TUPENI FEDHA ZETU NA CHA JUU YAISHE, SIMBA WAWAAMBIA AZAM
Hans Poppe |
SIMBA SC
imesema haitaki ugomvi wala malumbano na Azam FC, bali wanataka warudishwe
fedha zao zote walizotoa kumsaini mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa, Sh.
Milioni 55 pamoja na faida juu.
Azam FC jana
imemuuza Mrisho Khalfan Ngassa kwa dola za Kimarekani 75,000 (Sh. Milioni 120)
kwenda El Merreikh ya Sudan ambako amesaini mkataba wa miaka miwili,
utakaomuwezesha kulipwa mshahara wa dola za Kimarekani 4,000 (Sh Milioni 6,) kwa
mwezi huku naye akilipwa dola 50,000 (Sh. Milioni 75) za kusaini.
Akizungumza kwa njia ya simu jana kutoka Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba wao walimsajili
mchezaji huyo kwa taratibu, ila wanashangaa sasa Azam wanataka kufanya mambo
kinyume cha utaratibu.
“Sisi tuna
mkataba na huyu mchezaji, ambao tulisaini na wao Azam, ambao ilikuwa kama
kuununua mkataba wake wa kule Azam, baada ya wao wenyewe kushindwana na huyo
mchezaji. Tuliwapa Sh. Milioni 25 na baadaye tukaongeza naye mchezaji mkataba
wa mwaka mmoja, tukampa Sh. Milioni 30,”alisema Hans Poppe.
Kapteni huyo
Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), alisema kwa kuwa hawataki
malumbano na Azam, wanaomba warejeshewe fedha zao na faida kidogo, kwani
mchezaji huyo amenunuliwa akiwa anachezea Simba SC.
Awali,
Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu Ngassa wenye thamani ya dola
100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said Bakhresa akakataa akisema
utambana mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu nyingine.
Sasa, Ngassa
baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge
mwishoni mwa wiki hii, atakwenda Sudan kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na
klabu hiyo, ambayo ni jambo la kawaida kucheza hatua ya makundi ya michuano ya
klabu Afrika.
Azam
walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu baada ya kukerwa na
kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika
Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi
ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alifanya
hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam
kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara
nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa
kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa baadaye
Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji huyo Azam
FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni 30, kati
ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 akipewa gari.
NGASSA: SIMBA PANDENI DAU NIBAKI MSIMBAZI
Mrisho Ngassa |
Akizungumza
hapa, Ngassa alisema kwamba yeye kama mchezaji anaangalia maslahi na kwa
mshahara mzuri pamoja na dau nono la usajili alilopewa Matajiri wa Sudan
amelainika na kukubali kujiunga nayo.
Wakati Azam
FC imemuuza Ngassa kwa dola za Kimarekani 75,000 kwenda El Merreikh ambako
amesaini mkataba wa miaka miwili, kiungo huyo mshambuliaji amepewa dau la
kusaini mkataba wa miaka miwili, dola 50,000 na atakuwa analipwa mshahara wa
dola 4,000 kwa mwezi.
Awali,
Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu Ngassa wenye thamani ya dola
100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said Bakhresa akakataa akisema
utambana mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu nyingine.
Sasa Ngassa
baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge
mwishoni mwa wiki hii, atakwenda Sudan kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na
klabu hiyo, ambayo ni jambo la kawaida kucheza hatua ya makundi ya michuano ya
klabu Afrika.
Azam FC
imesema imeweka mbele maslahi ya mchezaji na taifa kwa ujumla katika maamuzi ya
kumuuza Sudan, kutoka Simba alikokuwa akicheza kwa mkopo. “Hii timu (Merreikh)
kila mwaka inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, maana yake
huyu mchezaji atakwenda kupata maendeleo na kuja kuisaidia zaidi Tanzania
katika mashindano ya kimataifa,”alisema kiongozi mmoja wa Azam.
Alipoulizwa
kuhusu Simba SC aliyokuwa anaichezea klabu hiyo, kiongozi huyo alisema wao
walimtoa kwa mkopo Ngassa kwenda kwa Wekundu wa Msimbazi hadi Mei 31, mwakani
na mkataba wao ndio unasema hivyo.
“Sisi
tuliwapa Simba huyu mchezaji kwa mkopo hadi Mei 31 na wakatupa Sh. Milioni 25,
ila tuko tayari kuwarudishia fedha zao walizota, lakini huyu mchezaji ni mali
yetu na hata TFF wa natambua hilo, na
tumekwishamuuza Merreikh,”alisema.
