.
Liverpool
itaingia katika mbio za kumnasa Wesley Sneijder endapo kiungo huyo wa
kimataifa wa Uholanzi atakubali kupunguza mahitaji yake makubwa ya
mshahara anayotaka kwasasa.
ingawa
Sneijder anaonekana hafanani na sifa za aina ya wachezaji ambao
wamiliki wa Liverpool wa FSG wamekuwa wakiwalenga ambazo ni umri mkubwa
wa miaka 28 na gharama ya mshahara wa pauni milioni 6 kwa mwaka lakini
meneja wa klabu hiyo Brendan Rodgers ameonekana kumtamani kiungo huyo
nguli.
Galatasary
ndio klabu pekee kuonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo wa Inter Milan
na sasa wanataka majibu ya mpango wa mchezaji huyo hii leo.
Sneijder
anaonekana kuwa na wasiwasi juu ya kuelekea Uturuki na anadhani kuna
haja ya kucheza soka karibu na nyumbani Uholanzi kutokana na sababu za
kifamilia.
Inter
italazimika kuachia aondoke kwa pauni milioni £6.2 lakini kuelekea
Anfield itategemea na punguzo la mshahara uliotakiwa na Sneijder
mwenyewe.
Sneijder
anafahamu kuwa masiha yake ya soka katika klabu ya Milan yanafikia
mwisho mwezi huu lakini juu ya hatma yake ya baadaye amenukuliwa
akisema.
Na hapa amenukuliwa na Gazzetta dello Sport akisema
Na hapa amenukuliwa na Gazzetta dello Sport akisema
'Tazama
wachezaji wote ambao wako katika soko la uhamisho katika soko la
wachezaji kipindi hiki wanaaamua nini cha kufanya kabla ya January 31,
na mimi nitafanya hivyo o,'.
'sitaki kuharakisha na vilevile sitaki kuharakishwa.
'baada ya kila kitu kuwa kimekamilika sitaki kuwa katika fikra hizo za kulazimishwa kuchagua jambo la kimaisha.'
No comments:
Post a Comment