Monday, January 21, 2013

CAPITAL ONE CUP: NI KIMBEMBE KWA CHELSEA NA VILLA, KUPINDUA VIPIGO?

>>KWA KANUNI, NI CHELSEA PEKEE KUNUFAIKA NA MAGOLI YA UGENINI MECHI YAO na SWANSEA!!
>>MAGOLI ya UGENINI KUANZA KUHESABIWA BAADA DAKIKA 120 TU!!
+++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
NUSU FAINALI
MARUDIANO
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumanne Januari 22
Aston Villa v Bradford [1-3]
Jumatano Januari 23
Swansea City v Chelsea [2-0]
FAINALI
Jumapili Februari 24
Uwanja wa Wembley, London
+++++++++++++++++++++++++
CAPITAL_ONE_CUP-BESTCAPITAL ONE CUP, zamani LIGI CUP au CARLING CUP, ipo hatua ya Nusu Fainali na Jumanne na Jumatano Usiku Mechi zake za marudiano zitachezwa huku kukiwa na mvuto mkubwa baada ya Chelsea kuchapwa 2-0 katika Mechi ya kwanza wakiwa nyumbani Stamford Bridge na Swansea City na Jumatano watakuwa huko Liberty Stadium kurudiana na Swansea City wakihitaji ushindi mnono ili watinge Fainali.
Jumanne ni marudiano Uwanjani Villa Park kati ya Aston Villa na Bradford City, Timu ya Daraja la chini huku Aston Villa wakihitaji kupindua kipigo cha Mechi ya Kwanza walipochapwa Bao 3-1.
Katika Mechi ya kwanza kati ya Chelsea na Swansea, makosa ya Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic yalimruhusu Michu kufunga Bao la kwanza na akarudia tena makosa yake na pasi yake ya nyuma kunaswa na Graham katika Dakika za mwishoni na kupachika Bao la pili.
KANUNI-JINSI MAGOLI YA UGENINI YANAVYOHESABIWA
Kwa mujibu wa Kanuni za CAPITAL ONE CUP, katika Mechi za Nusu Fainali, ikiwa idadi ya Jumla ya Magoli kwa Mechi mbili ni sawa mwishoni mwa Dakika 90, Mechi itakwenda muda wa Nyongeza wa Dakika 30.
Na ikiwa baada ya Dakika 120, idadi ya Jumla ya Magoli kwa Mechi mbili ni sawa, basi Mshindi atapatikana kwa kuhesabu kila Goli la ugenini mara mbili.
Lakini ikiwa bado, idadi ya Jumla ya Magoli ni sawa hata kwa kuchukulia Magoli ya Ugenini baada ya Dakika 120, basi Mshindi atapatikana kwa Mikwaju ya Penati tano tano.
Kwa misingi hiyo, katika Mechi kati ya Swansea City na Chelsea, ni Chelsea pekee ndio wanaweza kunufaika kwa Magoli ya ugenini na Swansea wao watahitaji ushindi au sare au kufungwa 1-0 ili kusonga mbele.
Ikiwa Chelsea watashinda 2-0, Mechi itaingia Dakika 30 za nyongeza na ikiwa bado ni 2-0 kwa Chelsea baada ya Dakika 120, Jumla ya Magoli kwa Mechi mbili ni 2-2 na hivyo Mikwaju ya Penati itaamua nani Mshindi.
Endapo Chelsea atashinda 3-1 katika Dakika 90, Mechi itaingia Dakika 30 za nyongeza na ikiwa bado 3-1 baada ya Dakika 120, Jumla ya Magoli itakuwa ni 3-3 na Magoli ya ugenini yatahesabiwa Dabo na Chelsea watasonga Fainali kwa Magoli ya ugenini bora.
Kanuni hizi pia, zitatumika sawia kwa Mechi ya marudiano kati ya Aston Villa na Bradford City ambapo Magoli ya Ugenini yataanza kuhuesabiwa tu baada ya Dakika 120 za Gemu.

No comments:

Post a Comment