UCHAGUZI WA WANAWAKE TWFA MKOA WA TABORA KUFANYIKA KESHO TAREHE 17/12/2012
Uchaguzi wa wanawake mkoa wa tabora TWFA unatarajia kufanyika kesho tarehe 17/12/2012 kuanzia saa tatu asubuhi katika ukumbi wa shule ya taasisi mkoani tabora kusaka viongozi watakaowakilisha mkoa wa tabora ngazi ya wanawake.
Viongozi hao waliopitishwa katika usaili ni wagombea wanane nao ni ANNA MWINGIRA nafasi ya mwenyekiti,REHEMA ADAM RAJABU nafasi ya katibu mkuu,CHRISTINA WILLIAM FUNGAMEZA nafasi ya katibu msaidizi,CATHERINE BUNDALA nafasi ya mkutano mkuu TWFA tanzania.
Pia wamo ELEONORA BRUNO LUZIGA ,FATUMA JORAM PELEZI,ZENA MWAKASANGA na MWANAIDI OMARY katika nafasi ya mjumbe wa TWFA mkoa wa tabora.
Haya ameyabainisha mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi mkoa wa tabora bw. MUSSA NTIMIZI na kubainisha pia majina ambayo hayajapitishwa katika usaili kuwa ni ANNA ANTONY,STELLA ENOS, na THABIT ELIAS kw akutokidhi vigezo vya TWFA.
WAKATI HUO HUO amebainisha kuhusu Mikoa sita ambayo ni wanachama wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA) ambayo haitashiriki katika uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro.
Kwa mujibu
wa taarifa ya TWFA, ya wanachama hao hawatashiriki kwa vile hadi sasa haijapokea
taarifa za uchaguzi kwenye vyama hivyo. Vyama hivyo ni vya mikoa ya Arusha,
Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Shinyanga na Tabora kwa taarifa iliyotolewa jana na ofisa habari wa shirikisho la soka tanzania TFF.
Uchaguzi huo
utafanyika kwenye hoteli ya Midland, na wagombea ni Isabela Kapera, Joan Minja
na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na
Cecilia Mkafum (Katibu Mkuu), Zena Chande (Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na
Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji.
YANGA KUPAA DESEMBA 28, KULA MWAKA MPYA ULAYA
SIMBA SC YASISTIZA MUDDE NI MCHEZAJI WAKE HALALI
Mussa Mudde |
SIMBA SC
imesema kwamba Mussa Mudde ni miongoni mwa wachezaji wake wa kigeni wanne
ilionao kwa sasa na imeshangazwa sana na habari zilizoandikwa katika tovuti ya
supersport.com ya Afrika Kusini zikisema kwamba anarejea Sofapaka.
Akizungumza jana kutoka Uingereza, Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba Mudde ana mkataba wa
miaka miwili na Wekundu hao wa Msimbazi.
“Nashangaa
hizo habari wamezitoa wapi, huyu ni mchezaji wetu na mimi nilipoondoka Dar es
Salaam nilimuacha pale, ni vema wakati mwingine wakawa wanawasiliana na sisi
pia kutuuliza,”alisema Hans Poppe.
Wiki hii,
supersport.com imeandika kwamba Mudde anarejea Sofapaka baada ya kuona mambo
hayamuendei vizuri Simba SC.
Tovuti hiyo
ilimnukuu na rais wa Sofapaka, Elly Kalekwa ambaye alisema kwamba ameingia
mkataba wa miaka miwili na kiungo huyo mkabaji wa Mganda arejee Nairobi.
Mbali na
Mudde, wachezaji wengine wa kigeni ambao hadi sasa wana uhakika wa kuvaa jezi
za Simba SC ni kipa Abbel Dhaira, mshambuliaji Emmanuel Okwi wote kutoka Uganda
pia na beki Komalbil Keita kutoka Mali.
Kutoka
kikosi cha Simba kilichocheza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, wachezaji Felix
Sunzu kutoka Zambia, Daniel Akuffo kutoka Ghana na beki Paschal Ochieng kutoka
Kenya, wametupiwa virago.
Mudde
alisajiliwa tangu mwanzo wa msimu, lakini akaenguliwa kutokana na kuwa majeruhi
na hakucheza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, wakati Dhaira pia amesajiliwa wiki
iliyopita ili kuanza kazi Januari.
