Tuesday, March 12, 2013

UCL: BARCA YAINYUKA AC MILAN 4-0, HAO ROBO FAINALI!!


UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZ>>TAYARI ROBO FAINALI: REAL, DORTMUND, JUVE, PSG, BARCA & GALATASARAY !
>>NANI KUUNGANA NAO MBILI KATI YA BAYERN, ARSENAL, MALAGA NA PORTO??
NDANI ya NOU CAMP, wakitakiwa waumwage ushindi wa AC Milan wa Bao 2-0 wa Mechi ya kwanza, Barcelona waliwatandika AC Milan Bao 4-0 na wao kutinga Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, kwa Jumla ya Mabao 4-2 kwa Mechi mbili.MESSI_ASHANGILIA_GOLI
Ushindi huu wa kishindo umemaliza kidogo majonzi ya vipigo vyao mfululizo hasa vile viwili toka kwa Mahasimu wao Real Madrid.
+++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Barcelona 4
-Messi  Dakika ya 5 & 40
-Villa 55
-Alba 90
AC Milan 0
+++++++++++++++++++++++++++
Alikuwa ni Supastaa Lionel Messi ambae alituliza nyoyo za Barcelona kwa kupachika Bao 2 katika Kipindi cha Kwanza na kuzifanya Timu hizi ziwe sare kwa Jumla ya Mabao 2-2 katika Mechi mbili.
Lakini Kipindi cha Pili, Barcelona waliimaliza kabisa AC Milan kwa kupiga Bao 2 nyingine zilizofungwa na David Villa na Jordi Alba.
VIKOSI:
Barcelona: Valdes; Dani Alves, Pique, Mascherano, Jordi Alba; Xavi, Busquets, Iniesta; Pedro, Messi, Villa
Akiba: Pinto, Fabregas, Puyol, Sanchez, Adriano, Song, Tello.
AC Milan: Abbiati; Abate, Mexes, Zapata, Constant; Ambrosini; Montolivo, Flamini; Boateng; Niang, El Shaarawy
Akiba: Amelia, De Sciglio, Muntari, Robinho, Nocerino, Bojan, Bonera.
Refa: Viktor Kassai (Hungary)
SCHALKE 2 GALATASARAY 3
HUKO Veltins-Areana Jijini Gelsenkirchen, Germany, Wenyeji Schalke, ambao walitoka sare ya Bao 1-1 na Galatasaray huko Uturuki katika Mechi ya kwanza, wametupwa nje ya UCL baada ya kuchapwa Bao 3-2 Uwanjani kwao.
+++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Schalke  2
-Neustadter  Dakika ya 17
-Michel Bastos 63
Galatasaray 3
-Altintop Dakika ya 37
-Yilmaz 42
-Umut Bulut 90
+++++++++++++++++++++++++++
Galatasaray sasa imetinga Robo Fainali ya UCL ikiungana na Real Madrid, Borussia Dortmund, Juventus, PSG na Barcelona huku Timu mbili za mwisho zinatarajiwa kupatikana baada ya Mechi za leo Jumatano Usiku.
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
RATIBA:
-Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumatano 13 Machi 2013
Bayern Munich v Arsenal [3-1]
Malaga v FC Porto [0-1]
+++++++++++++++++++++++++++
ROBO FAINALI:
Mechi ya 1=Tarehe 2 na 3 Aprili 2013
Mechi ya 2= Tarehe 9 na 10 Aprili 2013
NUSU FAINALI
Mechi ya 1= Tarehe 23 na 24 Aprili 2013
Mechi ya 2= Tarehe 30 Aprili  na 1 Mei 2013
FAINALI
25 Mei 2013
UWANJA wa WEMBLEY, London.
+++++++++++++++++++++++++++

No comments:

Post a Comment