Tuesday, October 2, 2012

Aguero: “Marefa wanabeba Wazawa”, Gerrard: “Ubingwa ni Miujiza!”

Jumatatu, 01 Oktoba 2012 18:00
   
Wakati Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard akikiri Liverpool kutwaa Ubingwa itakuwa ni miujiza, Straika wa Mabingwa Manchester City STEVEN_GERRARD_SHOUTINGanaetoka Argentina, Sergio Aguero, ameungama Marefa huko England wanawapendelea Wachezaji wa Kiingereza.
Gerrard na Ubingwa Liverpool
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard amesema itakuwa ni miujiza ikiwa Klabu hiyo itatwaa Ubingwa kabla hajastaafu.
Liverpool, ambao mara ya mwisho kutwaa Ubingwa wa England ilikuwa Mwaka 1990, wameuanza Msimu huu kwa kusuasua na wapo nafasi ya 14 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu.
Gerrard, Miaka 32, ametamka: “Itakuwa ni miujiza tukichukua Ubingwa kabla sijastaafu.”
Gerrard amekiri kuibuka kwa Timu kama Manchester City na kutwaa Ubingwa ndiko kumezidisha zaidi ugumu wa Liverpool kutwaa Taji hilo.
++++++++++++++++++++++++++++
Gerrard na Liverpool:
>>Aligunduliwa akichezea Timu ya Whiston Juniors akiwa na Miaka 9.
>>Alisaini Mkataba wa kuwa Mchezaji wa Kulipwa wa Liverpool Mwaka 1997.
>>Novemba 1998 alichezea Liverpool mara ya kwanza Mechi na Blackburn. >>Mwaka 2001 alishinga ‘TREBO’ Kombe la Ligi, FA Cup na UEFA Cup.
>>Octoba 2003 ralimbadili Sami Hyypia na kuwa Nahodha wa Liverpool.
>>Alipiga Bao na kuisaidia Liverpool kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2005
>>Alipiga Bao mbili Liverpool ilipotwaa FA Cup Fainali na West Ham Mwaka 2006.
>>Octoba 2008 alipiga Bao lake la 100 kwa Liverpool Mechi na PSV Eindhoven.
>>Asaini Mkataba mpya utakaombakisha Liverpool kama Balozi akistaafu.
++++++++++++++++++++++++++++
Amesema: “Si Manchester United na Arsenal pekee, sasa wapo Man City, Chelsea na Tottenham. Newcastle nao wamekuja.”
Aliongeza: “Tulikuwa wa 8 Msimu uliopita. Kama Msimu huu ukienda vyema, tukiwa na bahati pia na kupanda kidogo, tunaweza kufikia 4 bora. Lakini hata kama tukifika 4 bora nitakuwa na Miaka 33 mwishoni mwa Msimu na hiyo ndio maana tunahitaji miujiza kuwa Mabingwa kabla sijastaafu. Lakini nitaendelea kupigana na tutaona nini kitatokea!”


Sergio Aguero na Marefa
Sergio Aguero, Straika wa Manchester City anaetoka Argentina, anaamini Wachezaji wa Kiingereza wanapendelewa na Marefa ukilinganisha na wale kutoka nje.
Aguero ametamka: “Huwa sipendi kujihusisha na matatizo ya Marefa. Lakini hapa Marefa wanapendelea Wachezaji wa England. Lakini hatuna la kufanya ila kuendelea kucheza tu!”
Tuhuma hizi za Aguero zinafuatia matukio kwenye Mechi ya Ligi Kuu kati ya Fulham na Man City ambayo Wachezaji wenzake kutoka Argentina, Pablo Zabaleta na Carlos Tevez, walidai Penati baada ya kufanyiwa madhambi lakini Refa hakutoa.
Lakini alipohojiwa kama hadhani kuwa Wachezaji wa nje ya England huwa wanajidondosha kuhadaa Marefa, Aguero alijibu: “Pengine ndio. Inatokea lakini hapa si sawa wengine hupendelewa!”
Madai haya ya Aguero yamekuja Wiki tu baada ya Wachezaji wa England wanaochezea Liverpool, Steven Gerrard na Glen Johnson, kutamka kuwa Mchezaji mwenzao wa Liverpool anaetoka Uruguay, Luis Suarez, ni mhanga wa sifa yake mwenyewe na ndio maana Marefa hawamsapoti na kumpa Penati kutokana na sifa yake ya kuhadaa Marefa kwa kujiangusha ovyo.
Mara ya mwisho kwa Aguero kupewa Penati ni Mwezi Machi walipocheza na Arsenal na tangu wakati huo Marefa wamekuwa hawampi na wakati mwingine kumtwanga Kadi ya Njano kwa kujidondosha.

No comments:

Post a Comment