DEMBA BAAA AMEKAMILISHA USAJILI WAKE CHELSEA NA SASA NI MCHEZAJI HALALI WA THE BLUES,,AMENUNULIWA KWA PAUNDI MIL.7.5 TOKA NEWCASTLE
ALIYEKUWA mshambuliaji
nyota wa klabu ya Newcastle United, Demba Ba amekamilisha usajili wake
kwenda Chelsea huku kocha Alan Pardew akisisitiza kuwa nyota huyo
ameondoka kwa Baraka zote za klabu. Ba
mwenye umri wa miaka 27, mapema leo alikuwa kwenye mazungumzo na
Chelsea kuhusiana na maslahi yake binafsi baada ya klabu hiyo kukubali
kulipa kiasi cha paundi milioni 7.5 kwa Newcastle. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Senegal aliachwa katika kikosi kilichopambana na
Everton jana usiku na Pardew alifunguka kwa kusema mshambuliaji huyo wa
zamani wa West Ham United ameshakubaliana maslahi binafsi na Chelsea. Ba alijiunga na Newcastle mwaka 2011 akitokea West Ham na amefunga mabao 29 katika michezo 54 ya ligi aliyocheza. Newcastle
kwasasa inamfukuzia mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Ufaransa na
klabu ya Olympique Marseille, Loic Remy ili kuziba pengo la Ba
No comments:
Post a Comment