Sunday, February 3, 2013

OBI MIKEL MCHEZAJI WA MWAKA WA GOAL.COM NIGERIA.


KIUNGO nyota wa kimataifa wa Nigeria na klabu ya Chelsea John Obi Mikel amekubali tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa mashabiki wa Nigeria waliopiga kura katika mtandao wa Goal.com. Asilimia 36.84 ya wasomaji wa mtandao huo nchini Nigeria walimpigia kura Obi Mikel ambaye alikuwa akipambanishwa na mchezaji mwenzake wa Chelsea Victor Moses huku wengine wakiwa ni Ahmed Musa, Kano Pillars na Rueben Gabriel wote wanacheza CSKA Moscow ya Urusi na John Utaka wa klabu ya Montpellier ya Ufaransa. Akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mhariri Mtendaji wa mtandao wa Goal.com nchini Nigeria Lalade Adewuyi, Obi Mikel aliwashukuru mashabiki na kueleza nia yake ya kuingoza nchi hiyo kunyakuwa taji la michuano ya Mataifa ya Afrika pamoja na nchi yao kutopewa nafasi hiyo. Nigeria ambayo itakwaana na Ivory Coast katika mchezo wa robo fainali ya Afcon baadae leo huku wadau wengi wa soka wakiipigia chapuo Ivory Coast iliyosheheni wachezaji nyota wanaong’ara kwenye vilabu mbalimbali barani Ulaya kusonga mbele katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment