Wednesday, January 9, 2013

SIMBA NA AZAM SASA NI LEO USIKU AMAANKATIKA KOMBE LA MAPINDUZI


Simba SC
CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimefanya marekebisho ya ratiba ya michuano ya Kombe la Mapinduzi na sasa Simba SC itamenyana na Azam FC katika Nusu Fainali ya kwanza leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Awali, leo ilikuwa Tusker FC icheze na Miembeni kwenye Uwanja huo, lakini sasa timu hizo zitamenyana kesho katika Nusu Fainali ya pili.
Mchezo huo utakuwa ni marudio ya Nusu Fainali ya mwaka jana, ambayo Azam FC waliitoa Simba SC kwa kuichapa mabao 2-1.
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Muingereza Kalimangonga Sam Daniel Ongala, maarufu kama Kali, amesema kwamba wamefurahia kukutana na Simba SC katika Nusu Fainali kuliko Tusker ya Kenya, kwa sababu hiyo itakuwa njia ya mkato kwao kuingia Fainali.
Kuelekea mchezo wa kesho, Kocha wa Miembeni, Salum Bausi amesema hawahofii Tusker na watawaonyesha kwamba mpira ni zaidi yua nguvu 
Nahodha wa Tusker, Joseph Shikokoti amesema kwamba haoni timu ya kuwazuia kutwaa Kombe la Mapinduzi.
Shikokoti aliyewahi kuchezea Yanga alisema kwamba anafahamu Simba na Azam ni wazuri na anajua mojawapo watakutana nayo fainali, lakini amesistiza hakuna kati yao inayoweza kuwazuia wasitwae Kombe.
“Hili Kombe letu, tumeona uwezo wa timu zote, hata Simba na Azam ni wazuri, lakini tutawafunga wote tukikutana nao, hawana uwezo wa kutuzuia,”alisema Shikokoti.
Azam FC

No comments:

Post a Comment