Ngssa; Sasa mutu ya fweza |
BIASHARA
imeisha. Azam FC imemuuza Mrisho Khalfan Ngassa kwa dola za Kimarekani 75,000
kwenda El Merreikh ya Sudan ambako amesaini mkataba wa miaka miwili,
utakaomuwezesha kulipwa mshahara wa dola za Kimarekani 4,000 kwa mwezi huku naye
akilipwa dola 50,000 za kusaini.
Awali,
Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu Ngassa wenye thamani ya dola
100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said Bakhresa akakataa akisema
utambana mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu nyingine.
Sasa Ngassa
baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwishoni
mwa wiki hii, atakwenda Sudan kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na klabu hiyo, ambayo
ni jambo la kawaida kucheza hatua ya makundi ya michuano ya klabu Afrika.
Azam FC
imesema imeweka mbele maslahi ya mchezaji na taifa kwa ujumla katika maamuzi ya
kumuuza Sudan, kutoka Simba alikokuwa akicheza kwa mkopo. “Hii timu (Merreikh)
kila mwaka inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, maana yake
huyu mchezaji atakwenda kupata maendeleo na kuja kuisaidia zaidi Tanzania
katika mashindano ya kimataifa,”alisema kiongozi mmoja wa Azam.
Alipoulizwa kuhusu
Simba SC aliyokuwa anaichezea klabu hiyo, kiongozi huyo alisema wao walimtoa
kwa mkopo Ngassa kwenda kwa Wekundu wa Msimbazi hadi Mei 31, mwakani na mkataba
wao ndio unasema hivyo.
“Sisi
tuliwapa Simba huyu mchezaji kwa mkopo hadi Mei 31 na wakatupa Sh. Milioni 25,
ila tuko tayari kuwarudishia fedha zao walizota, lakini huyu mchezaji ni mali
yetu na hata TFF wanatambua hilo, na
tumekwishamuuza Merreikh,”alisema.
Alipoulizwa kuhusu
Simba kusaini mkataba mpya na Ngassa, alisema; “We uliona wapi dunia nzima timu
inapewa mchezaji kwa mkopo halafu inamsainisha mkataba? Simba lazima ifike
wakati waache kurudia makosa, haya ndio mambo ya Mbuyu Twite sasa,”alisema
kiongozi huyo wa Azam.
Katika kukamilisha
mauzo ya mchezaji huyo, kiongozi wa Marreikh akiwa Dar es Salaam mbele ya
viongozi wa TFF na Azam, alipigiwa simu Ngassa aliye hapa Kampala, Uganda na
kuhusishwa katika dili hilo, naye akakubali ndipo mambo yakamalizwa.
Aidha, Azam wameomba
TFF ihakikishe kunakuwa na ulinzi katika kambi ya timu ya taifa mjini hapa, ili
Simba wasimfanyie vurugu Ngassa na kumvuruga kisaIkolojia, wakati ndiyE tegemeo
la timu katika kampeni ya kutwaa Kombe la Challenge mwaka huu mjiini hapa.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe
akizungumza kutoka Dar es Salaam, alisema kwamba watawapeleka mahakamani Azam kwa
kitendo cha kumuuza mchezaji wao kinyume cha sheria.
“Haiwezekani
wamuuze wao, wakati wao walituuzia huyu mchezaji na sisi tuna mkataba ambao
tulisaini nao, hii ni kinyume cha sheria na sisi tutawapeleka mahakamani,”alisema
Hans Poppe ambaye anatua kesho mjini hapa.
Azam
walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu baada ya kukerwa na
kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika
Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi
ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alifanya
hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam
kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara
nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa
kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa
baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji
huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni
30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 akipewa gari.
HAKUNA MAJERUHI STARS, VIJANA WAKO TAYARI KUCHINJA KORONGO
Kikosi cha Stars |
KOCHA wa
timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesema hana
majeruhi hata mmoja kikosini mwake kuelekea mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la
Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kesho, Uwanja wa
Mandela, Namboole mjini hapa.
Akizungumza leo
mjini hapa baada ya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu Kyambogo, Poulsen
alisema kwamba timu iko tayari kwa mchezo huo wa kesho unaotarajiwa kuwa wa
kukata na shoka.
