Thursday, January 17, 2013

MAKOMBE ULAYA COPA del REY: Barca 2 Malaga 2, COPPA ITALIA: Fiorentina 0 AS Roma 1!

BARCA_v_REAL>>COPPA ITALIA-NUSU FAINALI: JUVE v LAZIO, INTER v AS ROMA!!
Barcelona, wakiwa kwao Nou Camp, wametoka sare ya 2-2 na Malaga katika Mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya COPA del REY walipomruhusu Ignacia Camacho kusawazisha Bao katika Dakika ya 90.
Katika Mechi nyingine ya Robo Fainali, Real Zargoza na Sevilla zilitoka 0-0.
Malaga ndio walitangulia kufunga katika Dakika ya 26 kwa Bao la Manuel Iturra na Barca kujibu haraka kwa Bao za Lionel Messi Dakika ya 29 na Carles Puyol Dakika ya 30 lakini Malaga, licha ya kucheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 75 baada ya Nacho Eraso kupewa Kadi Nyekundu, walisawazisha Dakika ya 90 kwa Bao la Ignacia Camacho.

COPA del REY
ROBO FAINALI
MATOKEO/RATIBA
Jumanne Januari 15
Real Madrid CF 2 Valencia 0
Jumatano Januari 16
Real Zaragoza 0 Sevilla 0
Barcelona 2 Malaga 2
Ijumaa Januari 18
[SAA 6 Usiku]
Atletico Madrid v Real Betis
Jumatano Januari 23
MARUDIANO
Sevilla FC v Real Zaragoza
Valencia v Real Madrid CF
Malaga v Barcelona
Real Betis v Atletico Madrid

COPPA ITALIA: Fiorentina 0 AS Roma 1
Bao la Dakika ya 97 la Mattia Destro, kufuatia sare ya 0-0 katika 90, limewapa AS Roma ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Fiorentina na kutinga Nusu Fainali ya COPPA ITALIA ambapo watachuana na Inter Milan.
Nusu Fainali nyingine ni kati ya Mabingwa wa Italy Juventus na Lazio.

COPPA ITALIA
NUSU FAINALI:
Jumanne Januari 22
SS Lazio v Juventus
Inter Milan v AS Roma
Jumanne Januari 29
Juventus v SS Lazio
AS Roma v Inter Milan

No comments:

Post a Comment