Thursday, January 3, 2013

STEWART AKIRI SELEMBE NOMA, LAKINI ASEMA HANA NAFASI AZAM


Selemba katika mechi ya jana, cheki kitu alichomfanya Khamis Mcha 'Vialli'
KOCHA wa Azam FC ya Dar es Salaam, Muingereza Stewart Hall amesifia kiwango cha kiungo wa zamani wa timu yake, Suleiman Kassim ‘Selembe’ ambaye kwa sasa anachezea Coastal Union ya Tanga kwamba kimepanda.
Pamoja na kusifia kiwango cha mchezaji huyo, Hall amesema kiungo hana nafasi Azam, kwa kuwa sasa ina wachezaji bora zaidi yake kama Kipre Herman Tchetche kutoka Ivory Coast na Brian Umony kutoka Uganda.
“Kweli ameimarika tofauti na alivyokuwa Azam, lakini sijutii kwa sababu kikosini nina wachezaji wazuri kama Kipre Tchetche na Umony, nitamkumbuka Selembe?”alisema.
Azam FC na Coastal Union jana zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.
Coastal leo ndio waliotawala mchezo na kupoteza nafasi kama tatu za wazi za kufunga mabao, kutokana na umakini mdogo kila walipopata nafasi hizo.
Azam walipata nafasi moja nzuri kipindi cha pili, lakini walinzi wa Coastal walisimama imara na kuondosha kwenye hatari jaribio hilo.
Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Salum Abubakar, Humphrey Mieno, Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche/Brian Umony dk 24 na Hamisi Mcha ‘Vialli’/Seif Abdallah dk 66. 
Coastal Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis ‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Hussein Twaha dk 50, Jerry Santo, Mohamed Mtindi, Soud Othman/Razack Khalfan dk90 na Danny Lyanga/Joseph Mahundi dk 90. 
Katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo, Miembeni iliitandika mabao 4-1 Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa mao Dze Tung.
Mabao ya Miembeni yalitiwa kimiani Adeyum Saleh Ahmed dakika ya 41 na 72, Mohamed Hamdani na Rashid Roshwa dakiaka ya 74, wakati la Mtibwa la kufutia machozi lilifungwa na Juma Mpakala dakika ya 10.

No comments:

Post a Comment