Thursday, December 6, 2012

CHELSEA VS FC NORDSJAELLAND JANA 6-1 | All Goals and Full Highlights [05/...



 

  RHINO RANGERS WAWEKA MIKAKATI  YA RAUNDI YA PILI YA LIGI DARAJA  LA KWANZA FDL ILI WAWEZE KUFUZU KUCHEZA LIGI KUU VPL

 

 Timu ya RHINO RANGERS ya mkoani tabora leo ilikuwa na kikao kikali  na wadau /wapenzi wa mpira wa miguu mkoani tabora cha kujadili kuhusu timu ya RHINO katika michuano ya ligi daraja la kwanza FDL .

 

Wadau hao walijadili mambo mengi yakiwemo

1.Ushirikishwaji wa wadau na wananchi katika mkoa wa tabora .katika maada hii ya kwanza wamejadili mambo mengi yakiwemo,

==kutengeneza kadi za uanachama

==kushirikiana na vyombo vya habari ili waweze kusonga mbele.

==kuunda TASK FORCE inayosema saidia rhino ishinde

==kuondoa utofauti /malumbano mengi baina ya timu mbili RHINO na POLISI

==Kuwashilikisha wadau wa wilayani.timu iwe inafanya TRIAL ya kutembelea wilaya zote za mkoa wa tabora ili wadau wenye uchu na maendeleo ya mpira wa miguu wa mkoa wa tabora wa wilayani waone umuhimu na kuichangia michango mbali mbali

 

2.Kuunda kamati ya saidia rhino ishinde.katika maada hii imewateua watu sita watakaoongoza hiyo task force ya saidia rhino ishinde nao ni,

1.NICO MWAIBALE

2.FATTY  DEWJ REMTULA

3.MUSSA NTIMIZI

4.MOSHI NKONKOTA

5.MASJ MASAWE

6.KANALI SIMON HONGOA

 

3.Uwezeshaji wa timu.Katika raundi ya pili ya ligi daraja la kwanza rhino rangers inahitaji shilingi mil.51,240,000 ili iweze kufanya vizuri katika mashindano hayo,pia inahitaji,viatu vya wachezaji,soksi,traksuti,mipira,grovsi na baadhi ya vifaa vya mazoezi na kamati ya saidia rhino ishinde imeahidi kufanya kazi vizuri,pia klabu ya rhino rangers inahitaji kusajili wachezaji watatu ambao wataleta nguvu katika kikosi chao ,

wanahitaji beki mmoja na washambuliaji wawili ili waweze kufanya vizuri na waweze  kupanda daraja la kwanza FDL msimu huu.

 4.Mkakati wa ligi daraja la kwanza mzunguko wa pili

5.mengineyo

UEFA CHAMPIONZ LIGI: Man United & Arsenal, nani Wapinzani wao MTOANO??

UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZ>>MAN UNITED kuivaa Celtic, Porto, AC Milan, Real, Valencia au Shakhtar
>>ARSENAL na PSG, Malaga, Barca, Dortmund, Bayern au Juve??
>>DROO RAUNDI ya MTOANO TIMU 16 kupangwa Desemba 20!
>>MECHI KUCHEZWA Februari & Machi 2013!!
Wakati Chelsea wanaweka historia ya kuwa Mabingwa wa kwanza Watetezi kushindwa kufikia hatua ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na kutupwa kucheza EUROPA LIGI na wenzao Manchester City, Mabingwa wa England, wakiyaaga kabisa Mashindano ya Ulaya Msimu huu, Manchester United na Arsenal ndio pekee toka England zipo Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Timu nyingine toka Visiwa vya Uingereza ambayo ipo Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ni Celtic ya Scotland.
+++++++++++++++++++
TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA Raundi ya Mtoano ya Timu 16:
WASHINDI wa MAKUNDI:
Paris St Germain
Schalke 04
Malaga
Borussia Dortmund
Juventus
Bayern Munich
Barcelona
Manchester United
WASHINDI wa PILI wa MAKUNDI:
Porto
Arsenal
AC Milan
Real Madrid
Valencia
Shakhtar Donetsk
Galatasaray
Celtic
+++++++++++++++++++
Kwa mujibu wa Kanuni za UEFA za Droo ya upangaji Ratiba ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16, zile Timu ambazo zimekuwa Washindi wa Makundi watawekwa Kapu Namba 1 na wale waliomaliza Nafasi ya Pili kwenye Makundi wapo Kapu Namba 2.
Droo itafanywa kwa kutoa Jina moja toka Kapu Namba 2 na kufuatia Jina jingine toka Kapu Namba 1 na Timu hizo ndizo zitakazokutana isipokuwa Timu zinazotoka Nchi moja na zile zilizokuwa Kundi moja haziwezi kupambanishwa.
Pia, Mechi za kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitachezwa nyumbani kwa Timu itakayotoka Kapu Namba 2, Timu zilizomaliza Nafasi ya Pili, na marudiano ni nyumbani kwa Washindi wa Makundi.
Kwa mujibu wa Kanuni hizi za UEFA, Wapinzani wa Manchester United na Arsenal wanaweza kuwa kama ifuatavyo:
-MAN UNITED anaweza kucheza na mmoja kati ya Celtic, Porto, AC Milan, Real Madrid, Valencia au Shakhtar Donetsk.
-ARSENAL mpinzani wake ni mmoja kati ya: PSG, Malaga, Barcelona, Borussia Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitachezwa Februari 12 na 20, 2013 na marudiao ni Machi 5 na 13, 2013.
TOKA UEFA CHAMPIONZ LIGI kwenda EUROPA LIGI:
[Timu zilizomaliza Nafasi ya 3 kwenye Makundi]
-KUNDI A: Dynamo Kiev
-KUNDI B: Olympiacos
-KUNDI C: Zenit St Petersburg
-KUNDI D: Ajax Amsterdam
-KUNDI E: Chelsea
-KUNDI F: BATE Borisov
-KUNDI G: Benfica
-KUNDI H: CFR Cluj-Napoca
 

FUPI za LEO: Obi Lupango, Messi anusurika & Fergie atoa Medali kwa Majeshi!!

