Monday, January 21, 2013

LA LIGA: Real yatandika 5-0, yaifukuza Atletico!

BARCA_v_REAL

LA LIGA
MSIMAMO-Timu za JUU:
[Kila Timu imecheza Mechi 20 isipokuwa inapotajwa]
1 FC Barcelona Pointi 55
2 Atletico de Madrid          47
3 Real Madrid CF 40
4 Real Betis Mechi 19 Pointi 34
5 Malaga CF 32
6 Rayo Vallecano 31
7 Valencia 30
8 Levante 30
9 Real Sociedad 29

JANA, wakicheza ugenini na Levante, Real Madrid walishinda Bao 5-0 katika Mechi ya Ligi ya Spain, La Liga huku Nyota wao Cristiano Ronaldo na Angel Di Maria, wakipiga Bao 2 kila mmoja.

MAGOLI:
Valencia 0
Real Madrid 5
-Gonzalo Higuain Dakika ya 9
-Angel Di Maria 34 & 45
-Cristiano Ronaldo 36 & 41

Ushindi huo wa Real umewafanya wafikishe Pointi 40 wakiwa Pointi 7 nyuma ya Timu ya Pili Atletico Madrid ambao jana waliifunga Levante Bao 2-0 kwa Bao za Adrian Lopez Alvarez, Dakika ya 32 na Koke, Dakika ya 60.
Atletico Madrid wako Pointi 8 nyuma ya Vinara Barcelona ambao juzi walipoteza Mechi yao ya kwanza ya La Liga Msimu huu baada ya kuchapwa 3-2 na Real Sociedad.
MATOKEO:
Jumapili Januari 20
Malaga 1 Celta Vigo 1
Osasuna 2 Deportivo La Coruna 1
Real Valladolid 2 Real Zaragoza 0
Atletico Madrid 2 Levante 0
Valencia 0 Real Madrid 5

No comments:

Post a Comment