Thursday, October 18, 2012

NGASSA AAHIDI MAMBO YA HATARI SIMBA SC

Mrisho Ngassa; Nipeni muda muone mambo ya hatari


KIUNGO Mrisho Khalfan Ngassa, amesema kwamba bado anaizoea taratibu staili ya uchezaji ya timu yake mpya, Simba SC na nafasi mpya anayopangwa kwa sasa na anaamini hadi Januari mwakani atakuwa ameizoea na kufanya ‘mambo ya hatari’.
Akizungumza   jana, Ngassa alisema kwamba Simba wanacheza mfumo tofauti na ambao ulikuwa unatumiwa na timu yake ya zamani, Azam FC hivyo anaendelea kujifunza na kuizoea.
“Mchezaji unapoingia timu mpya, kawaida unakutana na mambo mengi mapya, inabidi sana ujifunze na kuzoea.  Unacheza na watu wapya, ambao inabidi ujifunze namna ya kucheza nao na kuzoeana nao,”alisema Ngassa.
Ngassa alisema angalau anekutana na wachezaji ambao anacheza nao timu ya taifa, lakini safu ya ushambuliaji ya Simba inaundwa na wachezaji wengi wa kigeni kama Emmanuel Okwi, Daniel Akuffo na Felix Sunzu.
“Inabidi sana nijifunze taratibu, hata hivyo najisifu kwamba naendelea vizuri na hadi kufika Januari hivi, nitakuwa nimekwishazoea na kufanya mambo ya hatari,”alisema Ngassa na kusistiza hajashuka kiwango, ni mazingira mapya tu.    
Ngassa juzi alifunga bao lake la tatu tangu ajiunge na Simba Agosti mwaka huu, akitokea Azam FC wakati Simba ikilazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kagera kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hiyo ikiwa sare ya pili mfululizo kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya Jumamosi pia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union mjini Tanga.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, kutokana na Azam FC kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya nane, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’ kutoka wingi ya kulia.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa ni Simba walioonekana kufanya mashambulizi ‘yenye akili’ zaidi.
Kipindi cha pili Simba ilirudi na moto tena na katika dakika ya 51, Mrisho Khalfan Ngassa aliifungia timu hiyo bao la pili kwa shuti kali lililowababatiza mabeki wa timu hiyo na kutinga nyavuni.
Baada ya hapo, Kagera walizinduka na kuanza kulishambulia lango la Simba kupitia pembeni na katika dakika ya 64 Themi Felix aliunganisha kwa kichwa krosi ya George Kavilla na kuifungia Kagera bao la kwanza.
Bao liliwazindua Kagera, ambao waliongeza kasi ya kulishambulia lango la Simba na katika dakika ya 66, Juma Nyosso alimkwatua kwenye eneo la hatari Paul Ngwai na Salum Kanoni akaenda kumtungua Juma Kaseja, akiisawazishia Kagera.
Baada ya hapo timu zilianza kushambuliana kwa zamu na mpira ulinoga zaidi kutokana na mashambulizi ya pande zote mbili.

AZAM WAPO CHAMAZI TANGU JANA USIKU TAYARI KWA KIPUTE NA JKT RUVU JUMAPILI

Kikosi cha Azam


AZAM FC imerejea Dar es Salaam jana majira ya saa 1:00 ikitokea Mbeya, ambako juzi ililazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Azam sasa wanaingia kambini kujiandaa na mchezo wao ujao, Jumapili dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Chamazi, maarufu kama Azam Complex, Dar es Salaam. 
Pamoja na sare hiyo, Azam wamelalamikia uchezeshaji mbaya wa marefa wa mechi hiyo, kwamba uliwapokonya ushindi.
Azam FC wanadai refa alikataa mabao yao mawili yaliyofungwa na Abdi Kassim ‘Babbi’ na penalti ya wazi, baada ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ kuangushwa kwenye eneo la hatari
Wanadai bao la kwanza, refa alilolikataa ulikuwa ni mkwaju wa mbali wa Abdi Kassim ambao ulitinga nyavuni, kabla ya kurudi uwanjani na refa licha ya kuona kuwa lilikuwa ni bao halali, bado akaamua kukataa
Wanadai baadaye, Sure Boy alifanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari na kwa mshangao wa wengi, wakiwemo viongozi na wachezaji wa Prisons ambao walishashika vichwa, refa akapeta na mpira kuendelea
Zikiwa zimesalia dakika chache kabla ya mpira kumalizika, Azam FC wanadai walipata adhabu ndogo na Abdi Kassim aliupiga mpira ule na kutinga nyavuni, lakini kwa mara nyingine tena refa akakataa bao kwa madai kuwa kabla ya kufunga, Babbi alikuwa ameotea.
Baada ya ‘kufanyiwa dhuluma’ hiyo, Azam wanaendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakiwa wana pointi 17, baada ya kucheza mechi sana, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wapo kileleni kwa pointi zao 18 na wamecheza mechi nane.  