>>REKODI ya MULLER: Messi hachezi Jumapili, ila zipo Mechi 3 kuvunja REKODI!!
CLATTENBURG_na_CHELSEALEO Mashabiki wa Barcelona wamepata habari njema baada ya kuthibitishwa kuwa Supastaa wao, Lionel Messi, ambae jana alitolewa kwa machela Uwanjani Nou Camp wakati wa Mechi na Benfica, hakuumia sana kama ilivyoogopwa lakini Mashabiki wa Chelsea wamepata pigo baada ya FA kumshushia Kifungo cha Mechi 3 na Faini Pauni 66,000 Kiungo wao John Mikel Obi kwa kosa la kumtishia Refa Mark Clattenburg na huko Jijini Manchester, Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amepewa heshima kubwa ya kupokea na kutoa Medali kwa Wanajeshi wa Uingereza ambao wamemaliza utumishi wao toka uwanja wa vita wa Afghanistan.
John Mikel Obi
Kiungo wa Chelsea, John Mikel Obi, amefungiwa Mechi 3 na kupigwa Faini Pauni 66,000 kwa kosa la kumtishia Refa Mark Clattenburg ambalo alilikubali na ambalo lilitokea mara baada ya Mechi iliyochezwa Uwanja wa Stamford Bridge hapo Oktoba 28 kati ya Chelsea na Manchester United na Chelsea kunyukwa 3-2.
Ingawa Obi aliomba kusikilizwa binafsi na Jopo la FA lilioendesha Kesi dhidi yake huku akijitetea aliamini kuwa amekashifiwa Kibaguzi, Jopo hilo lilisema anayo hatia lakini halikumpa adhabu kali zaidi kwa vile tu wamekubali utetezi wake kuwa aliamini kabaguliwa.
Awali Chelsea iliwasilisha malalamiko yao kwa FA kwamba Refa Mark Clattenburg alimkashifu Kibaguzi John Mikel Obi wakati wa Mechi hiyo lakini FA ilitupilia mbali malamiko hayo na kumfungulia Kesi Obi kwa kuvamia Chumba cha Marefa mara baada ya Mechi na kumtishia Refa.
Lionel Messi hakuumia sana!MESSI_ASHANGILIA_GOLI
Barcelona imethibitisha kuwa Supastaa wao Lionel Messi amepata mchubuko tu baada ya kutolewa na machela wakati wa Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI waliyotoka sare na Benfica Uwanjani Nou Camp hapo jana.
Messi, alieingizwa Kipindi cha Pili cha Mechi hiyo, alitolewa baada ya Dakika 30 za kuwa Uwanjani alipogongana na Kipa wa Benfica na kuumia goti lake la kushoto na kulikuwa na wasiwasi mkubwa kuwa ameumia sana.
Messi, ambae ameshafunga Mabao 84 kwa Mwaka 2012, anasaka kuivunja rekodi ya Mjerumani Gerd Muller aliyoiweka Mwaka 1972 kwa kufunga Goli 85 akichezea Bayern Munich na West Germany.
Ingawa Messi hatarajiwi kucheza Mechi ya Jumapili ya La Liga ugenini na Real Betis, lakini Barcelona bado wanazo Mechi za La Liga dhidi ya Atletico Madrid na Real Valladolid, na pia ile ya Copa del Rey dhidi ya Cordoba katika Mwezi huu Desemba na hiyo ni fursa kubwa kwake kuvunja rekodi hiyo.
FERGIE_na_MAJESHISir Alex Ferguson
Ferguson leo aliyasahau matayarisho ya Timu yake Manchester United kwa ajili ya Dabi ya Manchester ya Jumapili hii dhidi ya Mahasimu wao Manchester City na kwenda kuwa Mgeni wa Heshima kwa kukabidhi Medali kwa Wanajeshi wa Uingereza ambao wamemaliza utumishi wao toka uwanja wa vita wa Afghanistan.
Wanajeshi hao ambao walizunguka katikati ya Mji kwa Paredi walimalizia kwa ukaguzi uliofanywa na Sir Alex Ferguson na kisha kuwatunukia Medali kila mmoja wao.
+++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND=RATIBA:
Jumamosi 8 Desemba 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v West Brom
Aston Villa v Stoke
Southampton v Reading
Sunderland v Chelsea
Swansea v Norwich
Wigan v QPR
Jumapili 9 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man City v Man United
[SAA 12 Jioni]
Everton v Tottenham
[SAA 1 Usiku]
West Ham v Liverpool
Jumatatu 10 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Fulham v Newcastle
Jumanne 11 Desemba 2012
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v Reading

 

MAMBO HAYA YATAISHA LINI HASA KATIKA USAJIRI RAGE KAGOMA KUMUACHIA NGASA


Mwenyekiti wa mabingwa wa soka nchini Simba ya jijini Dar es Salaam Alhaji Ismail Aden Rage amesema klabu ya Azam inayoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania Bara itakuwa inajifurahisha tu endapo ni kweli itakuwa imekamilisha taratibu za kumuuza mshambuliaji Mrisho Ngasa kuelekea katika klabu ya El Merreck ya Sudani.
Kauli ya Rage inafuatia kuwepo na taarifa iliyochapishwa hii leo katika Tovuti ya klabu hiyo kuwa klabu hiyo imekamilisha taratibu za kumuuza Ngasa kuelekea El Merreikh ya Sudani.

Taarifa hiyo imesomeka kwa kichwa cha habari "Ngasa atua Ell Mereikh kwa $75,000"

Kwa mujibu wa maelezo ya kina ya tovuti ya Azam ni kwamba
Azam FC leo imemuuza mchezaji wake Mrisho Halfan Ngasa kwa klabu ya El Mereikh katika majadiliano yaliyochukua takriban saa moja kwenye makao makuu ya klabu ya Azam FC na kuhudhuriwa na viongozi wa pande zote mbili.

El-Mereik wameshazungumza na mchezaji na kukubaliana maslahi yake binafsi ambapo Mrisho Ngasa atalazimika kusafiri hadi mjini Khartoom Sudan mara baada ya kuisha mashindano ya CECAFA Challenge Cup ili kuona mazingira ya klabu, kufanya vipimo vya Afya na kuangalia makazi yake binafsi.

Kuuzwa kwa Mrisho Ngasa nchini Sudan kunaifanya klabu ya Azam FC kupata kiasi cha zaidi ya Dola 50,000 pesa ambayo Azam FC waliiweka kama kima cha chini cha kumuuza Mrisho Ngasa.
Wakati Azam FC ikimtoa Ngasa iliweka kiasi hicho cha dola 50,000 kwa timu itakayomtaka lakini kutokana na kukosekana na mnunuzi huku Simba ikitoa ofa ya shilingi milioni 25, Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo ili akitokea mteja mwenye kufikia dau hilo waweze kumuuza.

Pia taarifa hiyo imeongeza kwa maneno kuwa,
"Mengi yalisemwa juu ya biashara ya mkopo kati ya Azam FC na Simba lakini msimamo wa Azam FC uliowekwa kwenye tovuti hii leo umethibitika baada ya El-Mereikh kufikia dau la kumnunua Mrisho Ngasa".

"Mrisho Ngasa, mchezaji mwenye kipaji cha hali ya Juu cha kusakata kabumbu anakwenda nchini Sudan kwenye kikosi chenye mafanikio zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati baada ya TP Mazembe".
.
Akiongea na Rockersports Mwenyekiti wa Simba Alhaji Rage amesema watanzania wanapaswa kuwa waangalifu na taarifa za mitandaoni kwani zinaweza kupotosha mambo.

