KIUNGO nyota wa
kimataifa wa Nigeria, John Obi Mikel amedai kuwa timu yake ya taifa
itaibuka kidedea katika michuano ya Mataifa ya Afrika inayoendelea
nchini Afrika Kusini baada ya kutinga hatua ya robo fainali. Nigeria
ilifanikiwa kutinga hatua hiyo jana baada ya kuibugiza Ethiopia kwa
mabao 2-0 na sasa wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Ivory Coast ambao
wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji la michuano hiyo kutokana nyota
wake waliosheheni kwenye kikosi chake. Obi
Mikel amesema kutokana na kiwango cha hali walichocheza katika mchezo
dhidi ya Ethiopia ana imani kuwa wanaweza kuvuka kikwazo kilichopo mbele
yao kama wakiendeleza juhudi zilezile. Nigeria imemaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi C ambalo linaongozwa na Burkina Faso.
No comments:
Post a Comment