BAHANUZI, YONDAN HAWAPO KESHO YANGA NA RUVU

Bahanuzi


BEKI Kevin Yondan na mshambuliaji Said Bahanuzi wataendelea kuwa nje ya Uwanja mwishoni mwa wiki, wakati timu yao, Yanga SC itakapokuwa ikiwania pointi tatu katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutokana na hali zao kutoimarika.
Wawili hao ambao ni majeruhi, wapo kwenye programu ya mazoezi mepesi na hadi jana hakuna mmoja kati yao aliyekuwa tayari kuanza programu kamili ya mazoezi ya kocha Mholanzi, Ernie Brandts.
Maana yake, Mbuyu Twite ataendelea kucheza pamoja na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika beki ya kati, wakati Jerry Tegete ataendelea kucheza na Didier Kavumbangu katika safu ya ushambuliaji.
‘Dogo’ Simon Msuva amemaliza adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa Oktoba 3, mwaka huu katika mechi dhidi ya Simba na Hamisi Kiiza amerejea kutoka Uganda, alipokwenda kuichezea timu yake ya taifa, The Cranes katika mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini.
Uganda ilitolewa na Zambia kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya jumla ya 1-1, Zambia wakianza kushinda nyumbani 1-0 na Uganda wakashinda kwao 1-0 pia mwishoni mwa wiki, hivyo mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti, ambako timu ya Kiiza ilitolewa.
Yanga imeweka kambi katika hoteli ya Uplands, Changanyikeni, Dar es Salaam huku ikiendelea kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Beki Kevin Yondan aliyeumizwa na kiungo wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ katika mechi baina ya wapinzani hao wa jadi, Oktoba 3, mwaka huu, wakati Bahanuzi ‘Spider Man’ alichanika nyama za paja la mguu wa kulia katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba Oktoba 8, mwaka huu.
Bahanuzi aliumia dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete katika mechi ambayo Yanga ililala 1-0, beo pekee la Themi Felix.
Bahanuzi ndiye tegemeo la mabao la Yanga kwa sasa, kwani tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, ameifungia mabao 12 katika mechi 13, ikiwemo ile dhidi ya Kagera aliyocheza kwa dakika 23 kabla ya kuumia na kutoka. 
Yanga kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 11, baada ya kucheza saba, kushinda tatu, sare mbili na kufungwa mbili.
Simba iliyocheza mechi nane, inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 18, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 17, iliyocheza mechi saba.



VPL: Wikiendi Taifa ni Yanga v Ruvu Shooting, Simba v Mgambo Tanga!

VPL_LOGOLIGI KUU VODACOM itanguruma tena Wikiendi hii na Jumamosi Vigogo Yanga, ambao sasa wameafikiana na Wadhamini VODACOM kuhusu Nembo kwenye Jezi zao, wapo nyumbani Uwanja wa Taifa, Dar es Saalam kucheza na Ruvu Shooting na Mahasimu wao Simba watacheza ugenini Jumapili huko Mkwakwani na Timu ‘íliyofufuka’ kwa kushinda Mechi 3 mfululizo, Mgambo JKT.
>>BONGO, KENYA-Sisi Sote ni Ndugu wapyaaa!
>>SIMBA v KAGERA: Watazamaji 9,842 watengeneza Milioni 58!!
RATIBA:


Jumamosi Oktoba 20
Yanga v Ruvu Shootings
Coastal Union v Mtibwa Sugar [Mkwakwani, Tanga]


Jumapili Oktoba 21
JKT Ruvu v JKT Oljoro [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mgambo JKT v Simba [Mkwakwani, Tanga]
Tanzania Prisons v Toto Africans [Sokoine, Mbeya]
++++++++++++++++++++++++++
Wakati huo huo, Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, na Shirikisho la Soka Kenya,FKF, wamefikia makubaliano ya kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuinua kiwango cha mpira wa miguu katika nchi hizo.
TAARIFA YA TFF:
Release No. 171
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 18, 2012



TFF, FKF ZAANZISHA USHIRIKIANO MPYA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) wamefikia makubaliano ya kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuinua kiwango cha mpira wa miguu katika nchi hizo.