Rage amesema mshambuliaji huyo alikopeshwa Simba kwa maandishi ambapo pia Azam ilipewa shilingi milioni 25 kwa makubaliano pia Simba kumlipa mshahara na gharama nyingine kama nyumba na gari.

Amesema ni kweli Simba hairuhusiwi kumuuza kwenda klabu nyingine hadi muda wake wa mkopo utakapo malizika Simba.

Rage amewataka Azam ndani ya Siku saba kuthibitisha tuhuma za rushwa kwa viongozi wa Simba ambapo Azam iliituhumu Simba kutoa rushwa wachezaji wao ili kupanga matokeo katika mchezo uliozikutanisha timu hizo katika ligi kuu.

 

TUPENI FEDHA ZETU NA CHA JUU YAISHE, SIMBA WAWAAMBIA AZAM

Hans Poppe

SIMBA SC imesema haitaki ugomvi wala malumbano na Azam FC, bali wanataka warudishwe fedha zao zote walizotoa kumsaini mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa, Sh. Milioni 55 pamoja na faida juu.
Azam FC jana imemuuza Mrisho Khalfan Ngassa kwa dola za Kimarekani 75,000 (Sh. Milioni 120) kwenda El Merreikh ya Sudan ambako amesaini mkataba wa miaka miwili, utakaomuwezesha kulipwa mshahara wa dola za Kimarekani 4,000 (Sh Milioni 6,) kwa mwezi huku naye akilipwa dola 50,000 (Sh. Milioni 75) za kusaini.
Akizungumza  kwa  njia ya simu jana kutoka Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba wao walimsajili mchezaji huyo kwa taratibu, ila wanashangaa sasa Azam wanataka kufanya mambo kinyume cha utaratibu.
“Sisi tuna mkataba na huyu mchezaji, ambao tulisaini na wao Azam, ambao ilikuwa kama kuununua mkataba wake wa kule Azam, baada ya wao wenyewe kushindwana na huyo mchezaji. Tuliwapa Sh. Milioni 25 na baadaye tukaongeza naye mchezaji mkataba wa mwaka mmoja, tukampa Sh. Milioni 30,”alisema Hans Poppe. 
Kapteni huyo Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), alisema kwa kuwa hawataki malumbano na Azam, wanaomba warejeshewe fedha zao na faida kidogo, kwani mchezaji huyo amenunuliwa akiwa anachezea Simba SC.
Awali, Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu Ngassa wenye thamani ya dola 100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said Bakhresa akakataa akisema utambana mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu nyingine.
Sasa, Ngassa baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwishoni mwa wiki hii, atakwenda Sudan kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na klabu hiyo, ambayo ni jambo la kawaida kucheza hatua ya makundi ya michuano ya klabu Afrika.
Azam walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu baada ya kukerwa na kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alifanya hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni 30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 akipewa gari.

NGASSA: SIMBA PANDENI DAU NIBAKI MSIMBAZI

Mrisho Ngassa
MRISHO Khalfan Ngassa amesema kama Simba wanampenda sana, wapande dau walilotoa El Merreikh ili aghairi kwenda Sudan.
Akizungumza hapa, Ngassa alisema kwamba yeye kama mchezaji anaangalia maslahi na kwa mshahara mzuri pamoja na dau nono la usajili alilopewa Matajiri wa Sudan amelainika na kukubali kujiunga nayo. 
Wakati Azam FC imemuuza Ngassa kwa dola za Kimarekani 75,000 kwenda El Merreikh ambako amesaini mkataba wa miaka miwili, kiungo huyo mshambuliaji amepewa dau la kusaini mkataba wa miaka miwili, dola 50,000 na atakuwa analipwa mshahara wa dola 4,000 kwa mwezi.
Awali, Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu Ngassa wenye thamani ya dola 100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said Bakhresa akakataa akisema utambana mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu nyingine.
Sasa Ngassa baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwishoni mwa wiki hii, atakwenda Sudan kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na klabu hiyo, ambayo ni jambo la kawaida kucheza hatua ya makundi ya michuano ya klabu Afrika.
Azam FC imesema imeweka mbele maslahi ya mchezaji na taifa kwa ujumla katika maamuzi ya kumuuza Sudan, kutoka Simba alikokuwa akicheza kwa mkopo. “Hii timu (Merreikh) kila mwaka inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, maana yake huyu mchezaji atakwenda kupata maendeleo na kuja kuisaidia zaidi Tanzania katika mashindano ya kimataifa,”alisema kiongozi mmoja wa Azam. 
Alipoulizwa kuhusu Simba SC aliyokuwa anaichezea klabu hiyo, kiongozi huyo alisema wao walimtoa kwa mkopo Ngassa kwenda kwa Wekundu wa Msimbazi hadi Mei 31, mwakani na mkataba wao ndio unasema hivyo.
“Sisi tuliwapa Simba huyu mchezaji kwa mkopo hadi Mei 31 na wakatupa Sh. Milioni 25, ila tuko tayari kuwarudishia fedha zao walizota, lakini huyu mchezaji ni mali yetu  na hata TFF wa natambua hilo, na tumekwishamuuza Merreikh,”alisema.
Alipoulizwa kuhusu Simba kusaini mkataba mpya na Ngassa, alisema; “We uliona wapi dunia nzima timu inapewa mchezaji kwa mkopo halafu inamsainisha mkataba? Simba lazima ifike wakati waache kurudia makosa, haya ndio mambo ya Mbuyu Twite sasa,”alisema kiongozi huyo wa Azam.
Azam walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu baada ya kukerwa na kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alifanya hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni 30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 akipewa gari.
Ngassa anang’ara katika Challenge ya mwaka huu mjini hapa, hadi sasa akiwa amefunga mabao matano sawa na John Bocco wa Azam na wafungana kileleni.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
John Bocco                   Tanzania  5
Mrisho Ngassa              Tanzania  5
Brian Umony                 Uganda    3
Suleiman Ndikumana    Burundi    3 (1 penalti)
Chris Nduwarugira        Burundi    3
Geoffrey Kizito              Uganda     2
Robert Ssentongo         Uganda    2
Khamis Mcha                Zanzibar   2
David Ochieng              Kenya       2
Clifton Miheso               Kenya       2
Dadi Birori                     Rwanda    2

