Monday, January 21, 2013

MAN UNITED YATUA QATAR KWA KAMBI YA SIKU 4!

!


FERGUSON_ASPIRE_ACADEMYVINARA wa BPL, Barclays Premier League, Manchester United, wametua Doha, Qatar kwa Kambi ya Mazoezi ya Siku 4 ambayo wataifanya kwenye Chuo cha Soka Aspire.
Man United walisafiri kwenda Qatar mara tu baada ya kutoka sare na Tottenham ya Bao 1-1 katika Mechi ya Ligi iliyochezwa White Hart Lane jana Jumapili na watakuwepo Qatar hadi Alhamisi ambako watarudi Jijini Manchester ili Jumamosi wacheze Mechi ya Raundi ya 4 ya FA CUP Uwanjani Old Trafford dhidi ya Fulham.
Hii ni Ziara ya pili ya Man United kwenye Chuo cha Aspire Mjini Doha, Qatar na ya kwanza waliifanya Januari Mwaka 2010.
Kikosi hicho cha Man United kikiongozwa na Meneja wao Sir Alex Ferguson kitanufaika na Mazoezi yasiyovurugwa na hali ya Baridi kali na Barafu ambayo sasa imeiandama Uingereza kwani Nchini Qatar sasa ni Bardi ya wastani ya Nyuzijoto 15 Centigrade huku Kijua kikichomoza Mchana kutwa.
Akiongelea safari hiyo, Ferguson alisema wanaridhika sana na Miundombinu ya Aspire na Hali ya hewa ya Qatar ni nzuri kwa Mazoezi.
Manchester United hawatacheza Mechi yeyote wakiwa Nchini Qatar.
+++++++++++++++++++++++++++++
FA CUP
RAUNDI YA 4
Ijumaa Januari 25
[SAA 4 Dak 30 Usiku]
Millwall v Aston Villa
Jumamosi Januari 26
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Stoke City v Manchester City
[SAA 12 Jioni]
Norwich City v Luton Town
Macclesfield Town v Wigan Athletic
Derby County v Blackburn Rovers
Hull City v Barnsley
Middlesbrough v Aldershot Town
Brighton & Hove Albion v Arsenal
Reading v Sheffield United
Huddersfield Town v Leicester
QPR v MK Dons
Bolton v Everton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Manchester United v Fulham
Jumapili Januari 27
[SAA 9 Mchana]
Brentford v Chelsea
[SAA 11 Jioni]
Leeds United v Tottenham Hotspur
[SAA 1 Usiku]
Oldham Athletic v Liverpool

No comments:

Post a Comment