Wednesday, January 30, 2013

COPA CLASICO: VIKOSI REAL v BARCA VINAJULIKANA LAKINI MAKIPA NANI??


>>NI ADAN v PINTO au LOPEZ v VALDES??
EL_CLASICO-KIPA_NANISIO SIRI, ndani ya Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya COPA del REY itakayochezwa Santiago Bernabeu Jumatano Usiku kati ya Mahasimu wakubwa Real Madrid na Barcelona, Mechi iliyobatizwa, COPA CLASICO, ni lazima Masupastaa Cristiano Ronaldo wa Real na Lionel Messi wa Barca, panga pangua, wamo Kikosini, lakini hadi sasa kitendawili kikubwa ni NANI WATAKUWA WAKILINDA NYAVU ZA TIMU HIZO MBILI?
Ni wazi Real Madrid watatinga kwenye hii EL CLASICO bila ya Wachezaji wao watano Pepe, Sergio Ramos, Casillas, Coentrao na Di Maria, ambao ni majeruhi na wengine Kifungoni, huku Barca ikiwakosa wawili tu, Eric Abidal na Jonathan Dos Santos.
++++++++++++++++++++++++++++++++
COPA del REY
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 30
[SAA 5 Usiku]
Real Madrid v Barcelona
Alhamisi Januari 31
[SAA 6 Usiku]
Atletico Madrid v Sevilla
MARUDIANO
Jumatano Februari 27
Sevilla v Atletico Madrid
Barcelona v Real Madrid
++++++++++++++++++++++++++++++++
Lakini kuumia kwa Nahodha na Kipa wao Nambari wani, Iker Casillas, kuliwalazimu Real Madrid Siku mbili tatu nyuma kumnunua Kipa mpya Diego Lopez kutoka Sevilla ingawa kabla ya kuumia Casillas, Meneja wa Real, Jose Mourinho, alianza kumtema Casillas na kumpa Namba Kipa Nambari mbili, Adan.
Lakini, hadi sasa, Kambi ya Real haijadokeza ni nani atapewa Namba kati ya Nambari mbili Adan na Kipa mpya Lopez.
Huko Barcelona pia upo utata wa nani atakuwa Kipa kwani chini ya Pep Guardiola walikuwa na utamaduni wa kuweka Kipa wao Nambari Wani, Valdes, kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na Jose Manuel Pinto kwenye Mechi zote za COPA del REY.
Wakiwa na Pinto golini, Barca walitinga Fainali 3 kati ya 4 na kutwaa COPA del REY mara mbili kati ya hizo.
Lakini tangu Kocha Tito Vilanova achukue mikoba ya Pep Guardiola, utamaduni huo wa kubadilisha Makipa kati ya Valdes na Pinto umekuwa haupo na hauna uhakika.
Wakati kukosekana kwa Mastaa watano wa Real, Pepe, Sergio Ramos, Casillas, Coentrao na Di Maria, kunaleta kitendawili kwa Kikosi cha Mabingwa hao wa Spain, huko Barca ni rahisi kuotea nini kitakuwa Kikosi chao ukiondoa nafasi ya Kipa.
Wakati Tito Vilanova bado ni mgonjwa, Barca watakuwa chini ya Kocha Msaidizi Jordi Roura, na pengine ugumu pekee kwake ni yupi aanze Fulbeki ya kulia kati ya Alves na Adriano, na ni rahisi kusema Masentahafu ni Pique na Puyol, Fulbeki kushoto ni Alba.
Katikati kwenye Kiungo ni Iniesta, Xavi, Fabregas na Busquets huku Mastraika ni Messi na Pedro.
NI EL CLASICO……COPA CLASICO!!!!

No comments:

Post a Comment