SELEMBE AWAPA MALARIA + WAKENYA, TAZAMA REKODI YA HARAMBEE NA HEROES TANGU 1977

Kikosi cha Zanzibar, Selembe wa kwanza kushoto walioinama,
KIUNGO wa Zanzibar, Suleiman Kassim ‘Selembe‘ ndiye mchezaji ambaye anawatia hofu mno Wakenya kuelekea mchezo wa leo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini hapa.
Mashabiki wa soka wa Kenya waliopo hapa na baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka nchini humo, wamekuwa wakimzungumzia Selembe kama mchezaji hatari na aliyebeba hatima yao leo.  
“Selembe, yule mchezaji yupo kama Fellaini (Marouane) ni hatari sana yule, kwa kweli amebeba hatima yetu, tukiweza kumbana yule, Zanzibar wala hawafurukuti,”alisema mmoja wa mashabiki wa Kenya juzi mjini hapa, akimfananisha kiungo huyo na kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye asili ya Morocco, anayechezea Everton ya England.
Kenya na Zanzibar zinamenyana katika Nusu Fainali ya kwanza kwenye Uwanja wa Mandela leo, mchezo ambao utafuatiwa na mechi nyingine kati ya Uganda na Tanzania Bara.
Kenya wanaonekana kuihofia mno Zanzibar kiasi cha kuthubutu kuwarejesha kambini wachezaji wake wawili iliyowarudisha nyumbani kwa utovu wa nidhamu, Paul Were na Kevin Omondi.
Baada ya kuifunga 1-0 Sudan Kusini katika mchezo wa pili wa Kundi A, wachezaji hao walikwenda kujirusha kwenye klabu ya usiku na kurejea kambini na wanawake, jambo ambalo lilifanya asubuhi yake wapandishwe ndege wote kurejea Nairobi, lakini kutokana na mchecheto wa mechi ya kesho, wamerejeshwa.
Kocha wa Harambee Stars, James Nandwa aliliomba Shirikisho la Soka Kenya (FKF) liliwarejeshe wachezaji hao kwa ajili ya Nusu Fainali.
Kocha wa Fisa FC, Charles ‘Korea’ Omondi, ambaye amekuwa akifanya mazoezi na wachezaji hao tangu warejeshwe nyumbani, amethibitisha wamebadilika kinidhamu na wako vizuri kimchezo.
Were na Omondi wapo kwa mkopo AFC Leopards na Gor Mahia kutoka timu inayoshiriki Ligi ya Jimbo la Nairobi, Fisa FC.
Mara ya kwanza na ya mwisho timu hizi kukutana katika hatua ya mtoano ilikuwa ni mwaka 1979 nchini Kenya, katika Nusu Fainali na wenyeji walishinda 2-0 Novemba 14 Uwanja wa Nyayo, Nairobi na mara zote zimekuwa zikikutana katika hatua ya makundi.
Na mara ya mwisho kabisa kukutana katika mashindano haya timu hizi ilikuwa ni mwaka 1996 nchini Sudan na Kenya ilishinda 1-0.
Kwa ujumla, timu hizi zimekutana mara 11 tangu kuanzishwa rasmi kwa michuano ya Challenge mwaka 1974 na Kenya imeshinda mechi saba, sare tatu na imefungwa moja. Kenya imeifunga Zanzibar jumla ya mabao 17, wakati yenyewe imefungwa saba.
                 
REKODI YA KENYA NA ZANZIBAR CHALLENGE
                   P    W  D   L    GF GA Pts
Kenya         11   7    3    1    17 7    24
Zanzibar     11   1    3    7    7   17   6
REKODI YA KENYA NA ZANZIBAR TANGU 1977:
Novemba 24, 1996; Sudan Kundi B
Kenya 1-0 Zanzibar
Novemba 27,  1995; Uganda Kundi A
Kenya 2-0 Zanzibar
Novemba 30, 1991; Kundi B Uganda
Kenya 3-2 Zanzibar
Desemba 6, 1989; Kundi B Kenya 
Zanzibar 0-0 Kenya B
Desemba 14, 1987; Kundi A Ethiopia
Kenya 0-0 Zanzibar
Desemba 6, 1984; Kundi B Uganda
Kenya 1-0 Zanzibar
Novemba 21, 1982; Kundi B Uganda
Kenya 2-2 Zanzibar
Novemba 17, 1981; Kundi A Tanzania
Kenya 2-1 Zanzibar
Novemba 22, 1980; Kundi B Sudan
Kenya 1-2 Zanzibar
Novemba 14, 1979; Nusu Fainali Kenya  
Kenya 2-0 Zanzibar
Desemba 2, 1977; Kundi A Somalia
Kenya 3-0 Zanzibar