“Vijana
wamejiandaa vizuri kabisa na wote wako katika hali nzuri ya kucheza ila
tunachoomba ni fair play kutoka kwa muamuzi maana tunacheza na wenyeji ambao
wana watazamaji wengi,” alisema.
Alisema timu
zote mbili ni nzuri na iwapo muamuzi atachezesha vizuri basi utakuwa ni mchuano
mkali. “Vijana wana ari na mchezo huu na tukipewa fair play tutacheza vizuri
kama tulivyofanya katika michezo dhidi
ya Rwanda,” alisema Poulsen.
Refa wa
mechi ya Cranes na Stars anatarajiwa kuwa Mohamed El Fadil kutoka Sudan ambaye
pia alichezesha mechi ya Stars dhidi ya Rwanda Robo Fainali.
Alisema ana
furaha kwa kuwa hakuna majeruhi hata mmoja na pia aliwasifu wachezaji wake kwa
kuonyesha umoja na nidahmmu ya hali ya juu. “Hawa wanakaa kama familia si
unawaona walivyo pamoja?” alisema Poulsen na kuongeza kuwa hilo ni muhimu sana
kwa mchezaji.
Naye kocha
msaidizi, Sylvester Mash alisema Stars ina nafasi kubwa sana ya kushinda mechi
hii kwa sababu wenyeji wao, The Cranes watakuwa wanacheza kwa wasiwasi kwa kuwa
wako nyumbani .
“Timu yetu ina
hamasa kabisa na ukizingatia Uganda wako nyumbani, wao ndio wana tension kubwa
zaidi,” alisema na kuongeza kuwa mchezo huu utakuwa wa kusisimua sana.
Akizungumza
kutoka Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhaminiwa
Stars, George Kavishe alisema Stars ina kila sababu ya kutinga fainali na kunyanyua
kombe kwa mara ya nne.
“Sisi kama
wadhamini tunasubiri ushindi maana tuna imani na Stars na hatua waliyofikia ni
nzuri nay a kutia moyo kwa hivyo watanzania wajitokeze kwa wingi na kuufuatilia
mchezo huu kesho,” alisema Kavishe.
Mchezo wa
Stars na Cranes utatanguliwa na semi fainali ya kwanza kati ya Zanzibar na
Kenya ambao pia ni mchezo wa kusisimua kwani timu zote mbili zimeshaonyesha
uwezo mkubwa.
Kocha wa
Zanzibar Salum Nassor ameshatangaza mara mbili akiwa Zanzibar na hapa Kampala
kuwa iwapo hataondoka na kombe basi atabwaga manyanga.
TFF WAITAFUTIA USHINDI WA MEZANI SERENGETI BOYS
Kikosi cha U17 ya Kongo kilichoitoa Serengeti |
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limewasilisha barua ya malalamiko yake dhidi ya
matumizi ya wachezaji wenye umri mkubwa na unyanyasaji uliofanyuwa kwa
maofisa wa timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 wa
Serengeti Boys wakati wa mechi ya marudiano ya michuano ya Mataifa ya
Afrika kwa Vijana dhidi ya Congo.
Serengteti
Boys iliondolewa kwenye mashindano hayo kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya
kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyofanyika
Novemba 18, 2012 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es salaam na baadaye
kukubali kipigo cha mabao 2-0 kwenye mechi ya marudiano jijini
Brazaville Jumapili iliyopita.
Hata
hivyo, mechi hizo mbili zilizingirwa na matukio tata, hasa kuhusu umri
wa wachezaji wa Congo ambao kimaumbile walionekanakuwa ni umri mkubwa
zaidi na kusababisha TFF kuwasiliana na Shirikisho la Mpira wa Miguu la
Afrika (CAF) kuhusu njia zinazowezekana kupata uthibitisho wa umri wa
wachezaji hao, lakini ilishindikana na ndipo TFF ilipocheza mechi hiyo
ikiwa na imeweka pingamnizi.
Katika
barua iliyotumwa CAF jana, TFF imerejea barua ya pingamizi
aliyokabidhiwa kamisaa wa mechi ya kwanza jijini Dar Es salaam, Bw.
Chayu Kabalamula na malalamiko yaliyowasilishwa kwa kamisaa wa mechi ya
marudiano kuhusu vurugu walizofanyiwa maofisa wa timu.