UCHOVU ULITUNYIMA USHINDI JANA, ASEMA KOCHA AZAM
Iddi Abubakar |
KOCHA wa
makipa wa Azam, Iddi Abubakar Mwinchumu amesema kwamba, jana walilazimishwa
sare ya 1-1 na Dragons ya hapa katika mchezo wa Kundi B kuwania Kombe la Hisani
kwenye Martyrs mjini hapa kutokana na uchovu wa safari na pia timu kucheza bila
makocha wake.
Akizungumza
baada ya mechi ya jana mjini hapa, Iddi alisema kwamba timu ilifika usiku sana
wa juzi na jana ikaingia uwanjani, hivyo wachezaji walikuwa wana uchovu, lakini
anaamini mechi ijayo kesho watashinda.
Aidha, Iddi
alisema pia timu kucheza bila makocha wake, ambao wamebaki Kenya nako kwa namna
moja au nyingine kulichangia matokeo hayo. “Ilikuwa ghafla tu, nikaambiwa Iddi
utaongoza timu katika mechi hii, nashukuru tumepata sare na tumecheza mpira
mzuri sana kila mtu ameona, ila kama makocha wangekuwapo tungecheza vizuri
zaidi na tungeshinda,”alisma Iddi ambaye ni kocha wa makipa Azam na kipa wa zamani wa timu hiyo.
Azam
ilicheza mechi hiyo bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na
Msaidizi wake, Kali Ongala ambao wamebaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari
Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche kutokana na
kukosa viza za kuingia DRC.
Katika mechi
ya jana, hadi mapumziko, wenyeji walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani
na mshambuliaji wao hatari, Nkate Jason dakika ya 24.
Nkate
alifunga bao hilo baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Azam, ambao
walichanganyana na kipa wao, Mwadini Ally. Pamoja na kufungwa, Azam walicheza
vizuri katika dakika 45 za kwanza na zaidi walikosa mipango tu ya kumalizia.
Hata hivyo,
mashambulizi ya pembeni ya wapinzani wao yalilitia misukosuko ya kutosha lango
la Azam katika ngwe hiyo.
Kipindi cha
pili Azam walirudi na kikosi kile kile, lakini walibadilika kiuchezaji na
iliwachukua dakika nne tu kukomboa bao, kupitia kwa Nahodha mpya, Jabir Aziz
aliyeunganisha pasi ya Abdi Kassim ‘Babbi’.
Baada ya bao
hilo, Azam waliendelea kushambulia lango la wapinzani wao, lakini safu ya
ulinzi ya Dragons ilisimama imara kudhibiti mashmbulizi hayo.
Katika
dakika ya 76, kipa Mwadini alipangua kwa uhodari mkubwa mkwaju wa penalti wa
Mukinzi Mawesi, baaada ya mchezaji huyo huyo kuangushwa kwenye eneo la hatari
na Ibrahim Mwaipopo.
Baada ya
hapo Azam walihamia langoni mwa Dragons, ambao safu yao imara ya ulinzi
iliwanusuru adhabu hii leo.
Azam ambao
ni washindi wa pili wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame
na Ligi Kuu, wamepangwa katika Kundi B pamoja na Dragons na Shark FC, ambayo
watacheza nayo Desemba 17.
Ikifuzu
kwenye kundi lake, Azam itaingia Nusu Fainali moja kwa moja, ambazo zitachezwa
Desemba 25 na Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa
tatu.
Kundi B,
lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa.
Kikosi cha
Azam jana kilikuwa; Mwadini Ally, Himidi Mao, Waziri Salum, Luckson Kakolaki,
David Mwantika, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Abdi Kassim, Gaudence Mwaikimba,
Abdallah Seif/Humphrey Mieno na Uhuru Suleiman/Zahor Pazi.
Azam wakiingia na wapinzani jana |
MAREKEBISHO YA KATIBA TFF YAPITA KWA KISHINDO
Rais wa TFF, Tenga |
WARAKA wa
marekebisho ya Katiba ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umepita baada ya
kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu waliopiga kura.
Jumla ya Wajumbe
waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 wameunga mkono wakati
waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa, hivyo
kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya marekebisho kikatiba.
Kura
zilizosema ndiyo kutoka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa vyama vya mikoa ni 46,
wajumbe kutoka vyama shiriki ni 13 wakati klabu za Ligi Kuu zilizounga mkono ni
11.
Kamati ya
Utendaji ya TFF inawashukuru wajumbe wote wa Mkutano Mkuu- kwa waliounga mkono
na waliokataa kwa vile walikuwa wanatekeleza wajibu wao wa kikatiba.
Vipengele
vilivyoingizwa ni ‘club licencing’ kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya Makamu wa
Pili wa Rais.
Vilevile
Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni
za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF.
Mkutano Mkuu
wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na 24
mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya
Mkutano Mkuu siku 60 kabla.
Wakati huo
huo: Mikoa sita ambayo ni wanachama wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania
(TWFA) haitashiriki katika uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Desemba 19
mwaka huu mjini Morogoro.
Kwa mujibu
wa taarifa ya TWFA, wanachama hao hawatashiriki kwa vile hadi sasa haijapokea
taarifa za uchaguzi kwenye vyama hivyo. Vyama hivyo ni vya mikoa ya Arusha,
Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Shinyanga na Tabora.
Uchaguzi huo
utafanyika kwenye hoteli ya Midland, na wagombea ni Isabela Kapera, Joan Minja
na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na
Cecilia Mkafum (Katibu Mkuu), Zena Chande (Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na
Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji. (Mwandishi wa Habari hizi ni Ofisa Habari wa TFF)
MAZOEZI YA TIMU YA TAIFA "TAIFA STARS" KATIKA KUJIANDAA NA MCHEZO WA KIRAFIKI DHIDI YA ZAMBIA DESEMBA 22 MWAKA JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA PICHA
VIJANA JAZZ WAIBUKA UPYA, WAIPUA MBILI KALI *Wamshukuru Rais Kikwete kwa kuwapatia vyombo vipya *Zilipendwa zao zakonga mashabiki Masae Bar, Kawe
DAR ES SALAAM, Tanzania
BAADA ya kuwa 'juu ya mawe' kwa muda
mrefu, bendi ya muziki wa dansi ya Vijana Jazz, 'Wana Air Pambamoto'
imeibuka upya kuanza kupiga muziki kwenye kumbi za starehe, huku ikiwa
imepua vibao viwili vipya kusuuza nyoyo za mashaki wake.
Ikipiga kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi
wa Masae Bar, Kawe wilaya ya Kinodoni jijini Dar es salaam, usiku wa
kuamkia leo, bendi hiyo imedhihirisha kwamba mashabiki wake wengi bado
wapo.
Kwenye ukumbi huo unaotazamana na
kilichokuwa kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packes, Vijana
Jazz ilithihirisha kuwa 'bado wamo', kwa kupiga nyimbo zake za zamani
zikiwemo 'Mary Maria', 'Mwsiho wa mwezi', 'Ngapulila' na 'mawifi',
zilizopigwa enzi za muasisi wa bendi hiyo, marehemu Ahmed Maneti katika
miaka ya 1980.
Nyimbo hizo ziliwafanya mashabiki wa
bendi hiyo, kucheza kwa hamasa kubwa huku baadhi yao wakifuatisha kuimba
samba mba na wanamuziki waliovuokuwa wakiimba jukwaani na wengine
kwenda jukwaani kutuza waimbaji.
Licha ya kuonyesha kuwa bendi hiyo bado
ni mahiri, wanamuziki wa zamani iliobaki nao ni Roshi Mselela, Nuru
Mhina (Baby White) na viongozi wa bendi Abdallah Mgonahazelu (Katibu) na
Saburi Athuman ambaye ni kiongozi wa bendi.
Vibao vibya ambavyo bendi hiyo imeipua
ni 'Utanieleza nini', utunzi wake kiongozi huyo na Kina mama wanaweza
uliotungwa na Mgonahazelu.
Athumani alisema, nyumbo hizo
zimesharekodiwa na hivi karibuni zitaanza kuingizwa sokoni, lakini
akasema bendi yake itafanya hivyo baada ya kuzipiga mara nyingi
majukwaani na kuzoeleka masikioni kwa mashabiki wao.
Alisema wakati kazi ya kuzirekodi nyimbo
hizo kwa ajili ya kiusikilizwa, imeshakamilika, sasa bendi imo katika
jitihada za kuzirekodi katika video ili ziweze kurushwa kwenye vipindi
vya Televisheni na pia kuuzwa kwa mashabiki.
