Sunday, February 3, 2013

AL BADRY ASIKITIKA KUONDOKEWA NA NYOTA WAKE KADHAA.


MENEJA wa klabu ya Al Ahly ya Misri, Hossam Al Badry amebainisha kuwa alitaka kuachana na timu hiyo wiki iliyopita baada ya bodi ya klabu hiyo kuwauza kwa mkopo baadhi ya wachezaji wake nyota. Klabu hiyo iliwapeleka wa mkopo mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Mohammed Abo Trika katika klabu ya Baniyas ya Muungano wa Falme za Kiarabu-UAE pamoja na Ahmed Fathi na Mohammed Nagy Gedo katika klabu ya Hull City ya Uingereza. Al Badry amedai kuwa alitaka kuondoka mara tu nyota hao walipoondoka lakini hivi ameelewa kuwa ni kutokana na matatizo ya kifedha yanayoikabili klabu hiyo ndio maana bodi ikaamua kufanya hivyo. Kocha amesema anafikiri ataendelea kuwepo klabuni hapo ingawa hata hivyo amesikitishwa kuondokewa na nyota wake hao.

No comments:

Post a Comment