Thursday, January 3, 2013

KIGGI MAISHA MAGUMU SIMBA SC


KIGGI Makassy hafurahii maisha Simba SC na lolote linaweza kutokea juu yake wakati wowote.
Kiungo huyo aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu kutoka mahasimu Yanga, amekutana na kile amabcho alikimbia timu yake ya zamani, benchi mfululizo.
Katika mchezo wa juzi wa Kombe la Mapinduzi visiwani hapa, Kiggi alionyesha dhahiri kuchukizwa na kitendo cha kutolewa dakika ya 27 nafasi yake ikichukuliwa na Edward Christopher.
Akitoka kupiga maridadi iliyounganishwa nyavuni na Haruna Chanongo, Kiggi aliitwa benchi kumpisha Edward na alionekana kutoka kwa huzuni na alipofika benchi alikataa hata kupokea chupa ya maji aliyopewa.
Habari zaidi zinasema, tayari Kiggi amekwishaanza mishemishe za kusaka timu nyingine ya kwenda kuchezea baada ya kuona yupo katika wakati mgumu Simba SC.   
Simba SC leo inashuka tena dimbani kumenyana Tusker ya Kenya katika mchezo wa pili wa Kundi A, baada ya kushinda 4-2 dhidi ya Jamhuri ya Pemba juzi. Je, Kiggi atapangwa? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.

No comments:

Post a Comment