Monday, January 7, 2013

WAKALA WA LAMPARD ASEMA LAZIMA AONDOKE KWANI VIONGOZI WAMEMCHOKA LAKINI MASHABIKI BADO WANAMTAKA.

 


Imethibitika kuwa Frank Lampard ataihama Chelsea mwishoni mwa msimu huu, kwa mujibu wa wakala wake Steve Kutner.
Akikaririwa na magazeti ya nchini Uingereza akisema,
"watendaji wa Chelsea walimwambia Frank kule Japan wakati wa michuano ya kombe la dunia la vilabu na hata mara baada ya ushindi dhidi ya Everton mwezi uliopita kuwa hakuna chochote kitakacho pelekea klabu kumpa ofa nyingine Lampard baada ya msimu huu"
"hakuna kitakacho badilika kwa vyovyote vile. Frank anapashwa kukubaliana na hayo inabidi ajikusanye kumalizia msimu kwa mafanikio katika klabu ambayo aliipenda sana."
Lampard alipata nguvu mpya kutokana na kushangiliwa na mashabiki wa Chelsea katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa michuano ya FA dhidi ya Southampton jumamosi pale alipofunga goli ambalo kimsingi lilimfanya kuwa sawa na mchezaji wa zamani klabu hiyo Kerry Dixon mwenye rekodi ya juu ya ufungaji magoli, lakini inaonekana sherehe ya ushangiliaji baada ya kufunga goli akiwa katika jezi yake maarufu namba 8 mgongoni inaelekea ukingoni.
Mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakitaka Lampard apewe mkataba mwingine lakini hali inavyo onekana ni kuwa hakuna nafasi nyingine ya kuendelea kusalia Stamford Bridge.
Mwenyewe Lampard amekaririwa akisema
"pengine sikuwa na mvuto wa kutosha lakini mashabiki wamekuwa na mimi katika kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja hapa"
Rodgers amtetea Suarez baada ya mpira wa mkono.
 Brendan Rodgers: 'Nadhani haikuwa makusudi ya mwamuzi'
Brendan Rodgers amesema goli la ushindi la Luis Suarez ambalo lilitokana na mpira uliotengenezwa kwa mkono kabla ya kufunga kwa mguu wa kulia halipaswi kuendelea kuzungumziwa aambapo pia amemsifia mshambuliaji huyo baada ya mchezo huo kati ya Liverpool na Mansfield.
Luis Suarez aliutuliza mpira kwa mkono kabla ya kufunga goli, ambalo lilikubaliwa na mwamuzi na kutoa matokeo ya ushindi wa kwa Liverpool.
Liverpool inajipanga na mchezo wa mzunguko wa nne wa michuano hiyo ya FA dhidi ya Oldham Athletic baada ya kupata goli la fuluku na kupelekea ushindi wa mabao 2-1 katika dimba la One Call Stadium.
Daniel Sturridge alifunga goli lake la kwanza katika timu yake mpya ya Liverpool dakika ya saba kabla ya Suarez kuandika bao la pili baada ya kuingizwa uwanjani kipindi cha pili.
 Kelele za kuzomea zilisikika uwanja mzima baada ya goli hilo kuruhusiwa, ambapo licha ya jitihada za wenyeji kuweka mpira kati na kuanza kwa lengo la kusawazisha jitihada zao hazikuza matunda ili kupata mchezo wa marudiano kule Anfield.
Akikaririwa Rodgers amesema,
"nimeona hakuna shaka yoyote kuwa ulikuwa ni mpira wa mkono, nadhani walichokiona waamuzi ni kuwa haikuwa makusudi, na ni wazi kabisa haikuwa makusudi.
"nilimuuliza mwamuzi wa akiba baada ya mchezo kama ulikuwa ni mpira wa mkono kwa kuwa sikuona moja kwa moja alinijibu ni kweli. Kwa hiyo ni wazi ilikuwa bahati mbaya kwa Mansfield na bahati kwetu kupata goli."

No comments:

Post a Comment