Alipoulizwa
kuhusu Simba kusaini mkataba mpya na Ngassa, alisema; “We uliona wapi dunia
nzima timu inapewa mchezaji kwa mkopo halafu inamsainisha mkataba? Simba lazima
ifike wakati waache kurudia makosa, haya ndio mambo ya Mbuyu Twite
sasa,”alisema kiongozi huyo wa Azam.
Azam
walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu baada ya kukerwa na
kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika
Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi
ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alifanya
hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam
kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara
nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa
kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa
baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji
huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni
30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 akipewa gari.
Ngassa
anang’ara katika Challenge ya mwaka huu mjini hapa, hadi sasa akiwa amefunga
mabao matano sawa na John Bocco wa Azam na wafungana kileleni.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
John Bocco Tanzania 5
Mrisho
Ngassa Tanzania 5
Brian Umony Uganda 3
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
Chris
Nduwarugira Burundi 3
Geoffrey
Kizito Uganda 2
Robert
Ssentongo Uganda 2
Khamis Mcha Zanzibar 2
David
Ochieng Kenya 2
Clifton
Miheso Kenya 2
Dadi Birori Rwanda 2
SELEMBE AWAPA MALARIA + WAKENYA, TAZAMA REKODI YA HARAMBEE NA HEROES TANGU 1977
Kikosi cha Zanzibar, Selembe wa kwanza kushoto walioinama, |
Mashabiki wa
soka wa Kenya waliopo hapa na baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka nchini humo,
wamekuwa wakimzungumzia Selembe kama mchezaji hatari na aliyebeba hatima yao
leo.
“Selembe,
yule mchezaji yupo kama Fellaini
(Marouane) ni hatari sana yule, kwa kweli amebeba hatima yetu, tukiweza kumbana
yule, Zanzibar wala hawafurukuti,”alisema mmoja wa mashabiki wa Kenya juzi
mjini hapa, akimfananisha kiungo huyo na kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye
asili ya Morocco, anayechezea Everton ya England.
Kenya na
Zanzibar zinamenyana katika Nusu Fainali ya kwanza kwenye Uwanja wa Mandela
leo, mchezo ambao utafuatiwa na mechi nyingine kati ya Uganda na Tanzania Bara.
Kenya
wanaonekana kuihofia mno Zanzibar kiasi cha kuthubutu kuwarejesha kambini
wachezaji wake wawili iliyowarudisha nyumbani kwa utovu wa nidhamu, Paul Were na
Kevin Omondi.
Baada ya
kuifunga 1-0 Sudan Kusini katika mchezo wa pili wa Kundi A, wachezaji hao
walikwenda kujirusha kwenye klabu ya usiku na kurejea kambini na wanawake,
jambo ambalo lilifanya asubuhi yake wapandishwe ndege wote kurejea Nairobi,
lakini kutokana na mchecheto wa mechi ya kesho, wamerejeshwa.
Kocha wa Harambee
Stars, James Nandwa aliliomba Shirikisho la Soka Kenya (FKF) liliwarejeshe
wachezaji hao kwa ajili ya Nusu Fainali.
Kocha wa Fisa
FC, Charles ‘Korea’ Omondi, ambaye amekuwa akifanya mazoezi na wachezaji hao
tangu warejeshwe nyumbani, amethibitisha wamebadilika kinidhamu na wako vizuri
kimchezo.
Were na
Omondi wapo kwa mkopo AFC Leopards na Gor Mahia kutoka timu inayoshiriki Ligi
ya Jimbo la Nairobi, Fisa FC.
Mara ya
kwanza na ya mwisho timu hizi kukutana katika hatua ya mtoano ilikuwa ni mwaka
1979 nchini Kenya, katika Nusu Fainali na wenyeji walishinda 2-0 Novemba 14
Uwanja wa Nyayo, Nairobi na mara zote zimekuwa zikikutana katika hatua ya
makundi.
Na mara ya
mwisho kabisa kukutana katika mashindano haya timu hizi ilikuwa ni mwaka 1996
nchini Sudan na Kenya ilishinda 1-0.
Kwa ujumla,
timu hizi zimekutana mara 11 tangu kuanzishwa rasmi kwa michuano ya Challenge
mwaka 1974 na Kenya imeshinda mechi saba, sare tatu na imefungwa moja. Kenya
imeifunga Zanzibar jumla ya mabao 17, wakati yenyewe imefungwa saba.
