Friday, January 18, 2013

MARCEDES KUONYESHA GARI ZAO MPYA ZA LANGALANGA FEBRUARI 4.


KAMPUNI ya Marcedes itatangaza rasmi magari yakayotumiwa na madereva wake nyota Lewis Hamilton na Nico Rosberg katika msimu mpya wa mashindano ya Langalanga wakati wa majaribio Februari 5 mwaka huu. Katika taarifa waliyotoa Marcedes katika mitandao ya kijamii ya facebook na twitter ilidai kuwa magari hayo mapya yatakayotumika mwaka huu aina ya F1W04 yataonekana Jumatatu ya Februari 4 katika majaribio kabla ya kuanza kwa msimu mpya katika Viwanja vya Jerez nchini Hispania. Hamilton ambaye ni bingwa wa dunia wa michuano ya langalanga mwaka 2008 alijiunga na Marcedes akitokea timu ya McLaren mwaka jana akichukua nafasi ya bingwa mara saba wa michuano hiyo Michael Schumacher aliyestaafu. Timu ya Marcedes ilimaliza msimu uliopita ikiwa katika nafasi ya tano na wanaamini kuwa usajili huo mpya wa Hamilton unaweza kuwasaidia kufanya vizuri zaidi mwaka huu. Timu zingine ambazo zitatangza magari yao mapya mapema ni pamoja na McLaren Januri 31, Ferrari Februari mosi na Red Bull pamoja na bingwa mara tatu katika misimu mitatu iliyopita Sebastian Vettel, Februari 3.

No comments:

Post a Comment