Wednesday, January 2, 2013

VAN DER VAART ATENGANA NA MKEWE BAADA YA KUMSHUSHIA KIPIGO

.

KIUNGO nyota wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs na Real Madrid, Rafael van der Vaart ametengana na mkewe Sylvie baada ya nyota huyo kukiri kumpiga. Van der Vaart ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Hamburg ya nchini Ujerumani aliingia katika mzozo na mkewe wakatiwa shereheza kuukaribisha mwaka mpya na inaaminika kuwa alimpiga mbele ya wageni waliokuwepo katika sherehe ndogo waliyoandaa. Kiungo huyo alikiri kosa hilo na kudai kufanya jambo la kijinga na kuomba radhi wakati akihojiwa na gazeti moja nchini Ujerumani huku mke wake nae akidai kumsamehe mumwe huyo kwa kosa alilofanyiwa. Lakini pamoja na mkewe kumsamehe kiungo huyo wawili hao walitangaza kutengana baadae ikiwa ni wiki baada ya kufurahia sherehe za Noel wakiwa pamoja na mtoto wao Damian na kutuma picha ya pamoja katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

No comments:

Post a Comment