Wednesday, January 30, 2013

TOTO TUNDU’ BALOTELLI NJIANI KURUDI KWAO ITALY!!



>>INADAIWA MAN CITY IMEKUBALI KUMUUZA AC MILAN!!
BALOTELLI-WHY_ALWAYS_MEMABINGWA wa England, Manchester City, wameripotiwa kuwa wamekubali kumuuza Mchezaji wao makeke Mario Balotelli kwa AC Milan kwa Dau la Pauni Milioni 17.1.MANCINI_n_BALOTELLI-MSHIKEMSHIKE
Imeripotiwa kuwa Klabu hizo mbili zimefikia makubaliano ambayo malipo ya Dau la Uhamisho yatakuwa kwa awamu kwa Kipindi cha Miaka mitano.
Kabla ya kutua Man City, Balotelli alikuwa akiichezea Timu Mahasimu wa AC Milan, Inter Milan, ingawa yeye mwenyewe amekuwa akikiri tangu utoto wake ni Shabiki wa AC Milan.
Pia, inadaiwa Balotelli atakuwa akilipwa na AC Milan chini ya Mshahara aliokuwa akipata Man City wa Pauni 110,000 kwa Wiki na pia atasaini Mkataba wa Miaka minne.
Makubaliano ya Klabu hizo mbili yanagoja kuhitimishwa kwa Mchezaji huyo kupimwa afya yake huko Milan.
Msimu huu, Balotelli, mwenye Miaka 22, amekuwa hana namba ya kudumu na Man City na tangu Novemba amecheza Mechi 5 tu na Msimu huu ameifungia City Bao 1 tu kwenye Ligi.
Hivi karibuni, Balotelli na Meneja wa Man City Roberto Mancini walinaswa wakivutana Mashati wakati wa Mazoezi ya Timu hiyo na hilo likamfanya atimuliwe toka Timu ya Kwanza lakini baadae akarudishwa tena.
Ripoti za ndani ya Klabu ya Man City zimedai leo Balotelli alitinga Mazoezini mwa Man City na kuwaaga Wachezaji wenzake.

No comments:

Post a Comment