Katika
barua hiyo, TFF imeomba CAF iagize kuwa wachezaji wote wa Congo
waliocheza mechi hizo mbili wapimwe tena kwa kutumia kipimo cha M.R.I na
gharama za zoezi hilo zilipiwe na TFF; na pili Shirikisho limeomba kuwa
CAF ikubali kuipa Tanzania wiki tatu za kukusanya ushahidi na
kuuwasilisha Cairo kwa ajili ya maamuzi.
Kwa
mujibu wa kanuni za mashindano hayo, nchi shiriki zinatakiwa kuwapima
wachezaji wake kwa kutumia kipimo cha M.R.I ambacho kinaweza kutambua
umri wa vijana walio chini ya miaka 17 na kwamba matokeo yake yanatumwa
CAF, ambayo itahifadhi matokeo hayo hadi hapo kutakapotokea pingamizi na
ndipo itafanyia kazi kwsa kutoa matokeo ya vipimo hivyo.
“Ni
matumaini yetu kuwa suala letu litafanyiwa kazi na kutolwewa ufumbuzi
ili kulinda soka la vijana barani Afrika dhidi ya vitendo vilivyokomaa
vya udanganyifu wa umri,” alisema katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah.
Akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari jana, kocha Jacob Michelsen
alisema alishangaa kuona wachezaji wenye umri mkubwa zaidi wakichezeshwa
kwenye mechi ya marudiano, lakini akaisifu TFF kuwa inafuata njia
sahihi ya maendeleo na haina budi kuendelea na programu yake ya soka la
vijana.
"Najivunia
vijana wangu kwa kuwa walijituma kwa muda wote pamoja na kwamba wenyeji
waliongeza wachezaji wenye umri mkubwa zaidi kuliko waliokuja huku,"
alisema kocha huyo kutoka Denmark.
"Kitu
cha msingi ni kufuata njia sahihi ya kuendeleza soka na natumaini TFF
iko kwenye njia sahihi na itaendelea na programu yake ya vijana. Hakuna
njia ya mkato kama mnataka maendeleo. Ni lazima tufuate njia sahihi na
matunda yake tutayaona baadaye.
"Kila mara nasema mambo (ya vijana) huchukua muda mrefu (Things Take Time) na hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu.
"Wenzetu walitumia njia za ajabu na hata hiyo penati ya bao la kwanza haikuwa faulo. Ilitokea nje kabisa ya eneo la penati. Refa
alimuangalia
kibendera akaona ametulia, akamuangalia beki mchezaji akamuona
amesimama, mara akaangalia juu na kupuliza filimbi kuonyesha kuwa ni
penati."
Naye
kocha msaidizi, Jamhuri Kihwelo alishindwa kujizuia na kujikuta
akibubujika machozi wakati alipoelezea jinsi alivyoshambuliwa na askari
kabla ya mchezo huo.
ROLLING STONE YAANDAA KOZI YA MAKOCHA DARAJA C
KITUO
cha Kukuza Vipaji cha Rolling Stone kwa kushirikiana na Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kimeandaa kozi ya leseni C ya walimu wa
mpira wa miguu itakayofanyika kuanzia Desemba 10, 2012 hadi Desemba 23,
2012 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Kozi
hiyo itahusisha makocha walio na Cheti cha Kumaliza Elimu ya Sekondari
au wale waliohitimu kozi ya ualimu wa mpira wa miguu ya ngazi ya kati
(intermediate).
Mkurugenzi
wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni alisema kuwa washiriki wa kozi hiyo
wanatakiwa kuwa wamewasili Arusha ifikapo Desemba 9, 2012 na wanatakiwa
kwenda na vyeti vyao halisi vya elimu. Alisema tayari Rolling Stone
wameshasajili walimu 25 ambao watashiriki kozi hiyo na hivyo kuwataka
watu wengine wanye sifa kutoka mkoa wa Arusha na mikoa mingine
kujitokeza kushiriki mafunzo hayo muhimu.
Kayuni
alisema kuwa kadri taifa litakavyozalisha walimu wengi, ndivyo taifa
litakavyokuwa na uwezo wa kuandaa watoto na vijana wengi katika misingi
sahihi ya mpira wa miguu na hivyo kuwa na matumaini makubwa ya kufanya
vizuri.
