GERRARD MCHEZAJI BORA WA MWAKA UINGEREZA.
KIUNGO nyota wa
kimataifa wa Uingereza na klabu ya Liverpool, Steven Gerrard ametajwa
kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo kwa ya pili. Gerrard
mwenye umri wa miaka 32 ambaye ni nahodha wa Uingereza na Liverpool
alikabidhiwa tuzo hiyo aliyopata kutokana na kura zilizopigwa katika
mtandao wa Chama cha Soka cha nchi hiyo na Sir Bobby Charlton jijini
Burton. Mshambuliaji
wa Manchester United Danny Welbeck alishika nafasi ya pili katika
kinyang’anyiro cha tuzo hizo huku nafasi ya tatu ikishikwa na beki wa
Chelsea Ashley Cole. Akihojiwa
mara baada ya tuzo hizo Gerrard amesema ni heshima kubwa kwake kupata
tuzo hiyo haswa ikizingatiwa aina ya wachezaji wa nchi hiyo na ubora wao
ulivyo. Wachezaji
wengine ambao wamewahi kushinda tuzo hiyo mara mbili ni pamoja na
kiungo wa Chelsea Frank Lampard na mshambuliaji wa United Wayne Rooney.
No comments:
Post a Comment