Thursday, January 17, 2013

BAADA YA KUBADILISHWA NAMBA NA KUCHEZA KAMA SENTEFOWARD SASA WENGER ASEMA NI ASILIMIA 99% WALCOT ATASAINI MKATABA MPYA KUITUMIKIA THE GUNNERS


Theo Walcott

Kocha wa Arsenal Raia wa ufaransa  Arsene Wenger amesema  "99%" anauhakika kuwa mshambuliaji wake  Theo Walcott atasaini kandarasi mpya klabuni hapo mwishoni mwa juma hili ambapo mambo yatakuwa yamekamilika Walcot  23, ambaye yupo katika miezi sita ya mwisho klabuni  hapo na anao uwezo wa kuondoka wakati wa kiangazi.
Laki ni wenger amesema kuwa kwa sasa ana asilimia 99 za kumbakisha mchezaji huyo .
"sikuwa na furaha pale niliposkia angeondoka "
"Imetuchukua muda kufika  hapa tulipotaka bado hatujalimaliza lakini itakuwa tayarai ndani ya juma hili" .
Walcott ndio mfungaji anaeongoza kwa arsenal akiwa amefunga magoli  14 .
Mchezaji huyo alikataa kandarasi ambayo angepewa ujira wa pauni  £75,000 lakini yeye alitaka kulipwa pauni laki moja kwa juma
Wenger bado anahusishwa  na kutaka kumsajiri winga wa  Crystal Palace  Wilfried Zaha, Mchezaji huyo Mwenye miaka 20 Aidha  mfaransa huyo amethibitisha kutaka kumsajiri mchezaji  , Taarifa zinasema kuwa Arsenal wako mbioni kumsajiri  mshambulijai wa Napoli mwenye miaka  25-Kutoka Uruguay   Edinson Cavani. 
huku akisema bei inaweza kupanda na ni jambo la kawaida  lakini inaweza kupungua siku za mwisho au saaa kdhaa kabla dirisha kufungwa 
 
 

No comments:

Post a Comment