Tuesday, October 2, 2012

QPR yadidimizwa mkiani!

Jumanne, 02 Oktoba 2012 10:46
 
BPL_LOGO>>MECHI YAWEKA REKODI: KADI za NJANO 8 Mechi moja Timu moja!
West Ham wamezidi kumletetea mchecheto Meneja wa Queens Park Rangers Mark Hughes wakati jana walipotua nyumbani kwao Loftus Road na kuwatandika bao 2-1 na kuwaacha wakimaliza Mechi hiyo wako Mtu 10 na pia kuendelea kubaki mkiani mwa Msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kuambulia Pointi mbili tu katika Mechi 6.
++++++++++++++++++++++++++
KADI za KIHISTORIA:
• West Ham ndio Timu ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu England kupata Kadi za Njano 8 katika Mechi moja.
• QPR wamezoa jumla ya Kadi Nyekundu 10 tangu mwanzo mwa Msimu wa 2011-12 ambazo ni Kadi 3 zaidi ya Timu nyingine yeyote.
++++++++++++++++++++++++++
West Ham walianza vyema na kupata bao katika Dakika ya 3 tu alilofunga Matt Jarvis na Ricardo Vaz Te akapiga bao la pili kabla ya mapumziko.
++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
QPR 1
-Taarabt 57′
WEST HAM 2
-Jarvis 3′
-Vaz Te 35′
++++++++++++++++++++++++++
Baada ya mapumziko, QPR wakazinduka na kukaza buti hasa baada ya kuwaingiza Adel Taarabt na Samba Diakite, na Taarabt ndie alieipa QPR bao lao moja kwa shuti kali na zuri.
Hata hivyo, QPR walipata dosari pale Samba Diakite alipobandikwa Kadi za Njano mfululizo na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Ushindi huu umewapaisha West Ham hadi nafasi ya 7 na kuleta faraja kwa Meneja Sam Allardyce ambae pia alifurahi kurudi Uwanjani kwa Straika wake mpya wa mkopo kutoka Liverpool, Andy Carroll, ambae alumia katika Mechi yake ya kwanza kuichezea West Ham na jana alimudu kucheza Dakika 20 za mwisho.


VIKOSI;
Queens Park Rangers: Julio Cesar, Hill, Onuoha (Hoilett - 84' ), Nelsen, Park Ji-sung (Diakite - 55' ), Wright-Phillips (Taarabt - 56' ), Granero, Faurlin, M'bia, Cisse, Zamora
Akiba: Green, Diakite, Taarabt, Ephraim, Ehmer, Mackie, Hoilett

West Ham United: Jaaskelainen, Reid (Tomkins - 23' ), O'Brien (McCartney - 35' ), Collins, Demel, Nolan, Jarvis, Noble, Diame, Cole, (Carroll - 72' ), Vaz Te
Akiba: Henderson, McCartney, Tomkins, Benayoun, O'Neil, Carroll, 11 Maiga
Refa: Clattenburg
Watazamaji: 17,363

No comments:

Post a Comment