Tuesday, March 12, 2013

BAAADA YA BARCA KUWEKA REKODI JANA KATIKA UCL YA BAO 4-0 DHIDI YA AC MILAN LEO TUNATARAJIA KUONA MAAJABU MENGINE KUTOKA KWA WASHIKA MITUTU WA LONDON ARSENAL DHIDI YA BAYERN MUNICH

>>ARSENAL KUGEUZA KIPIGO 3-1 NDANI YA ALLIANZ ARENA, MUNICH?
BAYERN_v_ARSENAL_SQUADSARSENAL, matumaini ya mwisho ya England kuikomboa Nchi hiyo balaa la kutokuwa na hata Timu moja kwenye Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI tangu Msimu wa 1995/6, leo Usiku wanatinga Allianz Arena Jijini Munich kuivaa Bayern Munich wakitakiwa kugeuza kipigo cha Bao 3-1 walichopewa katika Mechi ya kwanza ili wao kusonga mbele.

RATIBA:
-Mechi kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumatano 13 Machi 2013
Bayern Munich v Arsenal [3-1]
Malaga v FC Porto [0-1]

Lakini kazi hiyo kwa Arsenal ni ngumu sana na ugumu umeongezeka baada ya taarifa za kuumia kwa Kiungo wao tegemezi Jack Wilshere ambae atakuwa nje kwa Wiki 3 baada ya kuumia enka.
Pia Arsenal itamkosa Straika wao Lukas Podolski, alieumia enka, na Kipa Wojciech Szczesny ambae amepumzishwa.
Lakini kwenye Kikosi cha Wachezaji 18 walioenda Germany wamo Lukasz Fabianski, Abou Diaby, Andrey Arshavin na Kieran Gibbs ambao hivi karibuni walikuwa wakikosekana Kikosini.

KIKOSI CHA ARSENAL SAFARINI MUNICH:
Fabianski, Mannone, Jenkinson, Mertesacker, Vermaelen, Koscielny, Gibbs, Arteta, Coquelin, Ramsey, Diaby, Oxlade-Chamberlain, Rosicky, Cazorla, Walcott, Giroud, Gervinho, Arshavin

Arsenal hawataweza kumtumia Nacho Monreal kwa sababu alishaichezea Malaga hatua za Makundi ya UCL.
Huko Kambini Bayern Munich zipo habari kuwa Bayern Munich itawakosa Franck Ribbery, alieumia, Arjen Robbens, mwenye maumivu, pamoja na Schweinsteiger na Beki Jerome Boateng ambao wako Kifungoni.
Pia, Bayern haitakuwa na majeruhi wa muda mrefu Beki Holger Badstuber ambae atakuwa nje Msimu wote.
VIKOSI VINATARAJIWA:
BAYERN MUNICH: Manuel Neuer, Philipp Lahm, Daniel Van Buyten, Dante, David Alaba, Javier Martinez, Luiz Gustavo, Thomas Muller, Toni Kroos, Xherdan Shaqiri, Mario Mandzukic.
ARSENAL: Lukasz Fabianski, Bacary Sagna, Per Mertesacker, Laurent Koscieln, Thomas Vermaelen, Abou Diaby, Theo Walcott, Santi Cazorla, Mikel Arteta, Olivier Girou, Gervinho.
MALAGA V FC PORTO [Mechi ya kwanza 0-1]
Kocha wa Malaga Manuel Pellegrini amepatwa na wasiwasi kwa kuzagaa taarifa kuwa hii ndio Mechi kubwa kabisa katika historia ya Klabu hiyo wakiwania kupindua kipigo cha Bao 1-0 walichopewa na FC Porto huko Ureno katika Mechi ya kwanza na amekuwa na hofu hilo litaathiri Saikolojia ya Timu yake.
Huko Jijini Malaga kumekuwa na shamrashamra Msimu wote huu kwa kuiona Timu yao ikicheza kwa mara ya kwanza kwenye UCL na tena bila kufungwa katika Mechi zake zote za UCL Msimu huu hadi walipochapwa na FC Porto.
Ukubwa wa Mechi hii kwa Malaga umeongezeka maradufu kwao baada ya UEFA kuwafungia kucheza Ulaya kwa Misimu minne kuanzia Msimu ujao kwa kushindwa kulipa Madeni yao kwa Wachezaji na Wadau wengine.
Kwa sasa Malaga wako nafasi ya 4 kwenye La Liga wakiwa nyuma ya Vinara Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid.

ROBO FAINALI:
Mechi ya 1=Tarehe 2 na 3 Aprili 2013
Mechi ya 2= Tarehe 9 na 10 Aprili 2013
NUSU FAINALI
Mechi ya 1= Tarehe 23 na 24 Aprili 2013
Mechi ya 2= Tarehe 30 Aprili  na 1 Mei 2013
FAINALI
25 Mei 2013
UWANJA wa WEMBLEY, London.

No comments:

Post a Comment