REKODI YA KENYA NA ZANZIBAR CHALLENGE
P W D L GF GA Pts
Kenya 11 7 3 1 17 7 24
Zanzibar 11 1 3 7 7 17 6
REKODI YA KENYA NA ZANZIBAR TANGU
1977:
Novemba 24, 1996; Sudan Kundi B
Kenya 1-0
Zanzibar
Novemba 27, 1995; Uganda Kundi A
Kenya 2-0
Zanzibar
Novemba 30, 1991; Kundi B Uganda
Kenya 3-2
Zanzibar
Desemba 6, 1989; Kundi B
Kenya
Zanzibar 0-0
Kenya B
Desemba 14, 1987; Kundi A Ethiopia
Kenya 0-0
Zanzibar
Desemba 6, 1984; Kundi B Uganda
Kenya 1-0
Zanzibar
Novemba 21, 1982; Kundi B
Uganda
Kenya 2-2
Zanzibar
Novemba 17, 1981; Kundi A Tanzania
Kenya 2-1
Zanzibar
Novemba 22, 1980; Kundi B Sudan
Kenya 1-2
Zanzibar
Novemba 14, 1979; Nusu Fainali Kenya
Kenya 2-0
Zanzibar
Desemba 2, 1977; Kundi A Somalia
Kenya 3-0
Zanzibar
STARS NA UGANDA PATACHIMBIKA LEO NAMBOOLE, KIKOSI CHA LEO NA REKODI YA MECHI ZOTE ZILIZOPITA BAINA YA TIMU HIZO
TANZANIA
Bara, Kilimanjaro Stars leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole
mjini hapa kumenyana na wenyeji, Uganda, The Cranes katika Nusu Fainali ya
Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kuanzia
saa 12:00 jioni.
Mchezo huo,
utatanguliwa na mechi nyingine ya hatua hiyo kati ya Zanzibar na Kenya, ambayo,
itaanza saa 10:00 jioni.
Hii inakuwa
mara ya pili mfululizo, Bara kukutana na Uganda katika Nusu Fainali ya michuano
hii, kwani hata mwaka jana pia mjini Dar es Salaam, zilikutana katika hatua
hiyo, Desemba 8, Uwanja wa Taifa.
Katika
mchezo huo, wenyeji wakiwa chini ya makocha wazalendo, walichapwa mabao 3-1
ndani ya dakika 120, Stars ikitangulia kupata bao mapema tu dakika ya 18,
mfungaji Mrisho Khalfan Ngassa, lakini Nahodha wa The Cranes Andy Mwesigwa akasawazisha dakika ya 56.
Mchezo
ulipohamia katika dakika za nyongeza, Uganda walipata mabao mawili na
kuwamaliza wenyeji, wafungaji Emmanuel Okwi dakika ya 102 na Isaac Isinde dakika
ya 111 kwa penalti.
Kocha wa
Stars, Mdenmark Kim Poulsen ametahadharisha wanataka uchezeshaji wa haki kutoka
kwa refa Mohamed El Fadil wa Sudan, ambaye pia aliwachezesha katika mechi dhidi
ya Rwanda Robo Fainali.
“Vijana
wamejiandaa vizuri kabisa na wote wako katika hali nzuri ya kucheza ila
tunachoomba ni uchezeshaji wa haki kutoka kwa refa, maana tunacheza na wenyeji
ambao wana watazamaji wengi,” alisema.
Poulsen alisema
timu zote mbili ni nzuri na iwapo muamuzi atachezesha vizuri basi utakuwa ni mchuano
mkali. “Vijana wana ari na mchezo huu na tukipewa haki tutacheza vizuri kama
tulivyofanya katika michezo dhidi ya Rwanda,” alisema Poulsen.
Kuhusu hali
ya timu, Mdenmark huyo alisema hana majeruhi hata mmoja na pia aliwasifu
wachezaji wake kwa kuonyesha umoja na nidahmmu ya hali ya juu. “Hawa wanakaa
kama familia, si unawaona walivyo pamoja?” alisema Poulsen na kuongeza kuwa
hilo ni muhimu sana kwa mchezaji.
Kwa upande
wake, Kocha Msaidizi wa Stars, Sylvester Marsh amesema kama Uganda waliwafunga
Tanzania Dar es Salaam mwaka jana, basi na wao watawafunga Kampala mwaka huu.
Kocha wa
Uganda, The Cranes, Msoctland, Bobby Williamson alisema kwamba Stars ni timu
nzuri, lakini haina uwezo wa kuifunga timu yake.
“Wana
wachezaji wazuri, wenye vipaji, lakini bado timu yangu ni nzuri katika
mashindano haya, tutawafunga,”alisema.
Safu ya
ushambuliaji ya Stars leo inatarajiwa kuongozwa na Mrisho Khalfan Ngassa na
John Raphael Bocco ‘Adebayor’ ambao wanaongoza kwa mabao katika mashindano
haya, kila mmoja akiwa na mabao matano.
Uimara zaidi
wa Stars upo katika safu ya kiungo, ambako kuna watu mahiri kama Frank Domayo,
Amri Kiemba, Salum Abubakar na Mwinyi Kazimoto.
