Wednesday, January 2, 2013

MAN U WAUANZA MWAKA WA 2013 KWA NEEMA NA BAADA MECHI ZA MWAKA MPYA, NINI WAMESEMA!

>>PULIS: "TOFAUTI YA STOKE NA CITY NI PAUNI MILIONI 220!!"
>>RVP: “NI TIMU SPESHO! NIMEZUNGUKWA NA MABINGWA!”
>>WENGER: “GEMU YETU ILIKOSA MALENGO!”
FERGIE_n_WENGER-KICHEKOMan City 3-0 Stoke
Meneja wa Stoke Tony Pulis: "Sina malalamiko, wao walikuwa Timu bora! Kuna Mtu aliniuliza nini tofauti kati ya Stoke na City na nilijibu Pauni 220 Milioni!” 
Wigan 0-4 Man Utd
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson: "Wigan ni Timu ngumu kucheza nayo kwao, kupata ushindi wa 4-0 ni matokeo mazuri kwetu! Javier Hernandez ni Mfungaji na ni Mchezaji hatari ndani ya boksi! Van Persie ni Mchezaji wa kipekee na Goli lake la kwanza lilikuwa zuri sana! Tulijua yeye Ni mchezaji bora na atatuongezea kitu hapa na hilo ndio amefanya!"
Robin Van Persie: “Hii ni Timu spesheli! Kila Mchezaji anamsaidia mwenzake! Sisi tunakabili Gemu kwa gemu lakini kila Mtu anataka kuwa Bingwa! Nahisi nimezungukwa na Mabingwa! Wanajua namna ya kushinda na hilo hufanya kazi yangu kuwa rahisi!”
Tottenham 3-1 Reading
Meneja wa Tottenham Andre Villas-Boas: "Tumefanya vyema kwa kumaliza Kipindi hiki kigumu cha Krismasi na Mwaka mpya kwa kupata Pointi 10 katika Mechi 4."
Swansea 2-2 Aston Villa
Bosi wa Aston Villa Paul Lambert: "Zikibakia Sekunde 30 unategemea ushindi! Tuna majeruhi wengi lakini Wachezaji wanahitaji pongezi! Tumetoka kipindi kigumu na matokeo haya yana afadhali!”
Southampton 1 Arsenal 1
Bosi wa Arsenal Arsene Wenger: “Hatukutengeneza nafasi nyingi baada ya kufunga 5 na Reading na 7 na Newcastle! Gemu yetu ilikosa malengo, tulishindwa kupenya, hatukuwa na spidi-sifa zote ambazo kawaida tunazo!”

No comments:

Post a Comment