"Tunamshukuru Rais Jakaya Kikwete
ametutoa juu ya mawe, hivi vyombo mnavyoona ametuwezesha mheshimiwa
Kikweye. Kwa kweli tunamshukuru sana", alisema Mgoma Hazeru wakati kabla
ya bendi hiyo kuanza kuiba wimbo wao mpya wa 'Utanieleza nini'.
Vijana Jazz ni moja ya bendi ambazo
Mratibu wa Budurano zote kwenye ukumbi huo wa Masae, Juma Mbizo, amesema
atakuwa anazitumia kutoa burudani kwa mashabiki. Nyingine ni kama
Msondo Band na FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma'.
AZAM YAANZA NA SARE KWA DRAGONS IKICHEZA BILA KOCHA
Mshambuliaji wa Azam, Gaudence Mwaikimba akiwatoka mabeki wa Dragons katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Hisani leo Uwanja wa Martyrs mjini Kinshasa, DRC. Timu hizo zilitoka 1-1. |
WAWAKILISHI
wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, (CAF), Azam FC wameanza
na sare ya 1-1 dhidi ya Dragons ya hapa katika mchezo wa Kundi B kuwania Kombe
la Hisani kwenye Martyrs mjini hapa.
Hadi
mapumziko, wenyeji walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na
mshambuliaji wao hatari, Nkate Jason dakika ya 24.
Nkate
alifunga bao hilo baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Azam, ambao
walichanganyana na kipa wao, Mwadini Ally. Pamoja na kufungwa, Azam walicheza
vizuri katika dakika 45 za kwanza na zaidi walikosa mipango tu ya kumalizia.
Hata hivyo,
mashambulizi ya pembeni ya wapinzani wao yalilitia misukosuko ya kutosha lango
la Azam katika ngwe hiyo.
Kipindi cha
pili Azam walirudi na kikosi kile kile, lakini walibadilika kiuchezaji na
iliwachukua dakika nne tu kukomboa bao, kupitia kwa Nahodha mpya, Jabir Aziz
aliyeunganisha pasi ya Abdi Kassim ‘Babbi’.
Baada ya bao
hilo, Azam waliendelea kushambulia lango la wapinzani wao, lakini safu ya
ulinzi ya Dragons ilisimama imara kudhibiti mashmbulizi hayo.
Katika
dakika ya 76, kipa Mwadini alipangua kwa uhodari mkubwa mkwaju wa penalti wa
Mukinzi Mawesi, baaada ya mchezaji huyo huyo kuangushwa kwenye eneo la hatari
na Ibrahim Mwaipopo.
Baada ya
hapo Azam walihamia langoni mwa Dragons, ambao safu yao imara ya ulinzi
iliwanusuru adhabu hii leo.
Azam
ilicheza mechi ya leo bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na
Msaidizi wake, Kali Ongala ambao wamebaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari
Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche kutokana na
kukosa viza za kuingia DRC.
Azam ambao
ni washindi wa pili wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame
na Ligi Kuu, wamepangwa katika Kundi B pamoja na Dragons na Shark FC, ambayo
watacheza nayo Desemba 17.
Ikifuzu
kwenye kundi lake, Azam itaingia Nusu Fainali moja kwa moja, ambazo zitachezwa
Desemba 25 na Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa
tatu.
Kundi B,
lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa.
Kikosi cha
Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Himidi Mao, Waziri Salum, Luckson Kakolaki,
David Mwantika, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Abdi Kassim, Gaudence Mwaikimba,
Abdallah Seif/Humphrey Mieno na Uhuru Suleiman/Zahor Pazi.
Azam wakishangilia bao la kusawazisha |
Sefi Abdallah wa Azam akchuana na beki wa Dragons |
Abdi Kassim ''Babbi' amemuacha mtu chini, anataka kuanza safari |
Uhuru Suleiman kulia anatafuta mbinu za kumtoka beki wa Dragons |
Mwaikimba anatafuta njia... |
Himid Mao aliyecheza beki ya kulia leo, akiupitia mpira miguuni mwa winga matata wa Dragons |
Soka tamu iliwafurahisha viongozi wa Azam, kulia Katibu, Nassor Idrisa na kushoto Mapwisa |
No comments:
Post a Comment