Stars pia
inajivunia safu imara ya ulinzi, chini ya Nahodha, kipa Juma Kaseja, mabeki
Erasto Nyoni, Amir Maftah, Kevin Yondan na Shomary Kapombe ambao wameruhusu bao
moja tu katika mechi nne zilizopita, tena la penalti, dhidi ya Burundi.
Bocco,
aliyeimarika zaidi kiuchezaji, mwenye nguvu, anayeenda hewani na kuambaa vema
na mpira, atasimama mbele ya mdomo wa goli la Korongo wa Kampala, wakati Ngassa
atakuwa akishambulia kutokea pembeni.
Domayo,
Kiemba na Sure Boy watakuwa wote wakikaba kwa bidii, wakati Kazimoto atakuwa
akiiendesha timu, zaidi ya kuwatengenezea nafasi za kufunga Bocco na Ngassa.
Kiemba amekuwa
akitumia mwanya wa timu kufanya mashambulizi ya kushitukiza kupanda kusaidia na
ndiyo maana aliwafunga Rwanda, jambo ambalo linatarajiwa na leo pia.
Kazimoto
mwenye mashuti makali hajafunga hata bao moja katika mechi nne zilizopita,
lakini matarajio ya wengi atatikisa nyavu kuanzia leo baada ya kuizoea zaidi
hali ya Kampala.
Uganda nao
wana ukuta sugu, ambao haujaruhusu hata bao moja hadi sasa, ikiongozwa na kipa
Hamza Muwonge, mabeki Iguma Dennis, Godfrey Walusimbi,Henry kalungi na Isaac
isinde, wakati safu ya kiungo ya kiungo inatarajiwa kuongozwa na Hassan Wasswa,
Geoffrey Kizito na Moses Oloya.
Safu ya
ushambuliaji leo bila shaka dhamana watapewa, Robert Ssentongo, Hamisi Kiiza na
Brian Umony, wakati Emmanuel Okwi anaweza kuanzia benchi tena. Mchezo wa leo
unatarajiwa kuwa mkali, Uganda wakicheza mbele ya malefu ya mashabiki wao na
Bara wakijaribu kulipa cha Dar es Salaam
mwaka jana.
Timu hizi
zimekutana mara 12 katika Challenge tangu mwaka 1975, kila timu ikishinda mechi
tano, sare mbili na Bara imefunga mabao 16, wakati imefungwa mabao 17.
Uganda; Hamza Muwonge, Iguma Dennis, Godfrey
Walusimbi, Henry Kalungi, Isaac Isinde, Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito, Moses
Oloya, Robert Ssentongo, Hamisi Kiiza na Brian Umony.
Tanzania; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir
Maftah, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Franko Domayo, Amri Kiemba, Salum
Abubakar, Mwinyi Kazimoto, John Bocco na Mrisho Ngassa.
Mungu
zibariki timu zetu, Bara na Zanziabr leo, ibariki Tanzania. Amin.
MATOKEO YA JUMLA STARS NA CRANES
TANGU 1975:
P W D L GF
GA Pts
Uganda 12 5 2 5 17 16 17
Tanzania 12 5 2 5 16 17 17
REKODI YA STARS NA CRANES CHALLENGE
TANGU 1974:
Desemba 8, 2011; Nusu Fainali, Dar es Salaam
Uganda 3–1
Tanzania (dakika 120)
Januari 9, 2009; Kundi A Uganda
Tanzania 1-2
Uganda
Desemba 11, 2001; Kundi B Rwanda
Tanzania 1-0
Uganda
Desemba 1, 1995; Kundi B Uganda
Tanzania 2-1
Uganda B
Desemba 10, 1994; Fainali Kenya
Tanzania 2-2
Uganda: (Tanzania ilishinda kwa penalti 4-3)
Desemba 10, 1992; Fainali Mwanza
Tanzania B(Kakakuona)
0-1 Uganda
Desemba 17, 1990; Nusu Fainali Zanzibar
Tanzania 1-1
Uganda (dakika 120, Uganda ilishinda penalti 6-5)
Desemba 1, 1984; Kundi A Uganda
Tanzania 1-1
Uganda
Novemba 20, 1983; Kundi A Kenya
Tanzania 1-1
Uganda
Novemba 17, 1982; Kundi A Uganda
Tanzania 0-1
Uganda
Novemba 9, 1979; Kundi A Kenya
Tanzania 5-3
Uganda
Desemba 10, 1974; Fainali Dar es Salaam
Tanzania 1-1
Uganda (Tanzania ilishinda kwa penalti 5-3)BPL WIKIENDI: NI DABI ya MANCHESTER, City v Man United!