Akizungumza baada ya mkutano uliowakutanisha vinara wa mashirikisho hayo Dar es Salaam jana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema wameamua kurejesha uhusiano huo uliokuwepo zamani baada ya kuwepo utulivu katika uendeshaji mpira wa miguu nchini Kenya.


Amesema maeneo ya ushirikiano ambayo wameagiza yafanyiwe kazi na sekretarieti za pande zote (TFF na KFF) ili baadaye yaingizwe katika Hati ya Makubaliano (MoU) ni mafunzo, waamuzi, mechi za timu za Taifa za wakubwa, vijana na wanawake, na Ligi Kuu.


Rais Tenga pia amesema wameamua kuwepo ziara za mafunzo (study tours) katika maeneo mbalimbali ambapo kwa Kenya wao Ligi Kuu yao iliingia katika mfumo wa kampuni mapema, hivyo itakuwa fursa nzuri kwa Bodi ya Ligi Kuu ambayo iko kwenye mchakato wa kuanzishwa kupata uzoefu kwa wenzao wa Kenya.


Naye Rais wa FKF, Sam Nyamweya aliyefuatana na Makamu wake wa Rais, Robert Asembo amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya ni wa kihistoria, hivyo wameamua kuuanzisha upya kwa faida ya nchi hizo.


Amesema hivi karibuni FKF ilichukua waamuzi kutoka Tanzania waliochezesha mechi ya kirafiki kati ya Kenya (Harambee Stars) na Afrika Kusini (Bafana Bafana), hivyo wameamua kubadilishana waamuzi kwa lengo la kuwaongezea uzoefu.


“Waamuzi wa Tanzania walichezesha vizuri mechi ile. Unajua kwetu kuna upinzani mkubwa katika klabu kama AFC Leopards na Gor Mahia, ukipanga refa utasikia wengine wanalalamika, mara huyo ni Mjaluo. Hata akichezesha vizuri bado watalalamika tu kutokana na upinzani uliopo katika klabu hizo,” amesema.


Rais Nyamweya ameongeza kuwa ili kuondoa malalamiko katika mechi za aina hiyo wanaweza kuchukua waamuzi kutoka Tanzania, na vilevile waamuzi kutoka Kenya wakachezesha mechi za aina hiyo nchini Tanzania.
Amesema vilevile wamepanga kuangalia uwezekano wa kuwa na mechi za kuandaa timu kabla ya kuanza Ligi Kuu za nchi hizo ambapo washindi watatu au wanne wa kwanza katika ligi hizo kushindana.


Kwa upande wa mafunzo, wamekubaliana kuwa kwa vile kila nchi ina wakufunzi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na la Afrika (CAF) watawatumia kuandaa mafunzo ya mara kwa mara kwa waamuzi, makocha, madaktari wa tiba ya michezo na viongozi badala ya kusubiri mafunzo ya aina hiyo kutoka kwa mashirikisho hayo ya kimataifa.



PAMBANO LA SIMBA, KAGERA SUGAR LAINGIZA MIL 58/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Kagera Sugar lililochezwa jana (Oktoba 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 limeingiza sh. 58,505,000.
Watazamaji 9,842 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000, na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 11,013,785.54 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,924,491.53.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 440,000, mtathimini wa waamuzi sh. 254,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
Umeme sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 3,183,890. Gharama za mchezo sh. 3,671,261.85, uwanja sh. 3,671,261.85, Kamati ya Ligi sh. 3,671,261.85, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,202,757.11 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,468,504.74.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
++++++++++++++++++++++++++


MSIMAMO VPL:
1 Simba Mechi 8 Pointi 18
2 Azam FC Mechi 7 Pointi 17
3 JKT Oljoro Mechi 8 Pointi 13
4 Kagera Mechi 8 Pointi 12
5 Yanga SC Mechi 7 Pointi 11
6 Coastal Mechi 7 Pointi 10
7 JKT Ruvu Mechi 8 Pointi 10
8 Prisons Mechi 7 Pointi 9
9 Ruvu Shooting Mechi 7 Pointi 9
10 JKT Mgambo Mechi 8 Pointi 9
11 Mtibwa Sugar Mechi 6 Pointi 8
12 Toto African Mechi 8 Pointi 7
13 African Lyon Mechi 8 Pointi 7
14 Polisi Moro Mechi 8 Pointi 2
 

LIGI za ULAYA: Zarudi tena kilingeni!