STARS NA UGANDA PATACHIMBIKA LEO NAMBOOLE, KIKOSI CHA LEO NA REKODI YA MECHI ZOTE ZILIZOPITA BAINA YA TIMU HIZO


Kikosi cha Stars leo; Kutoka kulia waliosimama John Bocco, Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Kevin yondan, Amri Kiemba na Mwinyi Kazimoto. Walioinama kutoka kushoto Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Shomary Kapombe, Salum Abubakar na Amir Maftah
TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa kumenyana na wenyeji, Uganda, The Cranes katika Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kuanzia saa 12:00 jioni.
Mchezo huo, utatanguliwa na mechi nyingine ya hatua hiyo kati ya Zanzibar na Kenya, ambayo, itaanza saa 10:00 jioni.     
Hii inakuwa mara ya pili mfululizo, Bara kukutana na Uganda katika Nusu Fainali ya michuano hii, kwani hata mwaka jana pia mjini Dar es Salaam, zilikutana katika hatua hiyo, Desemba 8, Uwanja wa Taifa.
Katika mchezo huo, wenyeji wakiwa chini ya makocha wazalendo, walichapwa mabao 3-1 ndani ya dakika 120, Stars ikitangulia kupata bao mapema tu dakika ya 18, mfungaji Mrisho Khalfan Ngassa, lakini Nahodha wa The Cranes  Andy Mwesigwa akasawazisha dakika ya 56.
Mchezo ulipohamia katika dakika za nyongeza, Uganda walipata mabao mawili na kuwamaliza wenyeji, wafungaji Emmanuel Okwi dakika ya 102 na Isaac Isinde dakika ya  111 kwa penalti.
Kocha wa Stars, Mdenmark Kim Poulsen ametahadharisha wanataka uchezeshaji wa haki kutoka kwa refa Mohamed El Fadil wa Sudan, ambaye pia aliwachezesha katika mechi dhidi ya Rwanda Robo Fainali.
“Vijana wamejiandaa vizuri kabisa na wote wako katika hali nzuri ya kucheza ila tunachoomba ni uchezeshaji wa haki kutoka kwa refa, maana tunacheza na wenyeji ambao wana watazamaji wengi,” alisema.
Poulsen alisema timu zote mbili ni nzuri na iwapo muamuzi atachezesha vizuri basi utakuwa ni mchuano mkali. “Vijana wana ari na mchezo huu na tukipewa haki tutacheza vizuri kama tulivyofanya katika michezo dhidi ya Rwanda,” alisema Poulsen.
Kuhusu hali ya timu, Mdenmark huyo alisema hana majeruhi hata mmoja na pia aliwasifu wachezaji wake kwa kuonyesha umoja na nidahmmu ya hali ya juu. “Hawa wanakaa kama familia, si unawaona walivyo pamoja?” alisema Poulsen na kuongeza kuwa hilo ni muhimu sana kwa mchezaji.
Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Stars, Sylvester Marsh amesema kama Uganda waliwafunga Tanzania Dar es Salaam mwaka jana, basi na wao watawafunga Kampala mwaka huu.
Kocha wa Uganda, The Cranes, Msoctland, Bobby Williamson alisema kwamba Stars ni timu nzuri, lakini haina uwezo wa kuifunga timu yake.
“Wana wachezaji wazuri, wenye vipaji, lakini bado timu yangu ni nzuri katika mashindano haya, tutawafunga,”alisema.
Safu ya ushambuliaji ya Stars leo inatarajiwa kuongozwa na Mrisho Khalfan Ngassa na John Raphael Bocco ‘Adebayor’ ambao wanaongoza kwa mabao katika mashindano haya, kila mmoja akiwa na mabao matano.
Uimara zaidi wa Stars upo katika safu ya kiungo, ambako kuna watu mahiri kama Frank Domayo, Amri Kiemba, Salum Abubakar na Mwinyi Kazimoto.
Stars pia inajivunia safu imara ya ulinzi, chini ya Nahodha, kipa Juma Kaseja, mabeki Erasto Nyoni, Amir Maftah, Kevin Yondan na Shomary Kapombe ambao wameruhusu bao moja tu katika mechi nne zilizopita, tena la penalti, dhidi ya Burundi.
Bocco, aliyeimarika zaidi kiuchezaji, mwenye nguvu, anayeenda hewani na kuambaa vema na mpira, atasimama mbele ya mdomo wa goli la Korongo wa Kampala, wakati Ngassa atakuwa akishambulia kutokea pembeni.
Domayo, Kiemba na Sure Boy watakuwa wote wakikaba kwa bidii, wakati Kazimoto atakuwa akiiendesha timu, zaidi ya kuwatengenezea nafasi za kufunga Bocco na Ngassa.
Kiemba amekuwa akitumia mwanya wa timu kufanya mashambulizi ya kushitukiza kupanda kusaidia na ndiyo maana aliwafunga Rwanda, jambo ambalo linatarajiwa na leo pia.
Kazimoto mwenye mashuti makali hajafunga hata bao moja katika mechi nne zilizopita, lakini matarajio ya wengi atatikisa nyavu kuanzia leo baada ya kuizoea zaidi hali ya Kampala.
Uganda nao wana ukuta sugu, ambao haujaruhusu hata bao moja hadi sasa, ikiongozwa na kipa Hamza Muwonge, mabeki Iguma Dennis, Godfrey Walusimbi,Henry kalungi na Isaac isinde, wakati safu ya kiungo ya kiungo inatarajiwa kuongozwa na Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito na Moses Oloya.
Safu ya ushambuliaji leo bila shaka dhamana watapewa, Robert Ssentongo, Hamisi Kiiza na Brian Umony, wakati Emmanuel Okwi anaweza kuanzia benchi tena. Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mkali, Uganda wakicheza mbele ya malefu ya mashabiki wao na Bara wakijaribu kulipa cha Dar es Salaam  mwaka jana. 
Timu hizi zimekutana mara 12 katika Challenge tangu mwaka 1975, kila timu ikishinda mechi tano, sare mbili na Bara imefunga mabao 16, wakati imefungwa mabao 17.
Uganda; Hamza Muwonge, Iguma Dennis, Godfrey Walusimbi, Henry Kalungi, Isaac Isinde, Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito, Moses Oloya, Robert Ssentongo, Hamisi Kiiza na Brian Umony.
Tanzania; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Franko Domayo, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, John Bocco na Mrisho Ngassa.  
Mungu zibariki timu zetu, Bara na Zanziabr leo, ibariki Tanzania. Amin.
MATOKEO YA JUMLA STARS NA CRANES TANGU 1975:
                     P    W  D   L    GF GA      Pts
Uganda         12 5    2    5    17 16       17
Tanzania       12 5    2    5    16 17       17
REKODI YA STARS NA CRANES CHALLENGE TANGU 1974:
Desemba 8, 2011; Nusu Fainali, Dar es Salaam
Uganda 3–1 Tanzania (dakika 120)
Januari 9, 2009; Kundi A Uganda
Tanzania 1-2 Uganda
Desemba 11, 2001; Kundi B Rwanda
Tanzania 1-0 Uganda
Desemba 1, 1995; Kundi B Uganda
Tanzania 2-1 Uganda B
Desemba 10, 1994; Fainali Kenya
Tanzania 2-2 Uganda: (Tanzania ilishinda kwa penalti 4-3)
Desemba 10, 1992; Fainali Mwanza
Tanzania B(Kakakuona) 0-1 Uganda
Desemba 17, 1990; Nusu Fainali Zanzibar
Tanzania 1-1 Uganda (dakika 120, Uganda ilishinda penalti 6-5)
Desemba 1, 1984; Kundi A Uganda
Tanzania 1-1 Uganda
Novemba 20, 1983; Kundi A Kenya
Tanzania 1-1 Uganda
Novemba 17, 1982; Kundi A Uganda
Tanzania 0-1 Uganda
Novemba 9, 1979; Kundi A Kenya
Tanzania 5-3 Uganda
Desemba 10, 1974; Fainali Dar es Salaam                                    
Tanzania 1-1 Uganda (Tanzania ilishinda kwa penalti 5-3)




CHELSEAAA YABWAGWA NJE KATIKA UEFA CHAMPIONZ LIGI LICHA YA KUIBUKA NA USHINDI MNONO WA MABAO 6-1


Mabingwa watetezi wa Ligi ya mabingwa Barani ulaya  Chelsea wametolewa nje ya michuano ya hiyo,
licha kuikandamiza   Nordsjaelland mabao sita kwa moja .

 Ushindi wa juventus Dhidi  ya  Shakhtar Donetsk huku  Rafa Benitez's akipata ushindi wa kwanza dhidi ya aikwa mkufunzi wa   Chelsea ulihitismisha ya chelsea  .

 Timu zote  mbili zilikosa mikwaju ya penati  kabla ya  David Luiz kufunga baada ya kuwahi mpira wa penati hiyo mara baada ya kukosa huku   Fernando Torres akifunga bao la pili kabla nusu ya kwanza haijamalizika  .

 Joshua John alisawazisha goli moja kabla ya   Torres hajafunga bao la pili  huku Gary Cahill, Juan Mata na  Oscar wakifunga katika kipindi cha pili .

