Friday, January 18, 2013

BAO LA MKALI WA SIMBA NA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA WINGA TELEZA NGASA LAIPANDISHA TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA.


TANZANIA imekwea kwa nafasi sita katika vwango vya ubora vinavyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kutoka nafasi ya ya 130 waliyokuwepo mwezi uliopita mpaka nafasi ya 124. Timu tano bora kwa upande wa dunia zote zimebaki katika nafasi zao waliokuwepo mwezi uliopita ambapo wanaongoza na Hispania inayoshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na nchi za Ujerumani, Argentina, Italia na anayefunga orodha ya tano bora ni Colombia. Kwa upande wa Afrika, Ivory Coast imeendelea kuongoza huku ikishika nafasi ya 14 kwa uapnde wa dunia, ikifuatiwa na Algeria inayoshika nafasi ya pili pamoja na kuporomoka kwa nafasi tatu mpaka ya 24 kwa uapnde wa dunia. Nchi zingine za Afrika ni Mali iliyobaki katika nafasi yake ya 25 waliyokuwepo mwezi uliopita wakifuatiwa na Ghana waliopanda kwa nafasi nne mpaka nafasi ya 26 na tano bora kwa upande wa Afrika inafungwa na mabingwa wa Afrika Zambia ambao wamekaa katika nafasi ya 39 baada ya kuanguka kwa nafasi tano.

No comments:

Post a Comment