Kozi
hiyo itaendeshwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Kayuni kwa
kushirikiana na mkufunzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika
(CAF), Bw. Dominic Niyonzima kutoka Rwanda.
Kwa
mujibu wa Rolling Stone, kila mshiriki atajigharimia nauli ya kwenda
Arusha na atatakiwa kwenda na ada ya fedha zinazolingana na Dola 100 za
Kimarekani (dola moja ni sawa na Sh1,580 za Tanzania).
SITA TU WAPITISHWA KUGOMBEA TAFCA
KAMATI ya
Uchaguzi ya Chama cha Waliku wa Mpira wa Miguu (TAFCA) imetangaza matokeo ya usaili
wa wagombea uongozi chama hicho, ikiwa imepitisha wagombea sita sita na
kuwaengua wagombea watano kwenye nafasi tofauti.
Baada ya
usaili wa wagombea hao, Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA iliwaengua wagombea hao
watano kwa kutokidhimasharti ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya TAFCA na Kanuni ya
9 ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na pia kutokidhi utashi wa masharti
ya 11 (1) ya kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Katika
nafasi ya mwenyekiti Oscar Don Korosso alipitishwa kuwa mgombea pekee baada ya
Kenedy Mwaisabula na Jamhuri Kihwelo kuenguliwa kwa kutokidhi masharti ya ibara
ya 26 (2) ya Katiba ya TAFCA na kanuni ya tisa ya Kanuni za Uchaguzi za
Wanachama wa TFF.
Katika
nafasi ya makamu mwenhyekiti, Kamati imempitisha Lister J. Manyara kuwa mgombea
pekee wa nafasi hiyo huku Marco Bundara akipitishwa kuwa mgombea pekee wa
nafasi ya katibu mkuu wa TAFCA.
Hali
kadhalika wagombea wawili wa nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF, Wilfred
Kidau na Magoma Rugora wamekidhi masharti ya Katiba ya TAFCA na Kanuni za
Uchaguzi za Wanachama wa TFF na hivyo watachuana kuwania kura za wajumbe wa
mkutano mkuu, huku Ally A Mtumwa
akienguliwa kwa kutokidhi masharti ya kanuni ya 11 (1) ya Kanuni za Uchaguzi za
Wanachama wa TFF.
Katika
nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji, wagombea wote wawili, Abubakar
Balingula na Aboubakar Salum wameenguliwa kwa kutokidhi masharti ya Ibara ya 26
(2) ya Katiba ya TAFCA na Kanuni ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa
TFF.MBWANA SAMATTA KINARA WA KUFUMANIA NYAVU TP MAZEMBE MSIMU HUU.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayechezea klabu ya TP Mazembe Mbwana Samatta amekuwa wa kwanza katika orodha ya wafungaji bora wa klabu hiyo iliyotolewa jana.
Taarifa hiyo ambayo ipo kwenye mtandao wa klabu hiyo inasema TP Mazembe msimu wa 2012 imefunga jumla ya mabao 112 na Mbwana Samatta amefunga mabao 23.
Mtanzania Mbwana Samatta ambaye huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)humwita jina la utani Samagoal amemaliza akiwa mfungaji bora kwa kufunga mbao 23 katika mashindano yote, mabao 6 akiyafunga katika mashindano ya klabu bingwa ya Afrika ambapo alishika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora wa msimu wa mashindano hayo.
Mtanzania mwingine Thomas Ulimwengu ameshika nafasi ya nne akiwa amefunga mabao 9 katika msimu mzima sawa na Given Singuluma.
Ifuatayo ni orodha kamili iliyotolewa na TP Mazembe kwenye mtandao wake
1.Samatta mabao 23, 2. Mputu mabao 16, 3. Lungu mabaon 13, 4.Ulimwengu na Singuluma mabao tisa, 6. Kanda na Traore mabao sita, Salakiaku mabao matano, 8. Bokanga na Kalaba mabao manne, 10.Lusadisu na Sinkala TUSILU mabao matatu, 13. Ilongo, Kasongo, Nkulukuta, Kabangu mabao mawili, 17. Hichani, Kasusula, Kanteng, Lofo, Sunzu na sundry.
