Thursday, January 17, 2013

MVUA KUBWA ILIYONYESHA NA KUSABABISHA MAFURIKO YASIMAMISHA MBIO ZA DAKAR.


MAFURIKO yamesababisha mashindano ya Dakar rally kusimamishwa jana lakini ufupi wa mbio hizo za hatua ya 11 bado umemuacha dereva Stephane Peterhansel kuendelea kuongoza zikiwa zimebakia siku tatu kufikia tamati ya mashindano hayo. Mito miwili iliyofurika iliwalazimu waandaaji wa mashindano hayo kusimamisha magari baada ya kilometa 53 katika kilometa 219 zilizokuwa zimepangwa katika hatua hiyo. Peterhansel ambaye alimaliza mbio hizo fupi akiwa katika nafasi ya sita alipewa dakika 52 zaidi ya Giniel de Villiers na kukaribia kunyakuwa taji lake la 11 la michuano hiyo inayofanyika Amerika Kusini. Kwa upande wa mbio za pikipiki nao walimaliza hatua hiyo fupi kabla ya mvua haijaanza kunyesha huku bingwa mtetezi Cyril Depres wa Ufaransa akijiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake mbele ya Ruben Faria wa Ureno.

No comments:

Post a Comment