BORUSSIA_DORTMUND_JUKWAA>>LA LIGA, SERIE A & BUNDESLIGA ni moto Wikiendi!!
Kufuatia ‘vakesheni’ ya Wiki mbili ya Ligi huko Barani Ulaya kupisha Mechi za Kimataifa kwa mujibu wa Kalenda ya FIFA, Ligi Vigogo, zile za La Liga, Serie A na Bundesliga, zitarudi tena kilingeni Wikiendi hii na Bundesliga itakuwa ya kwanza dimbani kwa Mechi pekee ya Ijumaa Oktoba 19 kati ya TSG Hoffenheim na SpVgg Greuther Fürth ndani ya Rhein-Neckar-Arena.
ZIFUATAZO ni RATIBA na MISIMAMO ya Ligi hizo:

LA LIGA
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Jumamosi Oktoba 20
Málaga v Valladolid [Estadio La Rosaleda]
Real Madrid v Celta Vigo [Estadio Santiago Bernabéu]
Valencia v Athletic Bilbao [Estadio Mestalla]
Deportivo La Coruña v Barcelona [Estadio Riazor]


Jumapili Oktoba 21
Getafe v Levante [Coliseum Alfonso Perez]
Espanyol v Rayo Vallecano [Cornellà - El Prat]
Granada v Real Zaragoza [Estadio Los Cármenes]
Osasuna v Real Betis [Estadio El Sadar]
Real Sociedad v Atlético Madrid [Estadio Anoeta]


Monday, October 22, 2012
Sevilla FC v Mallorca [Estadio Ramon Sanchez Pizjuan]
================================
MSIMAMO:
[Timu za juu tu]
[Kila Timu imecheza Mechi 7]
1 Barcelona Pointi 19
2 Atletico Madrid 19
3 Malaga 14
4 Real Betis 12
5 Real Madrid 11
6 Real Mallorca 11
7 Sevilla 11
8 Real Valladoid 10
9 Getafe 10
10 Rayo Vallecano 10
================================



SERIE A
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Jumamosi Oktoba 20
Juventus v Napoli [Juventus Stadium]
Lazio v AC Milan [Stadio Olimpico]


Jumapili Oktoba 21
Cagliari v Bologna [Sant'Elia]
Atalanta v Siena [Atleti Azzurri d'Italia]
Chievo Verona v Fiorentina [Bentegodi]
Inter Milan v Catania [Stadio Giuseppe Meazza]
Palermo v Torino [Renzo Barbera]
Parma v Sampdoria [Ennio Tardini]
Udinese v US Pescara [Stadio Friuli]
Genoa v AS Roma [Luigi Ferraris]


MSIMAMO:
[Timu za juu tu]
[Kila Timu imecheza Mechi 7]
1 Juventus Pointi 19
2 Napoli 19
3 Lazio 15
4 Inter Milan 15
5 AS Roma 11
6 Fiorentina 11
7 Catania 11
8 Sampdoria 10 [Wamekatwa Pointi 1]
9 Genoa 9
10 Torino 8 [Wamekatwa Pointi 1]
11 AC Milan 7
================================


BUNDESLIGA
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Ijumaa Oktoba 19
TSG Hoffenheim v SpVgg Greuther Fürth [Rhein-Neckar-Arena]


Jumapili Oktoba 20
Bayer Leverkusen v Mainz [BayArena]
Borussia Dortmund v Schalke 04 [Signal-Iduna-Park]
Eintracht Frankfurt v Hannover 96 [Commerzbank-Arena]
Fortuna Düsseldorf v Bayern Munich [LTU Arena]
VfL Wolfsburg v SC Freiburg [Volkswagen Arena]
Werder Bremen v Borussia Monchengladbach [Weserstadion]


Jumapili Oktoba 21
Nurnberg v FC Augsburg [EasyCredit-Stadion]
Hamburg SV v VfB Stuttgart [HSH Nordbank Arena]
=================================


MSIMAMO:
[Timu za juu tu]
[Kila Timu imecheza Mechi 7]
1 Bayern Munich Pointi 21
2 Eintracht Frankfurt 16
3 Schalke 14
4 Borussia Dortmund 12
5 Hannover 11
6 Bayer Leverkusen 11
7 Fortuna Dusseldorf 10
8 Hamburger 10
9 Mainz 10
10 Borussia Dortmund 9
=================================
 

CAF CHAMPIONZ LIGI: Nani Fainali kujulikana Wikiendi hii!!


