Monday, January 7, 2013

UNITED BADO YAMFUKUZIA ZAHA KIMYAKIMYA.


KLABU ya Manchester United bado inajiamini kwamba itamsajili kinda wa klabu ya Crystal Palace Wilfried Zaha pamoja na Tottenham Hotspurs kutangaza dau la kumyakuwa nyota huyo. Tottenham tayari wameshaanza mazungumzo na Palace kwa ajili ya uhamisho wa kinda huyo ambaye ana thamani inayofikia paundi milioni 20. Hata hivyo meneja wa Palace Ian Holloway ameonyesha wasiwasi kuwa kiwango cha Zaha hivi sasa kinaathiriwa na tetesi za usajili ambapo vilabu vikubwa vimekuwa vikipigana vikumbo kutaka saini yake. Meneja wa Tottenham Andre Villas-Boas ameonyesha kuwa tayari kumsajili kinda huyo na kisha kumruhusu kuendelea kucheza kwa mkopo kama klabu hiyo inavyotaka. Kwasasa meneja wa United Sir Alex Ferguson anatafuta nafasi ya kuzungumza ana kwa ana na Zaha ili aweze kumshawishi kutua katika klabu hiyo akiamini kuwa atamsaidia kinda huyo mwenye miaka 20 ili aweze kuwa tishio hapo baadae

No comments:

Post a Comment