>>DIFENSI YAMCHENGUA FERGIE!!
>>MANCINI: ‘Kubwagwa NJE ULAYA si AIBU!!’
HUKU
DABI ya JIJI la Manchester ikiwa kilingeni Jumapili ijayo Uwanjani
Etihad kati ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England Manchester City na
Vinara wa Ligi hiyo Manchester United, Sir AlexFerguson
amehimiza Wachezaji wake wa Manchester United kuwa makini na Difensi
yao inayovuja kama pakacha na mwenzake wa Manchester City, Roberto
Mancini, baada ya kuumbuka kwa kubwagwa nje ya michuano ya Ulaya na
kukosa hata kucheza EUROPA LIGI, amejipa moyo kuwa sasa mkazo wao upo
kwenye Ligi na FA Cup.
Msimu huu, Man United imesharuhusu Mabao
32 katika Mechi zote walizocheza na hizo ni nyingi mno kupita desturi
yao na Meneja wao Sir Alex Ferguson ameonya: “Inaleta wasiwasi.
Tukicheza kama tulivyocheza na Reading na City wana Wachezaji warefu
kina Balotelli na Dzeko, Mungu anajua nini kitatokea!”
++++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI WALIYOFUNGWA MAN UNITED kwa Msimu:
-2012/13: Goli 21 (Baada Mechi 15 tu)
-2011/12: 33
-2010/11: 37
-2009/10: 28
-2008/09: 24
-2007/08: 22
-2006/07: 27
-2005/06: 34
-2004/05: 26
-2003/04: 35
++++++++++++++++++++++++++++
Ingawa imeripotiwa Sentahafu wao mahiri
na Nahodha wao Nemanja Vidic yuko fiti baada ya kupona goti lake na
alitegemewa kucheza Mechi yao ya kukamilisha Ratiba ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI, kwa vile wameshafuzu, Jumatano Usiku Uwanjani Old Trafford dhidi
ya CFR Cluj, Ferguson amesema Mchezaji huyo anahitaji muda zaidi
kujijenga upya.
++++++++++++++++++++++++++++++++
DABI=Historia:
-Dabi ya kwanza kabisa ilichezwa Mwaka
1881, Novemba 2, na West Gorton (St. Marks), ndio Manchester City sasa,
walikuwa ndio Mwenyeji wa Newton Heath, sasa Manchester United, na
Newton Heath wakaibuka kidedea kwa Bao 3-0.
-Hadi sasa zimeshachezwa jumla ya Dabi
rasmi 164 na Man United ndio wanaongoza kwa kushinda 68 dhidi ya 46 za
Man City huku sare zikiwa 50.
MICHUANO |
Man City |
Sare |
Man United |
LIGI |
40 |
49 |
58 |
FA CUP |
3 |
0 |
6 |
LIGI CUP |
3 |
1 |
2 |
NGAO ya HISANI |
0 |
0 |
2 |
JUMLA |
46 |
50 |
68 |
++++++++++++++++++++++++++++++++++
Nae Roberto Mancini, baada ya jana
Jumanne Usiku kuchapwa Bao 1-0 na Borussia Dortmund huko Germany na
kujihakikishia kumaliza mkiani mwa Kundi D la UEFA CHAMPIONZ LIGI nyuma
ya Dortmund, Real Madrid na Ajax, na hivyo kukosa kusonga mbele na hata
kutupwa EUROPA LIGI, amejipa moyo kuwa pigo hilo si aibu bali litawapa
moyo kuutetea vyema Ubingwa wao wa England.
Hadi sasa kwenye Ligi, Man City wapo nafasi ya 2, Pointi 3 nyuma ya Vinara Man United.
+++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za juu:
[Kila Timu Mechi 15]
1 Man United Pointi 36
2 Man City 33
3 Chelsea 26
4 WBA 26
5 Tottenham 26
6 Everton 23
7 Swansea 23
8 West Ham 22
9 Stoke 22
10 Arsenal 21
+++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 8 Desemba 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v West Brom
Aston Villa v Stoke
Southampton v Reading
Sunderland v Chelsea
Swansea v Norwich
Wigan v QPR
Jumapili 9 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man City v Man United
[SAA 12 Jioni]
Everton v Tottenham
[SAA 1 Usiku]
West Ham v Liverpool
Jumatatu 10 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Fulham v Newcastle
Jumanne 11 Desemba 2012
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v Reading
UEFA CHAMPIONZ LIGI: NI HISTORIA, MABINGWA CHELSEA NJEEE!!!
>>CHELSEA saizi yao EUROPA LIGI!!
>>CELTIC, JUVE, GALATASARAY ZAKAMILISHA 16!!
