Monday, January 7, 2013

LIGI ULAYA: RONALDO AIOKOA REAL, BARCA HATARI, JUVE HOI!!

>>MESSI AANZA HESABU 2013 KWA PENATI, KIPA CASILLAS AANZA BENCHI!!
>>EDINSON CAVANI APIGA HETITRIKI, MFUNGAJI BORA SERIE A!!
BARCA_v_REALLIGI VIGOGO za Ulaya, Serie A na La Liga, Wikiendi zilirudi tena kilingeni na jana Jumapili huko Spain, Nyota Cristiano Ronaldo aliipigia Mtu 10 Real Madrid Bao 2 na kuipa ushindi wa 4-3 dhidi ya Real Sociedad huku vinara Barcelona wakizidi kupaa kwa kuichabanga Espanyol 4-0 katika Dabi ya Jiji la Barcelona lakini huko Italy vinara Juventus walishituliwa kwa kupigwa nyumbani Bao 2-1 na Sampdoria.
Ronaldo ainusuru Real!!
Jana Real Madrid, wakiwa kwao Santiago Bernabeu, walianza Mechi dhidi ya Real Sociedad huku Kipa Nambari Wani wa Spain, Iker Casillas, akianza Benchi kwa Mechi mbili mfululizo lakini ilibidi aingizwe baada ya Dakika 5 tu kufuatia kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu Kipa Adan Garrido na kuzaa Penati iliyoipa Real Sociedad Bao lao la kusawazisha baada ya Karim Benzema kuipa Real Bao la kuongoza katika Dakika ya Pili.
Katika Mechi hiyo Real Madrid walishinda Bao 4-3 na Bao nyingine kufungwa na Sami Khedira na mbili za Cristiano Ronaldo.
Bao zote 3 za Real Socied zilifungwa na Xabi Prieto.
Real Sociedad nao walimaliza Mtu 10 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Daniel Estrada aliepewa Kadi za Njano mbili.
Huko Nou Camp, Bao 4 ndani ya Nusu Saa ya kwanza za Xavi, Pedro, Bao 2, na Messi, kwa Penati, ziliwapa Barcelona ushindi wa Bao 4-0 dhidi ya Espanyol kwenye Mechi ambayo ni Dabi ya Jiji la Barcelona.
Ushindi huo umewafanya Barcelona wafikishe Pointi 52 wakiwa Pointi 11 mbele ya Timu ya Pili Atletico Madrid na Pointi 16 mbele ya Timu ya 3, Real Madrid ambao ndio Mabingwa watetezi.
Juve yabondwa, Cavani apiga Hetitriki kuizamisha AS Roma
Mabingwa na vinara wa Serie A Juventus walipatwa mshtuko baada ya kuchapwa 2-1 Uwanjani kwao na Sampdoria na kuuanza Mwaka 2013 vibaya.
Juventus ndio walitangulia kufunga kwa Penati ya Sebastian Giovinco katika Dakika ya 24 lakini Bao mbili za Straika kutoka Argentina Emanuel Icardi, Dakika ya 52 na 68, ziliwapa Sampdoria ushindi wa Bao 2-1.
Licha ya kufungwa Juventus bado wako kileleni wakiwa na Pointi 44 zikiwa ni Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili Lazio ambao Jumamosi waliifunga Cagliari 2-1.
Napoli wamepanda nafasi mbili hadi nafasi ya 3 baada ya kuichapa AS Roma 4-1 huku Straika wao kutoka Uruguay, Edinson Cavani, akipiga Hetitriki iliyomfanya aongoze katika Listi ya Mfungaji Bora akiwa na Bao 16 akifuatiwa na Mchezaji wa AC Milan, Stephan El Shaarawy, mwenye Bao 14.
SERIE A
MATOKEO:
Jumamosi Januari 5
Catania 0 Torino 0
Lazio 2 Cagliari 0
Jumapili Januari 6
AC Milan 2 Siena 1
Chievo Verona 1 Atalanta 0
Juventus 1 Sampdoria 2
Parma 2 Palermo 1
Udinese 3 Inter Milan 0
Napoli 4 AS Roma 1
Genoa 2 Bologna 0
Fiorentina 0 Pescara 2
LA LIGA
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Januari 4
Real Zaragoza 1 Real Betis 2
Jumamosi Januari 5
Sevilla FC 1 Osasuna 0
Levante 3 Athletic de Bilbao 1
Granada CF 1 Valencia 2
Deportivo La Coruna 1 Malaga CF 0
Jumapili Januari 6
FC Barcelona 4 RCD Espanyol 0
Celta de Vigo 3 Real Valladolid 1
Real Mallorca 1 Atletico de Madrid 1
Real Madrid CF 4 Real Sociedad 3
Jumatatu Januari 7
Rayo Vallecano v Getafe CF

No comments:

Post a Comment