopita ya Kombe la Mataifa ya Afrika na si Ubora kwa mujibu wa Listi ya Ubora Duniani ya FIFA.
Lakini mgawanyo huu wa Vyungu unaweza kuleta ‘Kundi la Kifo’ la Nchi za Ivory Coast, Nigeria, Algeria au Morocco, na Congo DR.
Wakongwe Misri, waliowahi kuwa Mabingwa mara 7, na Cameroun, Mabingwa mara 4, hawamo kwenye Fainali hizi za AFCON 2013 baada ya kuzikosa kwa kutolewa kama vile walivyoikosa AFCON 2012.
Timu mpya pekee ni Cape Verde, waliowabwaga Cameroun, na zipo Timu 9, Zambia, Ivory Coast, Mali, Ghana, Tunisia, Burkina Faso, Morocco, Niger na Angola, ambazo zilicheza AFCON 2012 huko Gabon na Equatorial Guinea Januari Mwaka huu.
Mechi ya ufunguzi AFCON 2013 na Fainali zitachezwa Mjini Johannesburg na Mechi nyingine 29 zilizobaki zitapigwa katika Miji ya Durban, Nelspruit, Port Elizabeth na Rustenburg.

 

MABINGWA Chelsea CHALI, Man United yatoka nyuma 2-0 na kushinda!!


UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZ>>BARCA yapewa ushindi na ALBA Dakika za Majeruhi!
Mabingwa watetezi wa Ulaya, Chelsea, wamepigwa bao 2-1 ugenini na Shakhtar Donetsk na wenzao wa England, Manchester United, wakiwa kwao Old Trafford, walipindua uongozi wa Braga wa Bao 2-0 ndani ya Dakika 20 na kushinda 3-2 huku huko Nou Camp Celtic ilivunjwa moyo Dakika za majeruhi baada ya Jordi Alba kuifungia Barca bao la pili na kuwapa ushindi wa Bao 2-1.
MATOKEO:
Jumanne Oktoba 23
FC Nordsjælland 1 Juventus 1
FC Shakhtar Donetsk 2 Chelsea 1
FC BATE Borisov 0 Valencia 3
LOSC Lille 0 Bayern Munich 1
FC Spartak Moskva 2 SL Benfica 1
FC Barcelona 2 Celtic 1
Galatasaray 1 CFR 1907 Cluj 1
Manchester United 3 Braga 2
++++++++++++++++++++++++++++++
BARCELONA 2 CELTIC 1
Bao la Dakika za majeruhi la Jordi Alba limewapa ushindi Barcelona Uwanjani kwao Nou Camp baada ya Celtic ya Scotland kutangulia kwa bao moja ambalo alifunga Samaras na Iniesta kusawazisha kabla ya haftaimu.
VIKOSI:
Barcelona: Valdes, Adriano, Bartra, Mascherano, Jordi Alba, Xavi, Song, Iniesta, Sanchez, Messi, Pedro
Akiba: Pinto, Fabregas, Villa, Jonathan, Montoya, Sergi Roberto, Tello.
Celtic: Forster, Lustig, Wilson, Ambrose, Izaguirre, Samaras, Brown, Wanyama, Ledley, Mulgrew, Hooper
Akiba: Zaluska, Matthews, Miku, Commons, Rogne, Kayal, Forrest.
Refa: Gianluca Rocchi (Italy)
++++++++++++++++++++++++++++++
MAN UNITED 3 BRAGA 2
Javier Hernandez, ‘Chicharito’, alipiga bao mbili na Jonny Evans bao moja baada ya Man United kutoka nyuma kwa bao 2-0 za Braga ya Ureno zote zikifungwa na Alan ndani ya Dakika 20 na kupata ushindi wa bao 3-2 wakiwa kwao Old Trafford huo ukiwa ushindi wao wa 3 mfululizo kwenye Kundi lao.
VIKOSI:
Man United: De Gea, Da Silva, Carrick, Evans, Buttner, Kagawa, Fletcher, Cleverley, Rooney, Hernandez, van Persie
Akiba: Johnstone, Ferdinand, Anderson, Giggs, Nani, Young, Welbeck.
Braga: Beto, Leandro Salino, Nuno Andre, Paulo Vinicius, Elderson, Custodio, Hugo Viana, Ruben Amorim, Alan, Ruben Micael, Eder
Akiba: Quim, Mossoro, Helder Barbosa, da Solva, Baiano, Ze Luis, Anibal.
Refa: Milorad Mazic (Serbia)
++++++++++++++++++++++++++++++
SHAKHTAR DONETSK 2 CHELSEA 1
Mabingwa wa Ulaya, Chelsea, leo wamegalagazwa ugenini na Shakhtar Donetsk baada ya kupigwa bao 2-1.
Shakhtar walifunga bao zao kupitia Alex Teixeira, Dakika ya 3, na Fernandinho, Dakika ya 52, na Chelsea kupata bao lao pekee katika Dakika ya 88 mfungaji akiwa Oscar.
VIKOSI:
Shakhtar Donetsk: Pyatov, Srna, Kucher, Rakitskiy, Rat, Hubschman, Fernandinho, Alex Teixeira, Mkhitaryan, Willian, Luiz Adriano
Akiba: Kanibolotskiy, Stepanenko, Eduardo, Gai, Douglas Costa, Kryvtsov, Ilsinho.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Terry, Luiz, Cole, Oscar, Ramires, Mikel, Lampard, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Hazard, Sturridge, Cahill, Azpilicueta, Bertrand.
Refa: Damir Skomina (Slovenia)
++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
[MECHI ZOTE Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumatano Oktoba 24
FC Porto v FC Dynamo Kyiv
GNK Dinamo v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v FC Schalke 04
Montpellier Hérault SC v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v RSC Anderlecht [SAA 1 USIKU]
Málaga CF v AC Milan
AFC Ajax v Manchester City FC
Borussia Dortmund v Real Madrid CF
++++++++++++++++++++++++++

No comments:

Post a Comment