Wednesday, March 13, 2013

RIO APONA RUNGU FA….MWENZAKE KULIVAA!! WILSHERE NJE WIKI 3!!!

>> MCDERMOTT AFUKUZWA READING!!
>>CHARLTON: “ROONEY HAONDOKI MAN UNITED!!”
WALCOTT_WILSHERE_OXBEKI wa Manchester United, Rio Ferdinand, amesalimika kuadhibiwa na FA,RIO_v_REAL Chama cha Soka England, kwa kosa la kumsukuma Fernando Torres wakati wa Mechi ya Man United na Chelsea waliyotoka sare 2-2 Old Trafford kwenye Robo Fainali ya FA CUP hapo Jumapili.
Lakini, Mchezaji mwenzake wa Man United ambae amenunuliwa hivi karibuni na yuko kwa Mkopo Crystal Palace, Chipukizi hatari Wilfried Zaha pamoja na Meneja wake wa Klabu hiyo, Ian Holloway, wamefunguliwa Mashitaka na FA kwa utovu wa Nidhamu uliotendeka kwenye Mechi kati ya Crystal Palace na Leeds United iliyochezwa majuzi Jumamosi.
Endapo Rio Ferdinand angefunguliwa Mashitaka na FA kwa kosa hilo la kumsukuma Torres, kitendo ambacho hakikuonekana na Refa Howard Webb, na angepatikana na hatia, basi angefungiwa Mechi 3 ambazo zingemaanisha lazima angezikosa Mechi za Marudiano ya FA CUP dhidi ya Chelsea na Dabi ya Manchester dhidi ya Man City inayochezwa hapo Aprili 8.
Inaaminika FA imeshindwa kumfungulia Ferdinand Mashitaka kwa vile Video zote zilizopatikana hazithibitishi mtitiriko wa kosa na hivyo kuweza kumhukumu.
Kuhusu Zaha, FA imetamka Chipukizi hiyo amefunguliwa Mashitaka kwa kuwaonyesha ishara ya kebehi Mashabiki wa Leeds wakati wa Mechi na Timu yake Crystal Palace.
Na Meneja wa Crystal Palace, Ian Holloway, ameshitakiwa kwa kauli zake kwa Waamuzi wakati wa Mechi hiyo hiyo kati ya Palace na Leeds.
Wote wamepewa hadi Ijumaa Machi 15 kujibu Mashitaka yao.
Jack Wilshere nje Wiki 3
WILSHERE_n_WENGERKiungo wa Arsenal, Jack Wilshere, atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 3 baada ya kuumia enka.
Kuumia kwa Wilshere kutamfanya aikose Mechi muhimu ya Arsenal na Bayern Munich itakayochezwa Jumatano huko Munich ikiwa ni marudiano ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, huku Arsenal ikiwa imechapwa Bao 3-1 katika Mechi ya kwanza.
Pia Wilshere, ambae sasa ni mmoja wa tegemezi wa England ingawa ameichezea Mechi 7 tu, atazikosa Mechi za Nchi hiyo za Mchujo wa kuingia Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil ambapo England itacheza na San Marino na Montenegro hapo Machi 22 na 26.
Akithibitisha kuumia kwa Wilshere, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ametangaza Kiungo huyo ana uvimbe kwenye enka yake.
Wilshere aliumia hiyo enka kwenye Mechi waliyofungwa na Tottenham 2-1 hapo Machi 3.
Brian McDermott atimuliwa Umeneja Reading
Klabu inayosuasua kwenye BPL, Barclays Premier League, Reading imemfukuza Meneja wao Brian McDermott.BRIAN_MCDERMOTT
McDermott, Miaka 51, ndie aliipandisha Reading Daraja Msimu huu lakini hivi sasa wapo kwenye kipigo cha 4 mfululizo kwenye BPL.
Kabu hiyo imetangaza kuwa Kocha wa Timu ya Chuo chao cha Soka, Eamonn Dolan, ndie atakaimu Umeneja kwa muda.
McDermott alijiunga na Reading Mwaka 2000 kama Msaka Vipaji na Kocha akifanya kazi chini ya Alan Pardew na Steve Copell na Mwaka 2009 aliteuliwa kama Meneja wa muda baada ya kufukuzwa Brendan Rodgers na baadae kuthibitishwa kama Meneja wa kudumu.
Mei 2012, Reading ilimilikiwa na Tajiri kutoka Urusi Anton Zingarevich ambae alinunua Hisa Asilimia 51 za Klabu hiyo.
Mwanzoni mwa Msimu huu Reading ilisuasua wakishinda Mechi 2 tu za BPL lakini mwanzoni mwa 2013 waliibuka na kushinda Mechi kadhaa na Mc Dermott kuteuliwa Meneja Bora wa BPL kwa Mwezi Januari.
Hata hivyo, vipigo toka kwa Stoke, Wigan na Everton na kufuaria kile cha Nyumbani cha 2-1 toka kwa Aston Villa hivi majuzi, kimewaacha Reading wakiwa nafasi ya 19 wakiwa na Pointi 23 sawa na Timu ya Mkiani QPR.
Wayne Rooney hauzwi asema Sir Bobby Charlton
FERGIE_N_CHARLTON1222Wayne Rooney atabaki Manchester United hadi amalize maisha ya Soka lake kwa mujibu wa Nguli Sir Bobby Charlton ambae ni Mkurugenzi Klabuni hapo.ROONEY_PENALTY
Uamuzi wa Meneja Sir Alex Ferguson kumpiga Benchi Rooney walipofungwa na Real Madrid Wiki iliyopita kulizua uvumi mkubwa wa kuhama kwa Mchezaji huyo kitu ambacho kilipingwa vikali na Ferguson.
Na sasa Charlton amesema: “Hamna njia ataruhusiwa kuhama kwa vile hivyo sivyo Sir Alex Ferguson anavyofanya kazi! Rooney ni Mfungaji Mabao wetu muhimu!”
Toka ahamie Old Trafford Mwaka 2009, Rooney ameshafunga Bao 167 katika Mechi 344 za Man United na kufunga Bao 33 katika Mechi 79 kwa England.
Lakini tangu Robin van Persie atue Old Trafford baada kunuliwa kwa Pauni Milioni 24 Agosti Mwaka jana kutoka Arsenal huku Straika huyo akipachika Bao 19 za BPL, nyota ya Rooney, aliefunga Bao 12 za Ligi, imefifia kidogo.
Hata hivyo, Charlton anategemea Rooney atang’ara tena kwani huwa anamudu changamoto.
Charlton amenena: “Sidhani kama changamoto hii ya Van Persie ni tatizo kwa Rooney. Ataibuka upya!”

No comments:

Post a Comment