Wednesday, January 30, 2013

SIR ALEX KUMVAA PILATO FA!!


>>NI KUHUSU KAULI YAKE KWA REFA MSAIDIZI BAADA SARE NA SPURS!!
>>HADI IJUMAA ATAKIWA KUJIBU MASHITAKA!!
>>MACHI 2011 ALIFUNGIWA MECHI 5 AKIMTUHUMU REFA ATKINSON  KUIPENDELEA CHELSEA!!
FERGIE_na_MAJESHISIR ALEX FERGUSON amefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kufuatia kauli yake kuhusu Refa Msaidizi baada ya Timu yake Manchester United kutoka sare 1-1 na Tottenham kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Januari 20 Uwanjani White Hart Lane.
Ferguson alimyooshea kidole Refa Msaidizi Simon Beck kwa kushindwa kuashiria Penati baada ya Straika wake Wayne Rooney kuangushwa ndani ya Boksi.
Mara baada ya kauli ya Ferguson, FA ilimtaka Meneja huyo kujieleza na sasa imeamua kufungua Mashitaka rasmi na amepewa hadi Ijumaa Saa 1 Usiku, Bongo Taimu, kuyajibu.
Kauli ambazo zimemtia matatani Ferguson ni pale alipotamka: “Kulikuwa hamna njia Mshika Kibendera angeweza kutoa ile [Penati!]-aliwapa kila kitu! Kilikuwa kitu cha wazi na alikuwa Yadi 10 au 12 na hakutoa! Wao walipewa kila kitu!”
Pia alikumbushia tukio ambalo Refa Msaidizi Simon Beck alipowakatili Man United Aprili 2010 walipofungwa 2-1 na Chelsea kwa Mshika Kibendera huyo kutokutoa Ofsaidi ya wazi dhidi ya Didier Drogba aliefunga Bao la ushindi.
Kihistoria, Ferguson na FA wana misuguano ya muda mrefu na Machi 2011 alifungiwa Mechi 5 na kupigwa Faini Pauni 30,000 kwa kumtuhumu Refa Martin Atkinson kwa kuipendelea Chelsea.

No comments:

Post a Comment