Wednesday, January 30, 2013

BPL: MABINGWA MAN CITY WANASA KWA YA MKIANI QPR!

>>NEWCASTLE PEKEE YASHINDA, ZOTE DROO!!
>>LEO ARSENAL v LIVERPOOL, MAN UNITED v SOUTHAMPTON, READING v CHELSEA!
BPL_LOGOJANA USIKU, Mabingwa wa England, Manchester City, wakicheza ugenini na Timu ya mkiani mwa Ligi Kuu England, Queens Park Rangers, walitoka sare ya 0-0 na kubaki nafasi ya Pili wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Manchester United ambao leo wana nafasi ya kulipanua pengo hilo kuwa Pointi 7 ikiwa wataifunga Southampton Uwanjani  Old Trafford.
Kati Mechi 4 za Ligi Kuu England, Mechi pekee iliyotoa Mshindi ni ile ya Aston Villa na Newcastle na zote zilizobaki zilimazika kwa sare.
MATOKEO:
Jumanne Januari 29
Aston Villa 1 Newcastle 2
QPR 0 Man City 0
Stoke 2 Wigan 2
Sunderland 0 Swansea 0
++++++++++++++++++++
ASTON VILLA 1 NEWCASTLE 2
Newcastle United wameshinda hii vita ya Timu zinazosuasua na balaa kwa Aston Villa limezidi kuendelea kwa Meneja wao Paul Lambert ambae Wiki iliyopita ilitolewa kwenye Makombe mawili, Capital One Cup na FA Cup, na Timu za Madaraja ya chini.
+++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Aston Villa 1
-Benteke Dakika ya 49 (Penati)
Newcastle 2
-Cisse Dakika ya 19
-Cabaye 31
+++++++++++++++++++++
Papiss Cisse na Yohan Cabaye waliwapa Newcastle uongozi wa Bao 2 kabla Haftaimu lakini Penati ya Kipindi cha Pili ya Villa iliyofungwa na Christian Benteke haikutosha kuwakomboa na Newcastle wakapata ushindi wao wa kwanza tangu katikati ya Desemba Mwaka jana.
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Clark, Vlaar, Baker, Lowton, Westwood, Bannan, N'Zogbia, Bennett, Benteke, Bent
Akiba: Given, Ireland, Agbonlahor, Holman, Bowery, Weimann, Lichaj.
Newcastle: Krul, Debuchy, Steven Taylor, Coloccini, Santon, Perch, Cabaye, Gouffran, Sissoko, Gutierrez, Cisse
Akiba: Harper, Williamson, Anita, Yanga-Mbiwa, Bigirimana, Shola Ameobi, Sammy Ameobi.
Refa: Mike Dean
SUNDERLAND 0 SWANSEA 0
Sunderland na Swansea zilitoka sare katika gemu iliyopooza.
VIKOSI:
Sunderland: Mignolet, Gardner, Bramble, O'Shea, Colback, Johnson, N'Diaye, Vaughan, Larsson, Sessegnon, Fletcher
Akiba: Westwood, Bardsley, Wickham, Kilgallon, Mangane, McClean, Elmohamady.
Swansea: Tremmel, Tiendalli, Williams, Chico, Davies, Dyer, de Guzman, Britton, Hernandez, Shechter, Michu
Akiba: Cornell, Bartley, Graham, Lamah, Routledge, Rangel, Ki.
Refa: Andre Marriner
STOKE 2 WIGAN 2
Wigan walipigana kutoka Bao 2 nyuma kabla ya Haftaimu na kupata sare ya 2-2 walipocheza ugenini na Stoke City.
+++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Stoke 2
-Shawcross Dakika ya 23
-Crouch 48
Wigan 2
-McArthur Dakika ya 50
-Di Santo 61
+++++++++++++++++++++
Sare hiyo imewafanya Wigan wapande hadi nafasi ya 17 na hivyo kujinasua mkiani mwa zile Timu 3 za mwisho na kuziacha huko Aston Villa, Reading na QPR.
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Cameron, Shawcross, Huth, Whitehead, Whelan, Nzonzi, Adam, Etherington, Walters, Crouch
Akiba: Sorensen, Jones, Owen, Upson, Wilkinson, Shotton, Jerome.
Wigan: Al Habsi, Golobart, Caldwell, Figueroa, Boyce, McArthur, McCarthy, Espinoza, Beausejour, Maloney, Di Santo
Akiba: Robles, Jones, Henriquez, Gomez, McManaman, Stam, Mustoe.
Refa: Mike Jones
QPR 0 MAN CITY 0
Timu ya mkiani mwa Ligi Kuu England Queens Park Rangers imewasimamsha Mabingwa Manchester City kwa kutoka nao sare ya 0-0 na Shujaa wao ni Kipa wao Julio Cesar alieokoa mipira mingi.
Man City walitawala Kipingi cha Kwanza huku Pablo Zabaleta akipiga posti na shuti la Gareth Barry likiokolewa.
VIKOSI:
Queens Park Rangers: Cesar, Onuoha, Nelsen, Hill, Traore, Mbia, Derry, Fabio, Granero, Taarabt, Remy
Akiba: Green, Park, Ben Haim, Zamora, Murphy, Faurlin, Bothroyd.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Garcia, Lescott, Clichy, Milner, Barry, Nasri, Aguero, Silva, Tevez
Akiba: Pantilimon, Dzeko, Sinclair, Kolarov, Rodwell, Nastasic, Rekik.
Refa: Phil Dowd
RATIBA:
Jumatano Januari 30
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Liverpool
Everton v West Brom
Norwich v Tottenham
[SAA 5 Usiku]
Fulham v West Ham
Man United v Southampton
Reading v Chelsea
RATIBA MECHI ZA WIKIENDI:
Jumamosi Februari 2
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
QPR v Norwich
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Stoke
Everton v Aston Villa
Newcastle v Chelsea
Reading v Sunderland
West Ham v Swansea
Wigan v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Fulham v Man United
Jumapili Februari 3
[SAA 10 na Nusu Jioni]
West Brom v Tottenham
[SAA 1 Usiku]
Man City v Liverpool

No comments:

Post a Comment