Katika ligi ya mabingwa wa Afrika wanaongoza kwa mabao ni
Emmanuel CLOTTEY wa Berekum Chelsea ambaye amefunga mabao 12 matatu kwa Penati
Mbwana Samatta alifunga mabao sita ya kawaida sawa na mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe Treasury Mputu lakini yeye moja ni kwa njia ya penalti na Mohamed Aboutrika wa Al Ahly lakini yeye mabao mawili ni kwanjia ya penalti.
Michuano ya Kombe la Uhai
inayoshirikisha timu B za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inatarajia
kuanza Desemba 7 mwaka huu na kumalizika Desemba 22 mwaka huu.
Mashindano haya ambayo yamedhaniwa na kampuni ya Azam kupitia maji ya Uhai yatashiriki wachezaji ambao usajili wao ulifanyika na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata leseni. Hakutakuwa na usajili mwingine wowote mbali na ule uliofanyika sambamba na wa Ligi Kuu.
Taratibu zote za michuano hiyo zitafahamishwa kwa klabu husika ikiwemo ratiba ya michuano hii
Mashindano haya ambayo yamedhaniwa na kampuni ya Azam kupitia maji ya Uhai yatashiriki wachezaji ambao usajili wao ulifanyika na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata leseni. Hakutakuwa na usajili mwingine wowote mbali na ule uliofanyika sambamba na wa Ligi Kuu.
Taratibu zote za michuano hiyo zitafahamishwa kwa klabu husika ikiwemo ratiba ya michuano hii
MWAKALEBELA AJA NA UHURU DAR CORPORATE BONANZA
TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini ni miongoni mwa
timu nane zitakazoshiriki bonanza la kusheherekea miaka 51 ya uhuru wa
Tanganyika litakalofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es
Salaam Desemba 9 mwaka huu kuanzia saa mbili asubuhi.
Mwenyekiti wa TASWA Majuto Omary alisema kuwa walipata barua toka Mkurugenzi wa kampuni ya Vennedrick (T) Limited kupitia Mkurugenzi wake Fredrick Mwakalebela na wameshathibitisha kuwa watashiriki.
Bonanza hili linameandaliwa na kampuni ya Vennedrick (T) Limited na litachezwa kwa mtindo wa ligi na timu mbili toka kila kundi zitafuzu hatua ya nusu fainali na limedhaminiwa na NMB banki na sasa wachezaji wa TASWA wapo kwenye maandalizi.
Timu za Barrick, NMB, DSTV na Radio Times zipo kundi A na TASWA FC, Jubilee, Azam Group na wenyeji Gymkhana wapo kundi B
Mwakalebela amesema kuwa mshindi wa kwanza, wa pili na watatu watapata zawadi na lengo la mashindano haya mbali na kuadhimisha miaka 51 ni kutumia fursa kujadili masuala mbalimbali ya michezo, matatizo na maendeleo na nini kifanyike.
Mwenyekiti wa TASWA Majuto Omary alisema kuwa walipata barua toka Mkurugenzi wa kampuni ya Vennedrick (T) Limited kupitia Mkurugenzi wake Fredrick Mwakalebela na wameshathibitisha kuwa watashiriki.
Bonanza hili linameandaliwa na kampuni ya Vennedrick (T) Limited na litachezwa kwa mtindo wa ligi na timu mbili toka kila kundi zitafuzu hatua ya nusu fainali na limedhaminiwa na NMB banki na sasa wachezaji wa TASWA wapo kwenye maandalizi.
Timu za Barrick, NMB, DSTV na Radio Times zipo kundi A na TASWA FC, Jubilee, Azam Group na wenyeji Gymkhana wapo kundi B
Mwakalebela amesema kuwa mshindi wa kwanza, wa pili na watatu watapata zawadi na lengo la mashindano haya mbali na kuadhimisha miaka 51 ni kutumia fursa kujadili masuala mbalimbali ya michezo, matatizo na maendeleo na nini kifanyike.