Group E
1 Juventus              6   8 12

2 Shakhtar Donetsk 6  4 10

3 Chelsea                  6  6 10

4 Nordsjaelland         6  -18 1

MATOKEO MENGINE 

Celtic2 - 1Spartak Moscow

Chelsea6 - 1Nordsjaelland

Man Utd0 - 1CFR Cluj-Napoca

Barcelona0 - 0Benfica
Bayern Munich4 - 1BATE Borisov

Braga1 - 2Galatasaray

Lille0 - 1Valencia


TIMU ZILIZO INGIA HATUA YA MTOANO 
KUNDI A 
1 Paris SG  

2 FC Porto
KUNDI B
Schalke 

2 Arsenal
KUNDI C 
Malaga  

2 AC Milan

KUNDI D 
Borussia Dortmund  

2 Real Madrid

KUNDI E 
Juventus  

2 Shakhtar Donetsk

KUNDI F 
Bayern Munich  

2 Valencia
KUNDI G
Barcelona  

2 Celtic 
KUNDI H
Man Utd  

2 Galatasaray


BPL WIKIENDI: NI DABI ya MANCHESTER, City v Man United!

>>DIFENSI YAMCHENGUA FERGIE!!
>>MANCINI: ‘Kubwagwa NJE ULAYA si AIBU!!’
MAN_CITY-VICHWA_CHINI_BAADA_KICHAPOHUKU DABI ya JIJI la Manchester ikiwa kilingeni Jumapili ijayo Uwanjani Etihad kati ya Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England Manchester City na Vinara wa Ligi hiyo Manchester United, Sir AlexFERGIE_na_SIMUFerguson amehimiza Wachezaji wake wa Manchester United kuwa makini na Difensi yao inayovuja kama pakacha na mwenzake wa Manchester City, Roberto Mancini, baada ya kuumbuka kwa kubwagwa nje ya michuano ya Ulaya na kukosa hata kucheza EUROPA LIGI, amejipa moyo kuwa sasa mkazo wao upo kwenye Ligi na FA Cup.
Msimu huu, Man United imesharuhusu Mabao 32 katika Mechi zote walizocheza na hizo ni nyingi mno kupita desturi yao na Meneja wao Sir Alex Ferguson ameonya: “Inaleta wasiwasi. Tukicheza kama tulivyocheza na Reading na City wana Wachezaji warefu kina Balotelli na Dzeko, Mungu anajua nini kitatokea!”
++++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI WALIYOFUNGWA MAN UNITED kwa Msimu:
-2012/13: Goli 21 (Baada Mechi 15 tu)
-2011/12: 33
-2010/11: 37
-2009/10: 28
-2008/09: 24
-2007/08: 22
-2006/07: 27
-2005/06: 34
-2004/05: 26
-2003/04: 35
++++++++++++++++++++++++++++
Ingawa imeripotiwa Sentahafu wao mahiri na Nahodha wao Nemanja Vidic yuko fiti baada ya kupona goti lake na alitegemewa kucheza Mechi yao ya kukamilisha Ratiba ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, kwa vile wameshafuzu, Jumatano Usiku Uwanjani Old Trafford dhidi ya CFR Cluj, Ferguson amesema Mchezaji huyo anahitaji muda zaidi kujijenga upya.
++++++++++++++++++++++++++++++++
DABI=Historia:
-Dabi ya kwanza kabisa ilichezwa Mwaka 1881, Novemba 2, na West Gorton (St. Marks), ndio Manchester City sasa, walikuwa ndio Mwenyeji wa Newton Heath, sasa Manchester United, na Newton Heath wakaibuka kidedea kwa Bao 3-0.
-Hadi sasa zimeshachezwa jumla ya Dabi rasmi 164 na Man United ndio wanaongoza kwa kushinda 68 dhidi ya 46 za Man City huku sare zikiwa 50.
MICHUANO Man City Sare Man United
LIGI 40 49 58
FA CUP 3 0 6
LIGI CUP 3 1 2
NGAO ya HISANI 0 0 2
JUMLA 46 50 68
++++++++++++++++++++++++++++++++++
Nae Roberto Mancini, baada ya jana Jumanne Usiku kuchapwa Bao 1-0 na Borussia Dortmund huko Germany na kujihakikishia kumaliza mkiani mwa Kundi D la UEFA CHAMPIONZ LIGI nyuma ya Dortmund, Real Madrid na Ajax, na hivyo kukosa kusonga mbele na hata kutupwa EUROPA LIGI, amejipa moyo kuwa pigo hilo si aibu bali litawapa moyo kuutetea vyema Ubingwa wao wa England.
Hadi sasa kwenye Ligi, Man City wapo nafasi ya 2, Pointi 3 nyuma ya Vinara Man United.
+++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za juu:
[Kila Timu Mechi 15]
1 Man United Pointi 36
2 Man City 33
3 Chelsea 26
4 WBA 26
5 Tottenham 26
6 Everton 23
7 Swansea 23
8 West Ham 22
9 Stoke 22
10 Arsenal 21
+++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 8 Desemba 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v West Brom
Aston Villa v Stoke
Southampton v Reading
Sunderland v Chelsea
Swansea v Norwich
Wigan v QPR
Jumapili 9 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man City v Man United
[SAA 12 Jioni]
Everton v Tottenham
[SAA 1 Usiku]
West Ham v Liverpool
Jumatatu 10 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Fulham v Newcastle
Jumanne 11 Desemba 2012
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v Reading

UEFA CHAMPIONZ LIGI: NI HISTORIA, MABINGWA CHELSEA NJEEE!!!

UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZ>>CHELSEA saizi yao EUROPA LIGI!!
>>CELTIC, JUVE, GALATASARAY ZAKAMILISHA 16!!
+++++++++++++++++++++++++++++++
TIMU ZILIZOFUZU KUCHEZA RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16:
-KUNDI A: PSG, Porto
-KUNDI B: Schalke, Arsenal
-KUNDI C: Malaga, AC Milan
-KUNDI D: Dortmund, Real Madrid
-KUNDI E: Juventus, Shakhtar Donetsk
-KUNDI F: Bayern Munich, Valencia
-KUNDI G: Barcelona, Celtic
-KUNDI H: Manchester United, Galatasaray
+++++++++++++++++++++++++++++++
Waliokuwa Mabingwa wa Ulaya, Chelsea, wametupwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI licha ya kuishindilia Nordsjælland Bao 6-1 na kumaliza Mechi katika Kundi E wakiwa nafasi ya 3 baada ya Juventus kuifunga Shakhtar Donetsk Bao 1-0 na kutwaa Nambari Wani na huku Shakhtar wakikamata nafasi ya pili, matokeo ambayo yamewafanya Chelsea kuwa Mabingwa wa kwanza watetezi kutolewa kwenye hatua ya Makundi.
MATOKEO:
Jumatano Desemba 5
Shakhtar Donetsk 0 Juventus 1
Chelsea 6 Nordsjælland 1
Lille 0 Valencia 1
Bayern München 4 BATE Borisov 1
Barcelona 0 Benfica 0
Celtic 2 Spartak Moskva 1
Manchester United 0 CFR 1907 Cluj 1
Braga 1 Galatasaray 2
FAHAMU: Droo ya kupanga Ratiba ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 itafanyika Desemba 20

 

 

NDOTO YA LIONEL MESSI KUVUNJA REKODI YA GERD MULLER YA MABAO 85 KIPINDI CHA MWAKA MMOJA YATOWEKA.


Mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi amejikuta akitolewa nje kwa machela kutokana na kupata maumivu makali katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Benfica.

Tito Vilanova hakumuanzisha mshambuliaji huyo kama ilivyo kawaida yake na kumuingiza katikati ya mchezo kipindi cha pili kwa lengo la kusukuma mashambuliaji zaidi.

Zikiwa zimesalia dakika tano mchezo huo kumalizika wakati huo matokeo yakiwa ni sare ya bila mabao, mshambuliaji huyo anayetazamiwa na wengi kushinda tuzo ya Ballon d'Or favorite aliwekwa chini na kuanza kulalamikia maumivu ya mguu wake kabla ya kutolewa nje ya dimba la Camp Nou kwa matibabu.

Maafisa wa Barcelona muda mfupi baadaye wakatumia mtandao wa kijamii wa twitter kwa kutoa ujumbe
"Messi amepatwa na mchubuko katika mguu wake wa kushoto . Anatakiwa kufanyiwa vipimo zaidi ukubwa wa jeraha lake,".

Baada ya mshambuliaji huyo kutolewa nje hakukuwa na mabadiliko yoyote ya matokeo na hivyo mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 0-0, matokeo ambayo yanaiondoa Benfica mashindano na kusogezwa katika Europa League wakati ambapo Celtic ikisonga mbele baada ya kuichapa Spartak Moscow.

Wengi walitazama kuwa usiku wa jumatano hii utakuwa ni usiku wa kihistoria kwa Messi kuvunja rekodi ya Gerd Muller ya kufunga magoli 85 katika kipindi cha mwaka mmoja.

Aidha majeraha ya Messi huenda yakamuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki kadhaa mpaka katika kipindi cha majira ya baridi, hiyo ikimaanisha kuwa Messi atakuwa ameshindwa kuvunja rekodi hiyo ya mwasisi wa kijerumani Muller

 

WACHEZAJI WA ERITREA WALIOTOWEKA WAJITOKEZA NA KUOMBA HIFADHI YA UKIMBIZI.

WACHEZAJI 17 na kiongozi mmoja wa timu ya taifa ya Eritrea waliokuwa wametoweka katika hoteli yao jijini Kampala, Uganda Jumapili wamonekana. Wachezaji hao walikutana na Waziri wan chi hiyo anayeshughulika masuala ya maafa, Musa Echweru na kuomba hifadhi kama wakimbizi huku wenzao wengine waliobakia ambao ni wachezaji wawili na viongozi watano wakirejea nyumbani Jumanne. Echweru alithibitisha kuwasiliana na wachezaji hao na kusema kuwa wamepeleka suala suala hilo kwa mamlaka husika ili waweze kulishughulikia. Eritrea walitolewa katika mashindano ya Kombe la Cecafa Jumamosi iliyopita na timu nzima ilitakiwa kurejea nyumbani Jumanne. Hiyo imekuwa ni tabia ya kawaida kwa wachezaji wa Eritrea kutoweka mara baada ya mechi za mashindano ambapo mwaka 2007 katika michuano hiyo iliyofanyika nchini Tanzania wachezaji 12 walipotea kabla ya kurudia tukio kama hilo miaka miwili baadae katika mashindano kama hayo yaliyofanyika nchini Kenya. Matukio ya uvunjaji wa sheria za haki za binadamu na kukosekana kwa uhuru wa vyombo vya habari pamoja na uhuru wa kisiasa nchini Eritrea ndio inachangia kwa kiasi kikubwa wachezaji hao kuamua kutoweka na kushindwa kurudi kwao huku wakiomba hifadhi ya kikimbizi katika nchi walizokwenda.

MESSI HATIHATI KUIKOSA REAL BETIS.

KLABU ya Barcelona imesema kuwa mshambuliaji wake nyota Lionel Messi amepata majeruhi ya goti lake la kushoto na kuna hatihati akakosekana katika wa La Liga dhidi ya Real Betis unaotarajiwa kuchezwa Jumapili. Katika taarifa iliyotumwa katika tovuti ya klabu hiyo imesema vipimo alivyofanyiwa nyota huyo vimethibitisha kuwa amepata mchubuko katika mfupa wa goti lake na kupona kwake kutakuwa taratibu hivyo kuwepo uwezekano mkubwa wa kukosa mchezo huo. Mchezaji huyo bora wa dunia aliondolewa katika machela katika mwishoni mwa mchezo wa kundi G wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Benfica baada ya kugongana na golikipa wa timu hiyo wakati akijaribu kufunga. Pamoja na sare ya bila kufungana iliyopata Barcelona katika mchezo huo walikuwa tayari wamefuzu katika hatua ya timu 16 bora wakiwa vinara wa kundi lao huku wapinzani wao Benfica wakishindwa kusonga mbele na kupata nafasi katika Europa League. Messi amebakisha bao moja ili kufikia rekodi ya mabao 85 aliyoweka Gerd Muller katika kipindi cha mwaka mmoja, hiiyo ikiwa mwaka 1972.

CAF REVEALS TOP THREE.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limetaja majina matatu ya mwisho ya wachezaji watakaogombea tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2012. Nyota wa Ivory Coast Yaya Toure ambaye anashikilia tuzo ya mwaka jana na Didier Drogba ambaye ameshinda tuzo hiyo mwaka 2006 na 2009 watakuwa wakipambana na kiungo wa kimataifa wa Cameroon na klabu ya Barcelona Alexander Song. Kwa upande wa orodha ya mwisho ya wachezaji wanaocheza ndani ya bara la Afrika wachezaji wa Zambia Rainford Kalaba na Stoppila Sunzu ambao wote wanacheza katika klabu ya TP Mazembe ya DRC na Mohamed Abou Trika wa Misri na klabu ya Al Ahly ndio watakaogombea tuzo hiyo. Mshindi katika tuzo hizo atatangazwa katika sherehe zitakazofanyika jijini Accra, Ghana Desemba 20 mwaka huu.