>>SAMATTA: Ataibeba Mazembe ugenini kuwafurahisha Wabongo?
NUSU FAINALI:
[MARUDIANO]
[SAA za BONGO]
Jumamosi Oktoba 20         
22:30 Espérance Sportive de Tunis v TP Mazembe [Stade El Menzah]


Jumapili Oktoba 21         
20:30 Al Ahly v Sunshine Stars [Cairo International Stadium]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Baada ya sare katika Mechi zote mbili za kwanza za Nusu Fainali za kusaka Klabu Bingwa Afrika, CAF CHAMPIONZ LIGI, Mabingwa watetezi Eseperance ya Tunisia na Vigogo Al Ahly wote wako nyumbani huku macho, masikio na dua za Watanzania wengi zikimwombea mwenzao Straika shupavu Mbwana Ally Samatta apate mafanikio kwa kuivusha Klabu yake Tout Poissant Mazembe ya Congo DR ugenini watakaporudiana na Esperance.
Wiki mbili zilizopita, TP Mazembe ikicheza nyumbani Lubumbashi ilitoka 0-0 na Esperance na safari hii huko Tunisia hamna budi ila magoli yapatikane ili kupata Mshindi atakaesonga Fainali.
Mazembe, ambao tegemezi lao ni Straika Samatta na Mputu, wataingia kwenye Mechi hii bila Stoppila Sunzu ambae ana Kadi na huenda wakawakosa majeruhi Rainford Kalaba na Hichani Himonde, wote wanatoka Zambia.
Tegemezi kubwa kwa Esperance ni Straika wa Ghana Harrison Afful, ambae Msimu uliopita ndie aliwapa Ubingwa kwa kufunga bao la ushindi kwenye Fainali, na Youssef Msakni.
Katika Mechi nyingine itakayochezwa bila ya Watazamaji huko Cairo, Misri, Al Ahly watakuwa nyumbani kuwakaribisha Sunshine Stars ambayo walitoka nayo sare ya bao 3-3 huko Ijebu Ode, Nigeria.
NUSU FAINALI:
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 6        
Sunshine Stars [Nigeria] 3 Al Ahly [Egypt] 3
Jumapili Oktoba 7         
TP Mazembe [Congo, DR] 0 Espérance Sportive de Tunis [Tunisia] 0
 

NAE Cole apigwa Faini…..SPAIN: Copa del Rey, Barca, Real kukutana Nusu Fainali??


ASHLEY_COLEHuko England, mara baada ya Nahodha wa Chelsea John Terry kunyoosha mikono juu na kukubali adhabu yake aliyopewa na FA ya kufungiwa Mechi 4 na Faini Pauni 220,000 huku akiomba radhi, mwenzake wa Chelsea Ashley Cole amepigwa Faini na FA ya Pauni 90,000 kwa kuikashifu kwenye Twitter wakati pia Klabu ya Chelsea imetangaza ‘kumshikisha adabu’ Terry kwa siri na huko Spain Droo ya Copa del Rey imefanywa na upo uwezekano kwa Mahasimu wakubwa, Real Madrid na Barcelona, kukutana Nusu Fainali.
>>KISIRISIRI: Chelsea yatangaza ‘kumshikisha adabu’ Terry kwa Ubaguzi!
>>‘KICK IT OUT’ yapinga Chelsea kumwadhibu kwa siri Terry!!
Chelsea na ‘Wabaguzi!’
Beki wa Chelsea na England, Ashley Cole, leo amepigwa Faini ya Pauni 90,000 na FA, Chama cha Soka England, kwa kosa la kutoa maneno yenye kashfa dhidi ya FA kwenye mtandao wa Twitter.
Cole, ambae alikubali makosa na kuomba radhi mara baada ya kushitakiwa, alitoa maneno hayo mara baada ya FA kumpata na kosa John Terry na kumwadhibu huku wakiuita ushahidi wa Ashley Cole kwenye Kesi hiyo kuwa hauaminiki na kuwapanga, kitu ambacho kilimwudhi Cole.
Wakati huo huo, Klabu ya Chelsea ambayo imekuwa ikilaumiwa na Wadau wanaopigania usawa kwenye Soka, Kundi la ‘Kick It Out’, ambalo hutaka ubaguzi utokomee kwenye Soka, imetangaza kuwa mara baada ya John Terry kuamua kutokata Rufaa kupinga adhabu yake, imemwadhibu Terry kwa ubaguzi lakini haiwezi kutangaza adhabu hiyo kwa vile ndio Msimamo wa Klabu yao kutotangaza adhabu za ndani ya Klabu.
Lakini Msimamo huu wa Chlesea umepingwa na Mwenyekiti wa ‘Kick It Out’, Lord Herman Ouseley, ambae amesema unaibomoa Chelsea na kuifanya ionekane si wa wazi kwenye Ubaguzi.



