SHENHUA KUMSHITAKI DROGBA FIFA.
KLABU ya Shanghai
Shenhua ya China imedai kuwa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Ivory
Coast Didier Drogba hana haki ya kusaini mkataba katika klabu ya
Galatasaray ya Uturuki kwakuwa bado hajamaliza mkataba wake. Galatasaray
walithibitisha Jumatau kuwa Drogba mwenye umri wa miaka 34 ameshakubali
kusaini mkataba wa miezi 18 na klabu hiyo unaokadiriwa kufikia kiasi
cha euro milioni sita huku kiasi euro milioni nne akikabidhiwa nyota
huyo. Hatahivyo
Shenhua ambao walimsajili Drogba baada ya kuondoka Chelsea katika
kipindi cha majira ya kiangazi msimu uliopita walionyesha kushangazwa na
taarifa hizo na wameamua kulipeleka Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA
ili lipate ufumbuzi. Kwasasa
Drogba yuko ya timu yake ya taifa katika michuano ya Mataifa ya Afrika
inayoendelea nchini Afrika Kusini huku timu yake ikiwa tayari imesonga
mbele katika hatua ya robo fainali baada ya kushinda michezo yake miwili
ya kwanza.
No comments:
Post a Comment