SINA MUDA WA KUPUMZIKA - MOURINHO.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho amesema kuwa hatakuwa na muda wa kupumzika wakati akiamua kuondoka katika klabu hiyo. Kumekuwa na tetesi kuwa Mourinho ambaye ni raia wa Ureno ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huku taarifa hizo zikielekeza kuwa kocha huyo atakwenda katika klabu za Manchester City au Paris Saint-Germain. Lakini kocha huyo wa zamani wa klabu za Porto, Chelsea na Inter Milan amesema kuwa kama ataondoka Santiago Bernabeu anatarajia haraka kutafuta timu nyingine na sio kupumzika. Mourinho amesema hatachukua likizo ya mwaka mzima kwa akiondoka Hispania ataelekea kokote kule kuendelea kufundisha. Madrid kwasasa inashika nafasi ya tatu katika La Liga wakiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo Barcelona kwa alama 11 huku wakiwa wamepitwa lama tano na mahasimu wao wa jiji Atletico Madrid ambao wanashika nafasi ya pili.

SHEHATA ATUPIWA VIRAGO BAADA YA KUFUNDISHA MIEZI MWILI NCHINI QATAR.

KLABU ya Al Arbi ya Qatar imemtupia virago vyake kocha wa zamani wa Misri Hassan Shehata baada ya kuifundisha klabu hiyo kwa kipindi cha miezi miwili pekee. Klabu hiyo ilitangaza kusitisha mkataba na Shehata kutokana na matokeo mabao iliyopata timu hiyo katika michezo yake ya Ligi Kuu nchini humo. Akihojiwa na televisheni ya Qatar Shehata amesema kuwa ameshangazwa na uamuzi uliochukuliwa na klabu hiyo ingawa kwa upande mwingine anashukuru kuondoka kwani alifanya kila awezalo lakini wachezaji wameshindwa kujisaidia. Shehata aliendelea kusema kuwa kuanza sasa atakuwa hakubali kazi yoyote ya kufundisha timu mpaka aifanyie uchunguzi klabu husika yasije kumkuta kama yaliyomkuta Al Arbi. Klabu hiyo sasa inashika mkia katika msimamo wa ligi nchini humo wakiwa wamejikusanyia alama nne pekee.

EUROPA LIGI: Alhamisi Timu 9 kuwania nafasi 5 zilizobaki!

>>19 tayari zishatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 32, Bado 5!
>>WAMO Liverpool na Tottenham kuwania nafasi!
EUROPA_LIGI_CUPKlabu 19 tayari zimeshatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA LIGI lakini bado zipo nafasi 5 zinazogombewa na Timu 9 ambazo zitapatikana Alhamisi Desemba 6 katika Mechi za mwisho za Makundi, na katika hizo 9 zilizo kwenye patashika ni Liverpool na Tottenham lakini wenzao Newcastle wao tayari wameshavuka.
Timu hizi 24 toka EUROPA LIGI zitajumuika na Timu 8 wamalizaji wa nafasi ya 3 katika Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ili kufanya jumla ya Timu 32 zitakazoingia Droo ya kupanga Raundi ya Mtoano itayochezwa nyumbani na ugenini.
Droo ya kupanga Raundi ya Mtoano ya Timu 32 itafanyika Desemba 20.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
KLABU 19 ZILIZOFUZU:
Olympique Lyonnais
FC Rubin Kazan
FC Internazionale Milano
Hannover 96
Bayer 04 Leverkusen
FC Metalist Kharkiv
FC Anji Makhachkala
Fenerbahçe SK
VfL Borussia Mönchengladbach
AC Sparta Praha
S.S. Lazio
Club Atlético de Madrid
FC Viktoria Plzeň
Levante UD
KRC Genk
FC Dnipro Dnipropetrovsk
SSC Napoli
Newcastle United FC
FC Girondins de Bordeaux
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Mabingwa watetezi Atlético de Madrid wao wamo katika Timu 19 ambazo tayari zimefuzu pamoja na Timu nyingine ya England, Newcastle.
Timu 9 zinazosaka nafasi 5 ni Liverpool FC au BSC Young Boys, toka Kundi A; FC Steaua Bucureşti au VfB Stuttgart au FC København toka Kundi E; FC Basel 1893 au Videoton FC toka Kundi G na Tottenham Hotspur FC au Panathinaikos FC kutoka Kundi J.
MAHESABU ya LIVERPOOL na TOTTENHAM KUFUZU:
KUNDI A:
Mechi:
-BSC Young Boys (Pointi 7) v FC Anji Makhachkala (Pointi 10)
-Udinese Calcio (Pointi 4) v Liverpool FC (Pointi 7)
Mahesabu:
-Anji wamefuzu hata kama watakutwa kwa Pointi na Liverpool na Young Boys kwa sababu ya rekodi yao bora ya uso kwa uso na wapinzani wao.
-Liverpool wakishinda wataipiku Young Boys kwa vile wana rekodi bora kupita wao. Sare itawasaidia ikiwa tu Young Boys hawashindi. Liverpool wakifungwa tu, wako nje.
-Udinese wako nje.
KUNDI J:
Mechi:
-NK Maribor (Pointi 4s) v S.S. Lazio (Pointi 9)
-Tottenham Hotspur FC (Pointi 7) v Panathinaikos FC (Pointi 5)
Mahesabu:
-Lazio wameshafuzu na watamaliza Nambari wani ikiwaTottenham hawashindi.
-Ikiwa Lazio na Tottenham watamaliza wamefungana Pointi, Mshindi ataamuliwa kwa tofauti ya Magoli au wakifungana kwa hilo basi Magoli ya kufunga na hilo likiwa sawa, Mshindi ataamuliwa kwa yupi yuko juu katika Listi ya Ubora ya UEFA.
-Tottenham watafuzu wakitoka sare au ushindi.
-Panathinaikos watafuzu wakishinda.
-Maribor tayari wako nje.
RATIBA:
Alhamisi Desemba 6
BSC Young Boys v FC Anzhi Makhachkala
Udinese Calcio v Liverpool FC
Hapoel TelvAviv FC v A. Académica de Coimbra
FC Viktoria Plzen v Club Atlético de Madrid
AEL Limassol FC v Olympique de Marseille
Fenerbahçe SK v VfL Borussia Mönchengladbach
CS Marítimo v Club Brugge KV
FC Girondins de Bordeaux v Newcastle United FC
VfB Stuttgart v Molde FK
FC København v FC Steaua Bucuresti
FC Dnipro Dnipropetrovsk v AIK
SSC Napoli v PSV Eindhoven
KRC Genk v FC Basel 1893
Sporting Clube de Portugal v Videoton FC
FC Internazionale Milano v Neftçi PFK
FK Partizan v FC Rubin Kazan
Olympique Lyonnais v Hapoel Kiryat Shmona FC
Athletic Club v AC Sparta Praha
NK Maribor v S.S. Lazio
Tottenham Hotspur FC v Panathinaikos FC
SK Rapid Wien v FC Metalist Kharkiv
Bayer 04 Leverkusen v Rosenborg BK
Levante UD v Hannover 96
FC Twente v Helsingborgs IF

No comments:

Post a Comment