Thursday, January 17, 2013

BAADA YA CHELSEA,MAN U ,MAN CITY KUMFUKUZIA KOCHA WA MAFANIKIO PEP GUARDIOLA JANA WALIPOKONYWA TONGE MDOMONI NA BAYERN MUNICH KW AMIAKA 3

PEP_GUARDIOLA>>ASAINI MIAKA 3 KUANZIA JUNI 2013!!
VIGOGO wa Ujerumani, Bayern Munich, wamethibitisha kuwa Kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola ndie atakuwa Meneja wao mpya kuanzia mwishoni mwa Msimu huu.
Guardiola, Miaka 41, amesaini Mkataba wa Miaka mitatu kuanzia Juni 2013.BAYERN_MUNICH_LOGO

WASIFU wa PEP GUARDIOLA:
KUZALIWA: 18 Januari 1971 Santpedor, Spain
KLABU ALIZOCHEZEA [Kiungo Mkabaji]:
-1983–1990 Timu ya Vijana Barcelona
-1990–1992 Barcelona B Mechi 59 Goli 5
-1990–2001 Barcelona Mechi 263 Goli 6
-2001–2002 Brescia Mechi 11 Goli 2
-2002–2003 AS Roma Mechi 4
-2003 Brescia Mechi 13 Goli 1
-2003–2005 Al-Ahli [Qatar] Mechi 18 Goli2
-2005–2006 Dorados [Mexico] Mechi 10 Goli 1
TIMU ya TAIFA:
-1991 Spain U21 Mechi 2
-1991–1992 Spain U23 Mechi 12 Goli 2
-1992–2001 Spain Mechi 47 Goli 5
-1995–2005 Catalonia Mechi 7
UMENEJA:
-2007–2008 Barcelona B
-2008–2012 Barcelona
-2013– Bayern Munich

Guardiola atachukua nafasi ya Kocha wa sasa Jupp Heynckes ambae atastaafu mwishoni mwa Msimu huu.
Kocha huyo kutoka Spain, aling’atuka mwenyewe kwa hiari yake Mei 2012 baada ya kuiongoza Barcelona tangu 2008 na kutwaa Mataji 14 yakiwemo mawili ya Ubingwa wa Ulaya.
Mtendaji Mkuu wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesema: "Pep Guardiola ni mmoja wa Makocha wenye mafanikio makubwa Duniani na tuna hakika si ataifanya Bayern peke yake ing’are lakini Soka lote la Germany!

No comments:

Post a Comment