+++++++++++++++++++++++++++++++
TIMU ZILIZOFUZU KUCHEZA RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16:
-KUNDI A: PSG, Porto
-KUNDI B: Schalke, Arsenal
-KUNDI C: Malaga, AC Milan
-KUNDI D: Dortmund, Real Madrid
-KUNDI E: Juventus, Shakhtar Donetsk
-KUNDI F: Bayern Munich, Valencia
-KUNDI G: Barcelona, Celtic
-KUNDI H: Manchester United, Galatasaray
+++++++++++++++++++++++++++++++
Waliokuwa Mabingwa wa Ulaya, Chelsea, wametupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI licha ya kuishindilia Nordsjælland
Bao 6-1 na kumaliza Mechi katika Kundi E wakiwa nafasi ya 3 baada ya
Juventus kuifunga Shakhtar Donetsk Bao 1-0 na kutwaa Nambari Wani na
huku Shakhtar wakikamata nafasi ya pili, matokeo ambayo yamewafanya
Chelsea kuwa Mabingwa wa kwanza watetezi kutolewa kwenye hatua ya
Makundi.
MATOKEO:
Jumatano Desemba 5
Shakhtar Donetsk 0 Juventus 1
Chelsea 6 Nordsjælland 1
Lille 0 Valencia 1
Bayern München 4 BATE Borisov 1
Barcelona 0 Benfica 0
Celtic 2 Spartak Moskva 1
Manchester United 0 CFR 1907 Cluj 1
Braga 1 Galatasaray 2
FAHAMU: Droo ya kupanga Ratiba ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 itafanyika Desemba 20
NDOTO YA LIONEL MESSI KUVUNJA REKODI YA GERD MULLER YA MABAO 85 KIPINDI CHA MWAKA MMOJA YATOWEKA.
Mshambuliaji
nyota wa Barcelona Lionel Messi amejikuta akitolewa nje kwa machela kutokana na
kupata maumivu makali katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Benfica.
Tito
Vilanova hakumuanzisha mshambuliaji huyo kama ilivyo kawaida yake na kumuingiza
katikati ya mchezo kipindi cha pili kwa lengo la kusukuma mashambuliaji zaidi.
Zikiwa zimesalia
dakika tano mchezo huo kumalizika wakati huo matokeo yakiwa ni sare ya bila
mabao, mshambuliaji huyo anayetazamiwa na wengi kushinda tuzo ya Ballon d'Or
favorite aliwekwa chini na kuanza kulalamikia maumivu ya mguu wake kabla ya
kutolewa nje ya dimba la Camp Nou kwa matibabu.
Maafisa wa
Barcelona muda mfupi baadaye wakatumia mtandao wa kijamii wa twitter kwa kutoa
ujumbe
"Messi
amepatwa na mchubuko katika mguu wake wa kushoto . Anatakiwa kufanyiwa vipimo
zaidi ukubwa wa jeraha lake,".
Baada ya
mshambuliaji huyo kutolewa nje hakukuwa na mabadiliko yoyote ya matokeo na
hivyo mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 0-0, matokeo ambayo yanaiondoa Benfica
mashindano na kusogezwa katika Europa League wakati ambapo Celtic ikisonga mbele
baada ya kuichapa Spartak Moscow.
Wengi walitazama
kuwa usiku wa jumatano hii utakuwa ni usiku wa kihistoria kwa Messi kuvunja
rekodi ya Gerd Muller ya kufunga magoli 85 katika kipindi cha mwaka mmoja.
WACHEZAJI WA ERITREA WALIOTOWEKA WAJITOKEZA NA KUOMBA HIFADHI YA UKIMBIZI.
WACHEZAJI 17 na kiongozi
mmoja wa timu ya taifa ya Eritrea waliokuwa wametoweka katika hoteli
yao jijini Kampala, Uganda Jumapili wamonekana. Wachezaji
hao walikutana na Waziri wan chi hiyo anayeshughulika masuala ya maafa,
Musa Echweru na kuomba hifadhi kama wakimbizi huku wenzao wengine
waliobakia ambao ni wachezaji wawili na viongozi watano wakirejea
nyumbani Jumanne. Echweru
alithibitisha kuwasiliana na wachezaji hao na kusema kuwa wamepeleka
suala suala hilo kwa mamlaka husika ili waweze kulishughulikia. Eritrea walitolewa katika mashindano ya Kombe la Cecafa Jumamosi iliyopita na timu nzima ilitakiwa kurejea nyumbani Jumanne. Hiyo
imekuwa ni tabia ya kawaida kwa wachezaji wa Eritrea kutoweka mara
baada ya mechi za mashindano ambapo mwaka 2007 katika michuano hiyo
iliyofanyika nchini Tanzania wachezaji 12 walipotea kabla ya kurudia
tukio kama hilo miaka miwili baadae katika mashindano kama hayo
yaliyofanyika nchini Kenya. Matukio
ya uvunjaji wa sheria za haki za binadamu na kukosekana kwa uhuru wa
vyombo vya habari pamoja na uhuru wa kisiasa nchini Eritrea ndio
inachangia kwa kiasi kikubwa wachezaji hao kuamua kutoweka na kushindwa
kurudi kwao huku wakiomba hifadhi ya kikimbizi katika nchi walizokwenda.