DROO ya COPA del REY
Huko Spain, FC Barcelona, Mabingwa watetezi wa Kombe la Mfalme, Copa del Rey, wamepangwa kukutana na Timu ya Daraja la chini Alaves kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 32 kwenye Drro iliyofanyika leo ambayo pia imepanga Mechi zote hadi hatua ya Nusu Fainali.
Timu nyingine ya Daraja la chini liitwalo Segunda B, Alcoyano, imepangwa kucheza na Mabingwa wa La Liga, Real Madrid, kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 32.
Wapinzani wa Barcelona, Alaves, wanakumbukwa sana pale kwenye Msimu wa Mwaka 2000/01 walipocheza vizuri na kufika Fainali ya UEFA CUP walipotolewa na Liverpool kwa Bao 5-4 katika Mechi iliyoamuliwa kwa ‘Goli la Dhahabu’ katika muda wa nyongeza.
Katika Droo hiyo ya leo, upo uwezekano kwa Mahasimu, Barcelona na Real Madrid, kukutana kwenye hatua ya Nusu Fainali ikiwa watashinda Mechi zao.
Msimu uliopita, Barca iliibwaga Real kwenye Robo Fainali ya Copa del Rey kwa jumla ya bao 4-3 katika Mechi mbili.
Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zinatakiwa kuchezwa Oktoba 31 na marudiano ni Novemba 28.
 

TERRY ASALIMU AMRI, akubali Kifungo Mechi 4, aomba Radhi!!


>>KUZIKOSA Spurs, Man United mara mbili na Swansea!
FREDINAND-TERRY_MKNO_HAMNAHatimae Nahodha wa Chelsea John Terry ameamua kutokata Rufaa kupinga Adhabu yake ya kufungiwa Mechi 4 na Faini ya Pauni 220,000 baada ya kupatikana na hatia na FA, Chama cha Soka England, ya kumkashifu kibaguzi Beki wa QPR Anton Ferdinand.
Uamuzi huu wa Terry, ambao umekuja katika Siku ya mwisho ya yeye kutakiwa akubali au apinge adhabu yake, unamaanisha atazikosa Mechi za Klabu yake Chelsea za Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham, Manchester United na Swansea City na pia Mechi ya CAPITAL ONE CUP dhidi ya Man United.
Tukio lililomsulubu Terry lilitokea Oktoba 23 Mwaka jana huko Uwanja wa Loftus Road kwenye Mechi ya Ligi ambayo QPR iliifunga Chelsea bao 1-0.
Baada ya hapo Kesi hiyo ilitinga Mahakamani baada ya Shabiki mmoja kupeleka malalamiko Polisi lakini Mwezi Julai Mahakama ya Westminster ilimwachia huru na hapo ndipo FA ikaamuru Jopo lake Huru la Nidhamu lisikilize Kesi hiyo na ndipo ikamtia hatiani baada ya kutoukubali utetezi wake.
Akikubali adhabu yake, Terry Miaka 31, amesema: “Naomba nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa kila mtu kwa lugha niliyotumia.”
Pia aliongeza: “Ingawa nimehuzunishwa na hukumu ya FA, ninakubali kuwa lugha niliyotumia, ukiachilia mbali mazingira yake, haikubaliki kwenye Uwanja wa mpira au popote pale maishani. Kama nilivyosema Mahakamani, ningekuwa najua nini kitatokea, lugha niliyotumia ni wazi haikufaa kwa Mtu wa nafasi kama yangu. Uamuzi uko chini ya kile Klabu ya Chelsea inataka na kwangu pia na hili halitarudiwa tena.’’
Hadi sasa Klabu ya Chelsea haijatoa tamko itamchukulia hatua gani Terry mbali ya kusema inasubiri uamuzi wa Terry kama atakata Rufaa au la.

No comments:

Post a Comment