MESSI HATIHATI KUIKOSA REAL BETIS.
KLABU ya Barcelona
imesema kuwa mshambuliaji wake nyota Lionel Messi amepata majeruhi ya
goti lake la kushoto na kuna hatihati akakosekana katika wa La Liga
dhidi ya Real Betis unaotarajiwa kuchezwa Jumapili. Katika
taarifa iliyotumwa katika tovuti ya klabu hiyo imesema vipimo
alivyofanyiwa nyota huyo vimethibitisha kuwa amepata mchubuko katika
mfupa wa goti lake na kupona kwake kutakuwa taratibu hivyo kuwepo
uwezekano mkubwa wa kukosa mchezo huo. Mchezaji
huyo bora wa dunia aliondolewa katika machela katika mwishoni mwa
mchezo wa kundi G wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Benfica baada ya
kugongana na golikipa wa timu hiyo wakati akijaribu kufunga. Pamoja
na sare ya bila kufungana iliyopata Barcelona katika mchezo huo
walikuwa tayari wamefuzu katika hatua ya timu 16 bora wakiwa vinara wa
kundi lao huku wapinzani wao Benfica wakishindwa kusonga mbele na kupata
nafasi katika Europa League. Messi
amebakisha bao moja ili kufikia rekodi ya mabao 85 aliyoweka Gerd
Muller katika kipindi cha mwaka mmoja, hiiyo ikiwa mwaka 1972.
CAF REVEALS TOP THREE.
SHIRIKISHO la Soka
barani Afrika-CAF limetaja majina matatu ya mwisho ya wachezaji
watakaogombea tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2012. Nyota
wa Ivory Coast Yaya Toure ambaye anashikilia tuzo ya mwaka jana na
Didier Drogba ambaye ameshinda tuzo hiyo mwaka 2006 na 2009 watakuwa
wakipambana na kiungo wa kimataifa wa Cameroon na klabu ya Barcelona
Alexander Song. Kwa
upande wa orodha ya mwisho ya wachezaji wanaocheza ndani ya bara la
Afrika wachezaji wa Zambia Rainford Kalaba na Stoppila Sunzu ambao wote
wanacheza katika klabu ya TP Mazembe ya DRC na Mohamed Abou Trika wa
Misri na klabu ya Al Ahly ndio watakaogombea tuzo hiyo. Mshindi katika tuzo hizo atatangazwa katika sherehe zitakazofanyika jijini Accra, Ghana Desemba 20 mwaka huu.
SINA MUDA WA KUPUMZIKA - MOURINHO.
MENEJA wa klabu ya Real
Madrid, Jose Mourinho amesema kuwa hatakuwa na muda wa kupumzika wakati
akiamua kuondoka katika klabu hiyo. Kumekuwa
na tetesi kuwa Mourinho ambaye ni raia wa Ureno ataondoka katika klabu
hiyo mwishoni mwa msimu huku taarifa hizo zikielekeza kuwa kocha huyo
atakwenda katika klabu za Manchester City au Paris Saint-Germain. Lakini
kocha huyo wa zamani wa klabu za Porto, Chelsea na Inter Milan amesema
kuwa kama ataondoka Santiago Bernabeu anatarajia haraka kutafuta timu
nyingine na sio kupumzika. Mourinho amesema hatachukua likizo ya mwaka mzima kwa akiondoka Hispania ataelekea kokote kule kuendelea kufundisha. Madrid
kwasasa inashika nafasi ya tatu katika La Liga wakiwa nyuma ya vinara
wa ligi hiyo Barcelona kwa alama 11 huku wakiwa wamepitwa lama tano na
mahasimu wao wa jiji Atletico Madrid ambao wanashika nafasi ya pili.
SHEHATA ATUPIWA VIRAGO BAADA YA KUFUNDISHA MIEZI MWILI NCHINI QATAR.
EUROPA LIGI: Alhamisi Timu 9 kuwania nafasi 5 zilizobaki!
>>19 tayari zishatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Bado 5!
>>WAMO Liverpool na Tottenham kuwania nafasi!
Klabu
19 tayari zimeshatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA LIGI
lakini bado zipo nafasi 5 zinazogombewa na Timu 9 ambazo zitapatikana
Alhamisi Desemba 6 katika Mechi za mwisho za Makundi, na katika hizo 9
zilizo kwenye patashika ni Liverpool na Tottenham lakini wenzao
Newcastle wao tayari wameshavuka.
Timu hizi 24 toka EUROPA LIGI
zitajumuika na Timu 8 wamalizaji wa nafasi ya 3 katika Makundi ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI ili kufanya jumla ya Timu 32 zitakazoingia Droo ya
kupanga Raundi ya Mtoano itayochezwa nyumbani na ugenini.
Droo ya kupanga Raundi ya Mtoano ya Timu 32 itafanyika Desemba 20.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
KLABU 19 ZILIZOFUZU:
Olympique Lyonnais
FC Rubin Kazan
FC Internazionale Milano
Hannover 96
Bayer 04 Leverkusen
FC Metalist Kharkiv
FC Anji Makhachkala
Fenerbahçe SK
VfL Borussia Mönchengladbach
AC Sparta Praha
S.S. Lazio
Club Atlético de Madrid
FC Viktoria Plzeň
Levante UD
KRC Genk
FC Dnipro Dnipropetrovsk
SSC Napoli
Newcastle United FC
FC Girondins de Bordeaux
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Mabingwa watetezi Atlético de Madrid wao
wamo katika Timu 19 ambazo tayari zimefuzu pamoja na Timu nyingine ya
England, Newcastle.
Timu 9 zinazosaka nafasi 5 ni Liverpool
FC au BSC Young Boys, toka Kundi A; FC Steaua Bucureşti au VfB Stuttgart
au FC København toka Kundi E; FC Basel 1893 au Videoton FC toka Kundi G
na Tottenham Hotspur FC au Panathinaikos FC kutoka Kundi J.
MAHESABU ya LIVERPOOL na TOTTENHAM KUFUZU:
KUNDI A:
Mechi:
-BSC Young Boys (Pointi 7) v FC Anji Makhachkala (Pointi 10)
-Udinese Calcio (Pointi 4) v Liverpool FC (Pointi 7)
Mahesabu:
-Anji wamefuzu hata kama watakutwa kwa
Pointi na Liverpool na Young Boys kwa sababu ya rekodi yao bora ya uso
kwa uso na wapinzani wao.
-Liverpool wakishinda wataipiku Young
Boys kwa vile wana rekodi bora kupita wao. Sare itawasaidia ikiwa tu
Young Boys hawashindi. Liverpool wakifungwa tu, wako nje.
-Udinese wako nje.
KUNDI J:
Mechi:
-NK Maribor (Pointi 4s) v S.S. Lazio (Pointi 9)
-Tottenham Hotspur FC (Pointi 7) v Panathinaikos FC (Pointi 5)
Mahesabu:
-Lazio wameshafuzu na watamaliza Nambari wani ikiwaTottenham hawashindi.
-Ikiwa Lazio na Tottenham watamaliza
wamefungana Pointi, Mshindi ataamuliwa kwa tofauti ya Magoli au
wakifungana kwa hilo basi Magoli ya kufunga na hilo likiwa sawa, Mshindi
ataamuliwa kwa yupi yuko juu katika Listi ya Ubora ya UEFA.
-Tottenham watafuzu wakitoka sare au ushindi.
-Panathinaikos watafuzu wakishinda.
-Maribor tayari wako nje.
RATIBA:
Alhamisi Desemba 6
BSC Young Boys v FC Anzhi Makhachkala
Udinese Calcio v Liverpool FC
Hapoel TelvAviv FC v A. Académica de Coimbra
FC Viktoria Plzen v Club Atlético de Madrid
AEL Limassol FC v Olympique de Marseille
Fenerbahçe SK v VfL Borussia Mönchengladbach
CS Marítimo v Club Brugge KV
FC Girondins de Bordeaux v Newcastle United FC
VfB Stuttgart v Molde FK
FC København v FC Steaua Bucuresti
FC Dnipro Dnipropetrovsk v AIK
SSC Napoli v PSV Eindhoven
KRC Genk v FC Basel 1893
Sporting Clube de Portugal v Videoton FC
FC Internazionale Milano v Neftçi PFK
FK Partizan v FC Rubin Kazan
Olympique Lyonnais v Hapoel Kiryat Shmona FC
Athletic Club v AC Sparta Praha
NK Maribor v S.S. Lazio
Tottenham Hotspur FC v Panathinaikos FC
SK Rapid Wien v FC Metalist Kharkiv
Bayer 04 Leverkusen v Rosenborg BK
Levante UD v Hannover 96
FC Twente v Helsingborgs IF
No comments:
Post a Comment