TIMU za taifa za Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars na Visiwani, Zanzibar Heroes kesho zinatarajia kujitupa uwanjani kwa nyakati tofauti kuwania nafasi ya kucheza fainali ya michuano ya Cecafa Tusker Cup inayofanyika jijini Kampala, Uganda. Zanzibar Heroes ambao wametinga hatua hiyo baada ya kuindoa Burundi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 6-5 katika mchezo wa robo fainali itaingia uwanjani kuchuana na timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars ambayo iliiondosha Malawi kwa bao 1-0 lililofungwa na mchezaji wa zamani wa Yanga Mike Baraza. Kwa upande wa Kilimanjaro Stars wao wataingia uwanjani huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuiondosha Rwanda katika michuano hiyo baada ya kuifunga mabao 2-0 yaliyofungwa na nyota wake machachari Amri Kiemba na John Bocco ambaye anashikilia usukani wa kufunga mabao mengi sambamba na Mrisho Ngassa wote wakiwa na mabao matano. Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Uganda wametinga katika hatua hiyo baada ya kuifunga timu ngumu ya Ethiopia ambayo itashiriki michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani kwa mabao 2-0 hivyo Stars haitakuwa na kazi rahisi katika mchezo wa leo. Kocha wa Stars Kim Poulsen amesema kuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya kuikabili Uganda na wana matumaini ya kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo ingawa alikiri hautakuwa mchezo rahisi. Mchezo wa kwanza utakaoanza unatarajiwa kuwa kati ya Zanzibar Heroes na Harambee Stars majira ya saa 10 za jioni wakati mchezo utakaofuata utachezwa majira ya saa moja usiku.
WALEVI, WAZINZI HARAMBEE STARS WAPANDISHWA NDEGE KUJA KUIVAA ZANZIBAR HEROES KESHO
Paul Wer |
Wawili hao
waliondoka jana usiku Nairobi, mara tu baada ya Harambee Stars kuvuzu Fainali,
wakiifunga 1-0 kwa mbinde Malawi na tayari wapo Kampala, Uganda kwa ajili ya
mchezo huo dhidi ya Zanzibar Stars.
Baada ya
kuifunga 1-0 Sudan Kusini katika mchezo wa pili wa Kundi A, wachezaji hao walikwenda
kujirusha kwenye klabu ya usiku na kurejea kambini na wanawake, jambo ambalo
lilifanya asubuhi yake waoandishwe ndege wote kurejea Nairobi, lakini kutokana
na mchecheto wa mechi ya kesho, wamerejeshwa.
Kocha wa Harambee
Stars, James Nandwa aliliomba Shirikisho la Soka Kenya (FKF) liliwarejeshe wachezaji
hao kwa ajili ya Nusu Fainali.
Kocha wa Fisa
FC, Charles ‘Korea’ Omondi, ambaye amekuwa akifanya mazoezi na wachezaji hao tangu
warejeshwe nyumbani, amethibitisha wamebadilika kinidhamu na wako vizuri
kimchezo.
Were na
Omondi wapo kwa mkopo AFC Leopards na Gor Mahia kutoka timu inayoshiriki Ligi
ya Jimbo la Nairobi, Fisa FC.
Mchezo kati
ya Zanzibar Heroes na Kenya utaanza kesho saa 10:00 jioni, ukifuatiwa na Nusu
Fainali ya pili, kati ya Uganda na Tanzania Bara Kilimanjaro Stars.
HANS POPPE AJA KAMPALA KWA MAMBO MAWILI MAKUBWA, WANAOSEMA SIMBA IMEFULIA WANAJIDANGANYA
Hans Poppe |
Akizungumza jana kwa simu kutoka Dar es Salaam, Kapteni huyo wa zamani wa
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) anakuja Kampala kufanya kazi za Simba SC.
Ingawa Hans
Poppe hakutaka kuzugumzia kwa undani ujio wake hapa, lakini tunatambua amekuja kufanya mazungumzo na kocha Mmalawi, Kinnah
Phiri na wachezaji kadhaa waliowavutia katika mashindano haya, akiwemo
mshambuliaji Mganda Brian Umony.
Lakini pia,
Hans Poppe anakuja kumalizana na mshambuliaji wao Mganda, Emmnanuel Okwi ambaye
amemaliza mkataba wake.
Vyombo vya
habari Dar es Salaam vimeripoti kuwa, Okwi atasaini mkataba wa mwaka mmoja
zaidi Simba SC kwa dau la dola za Kimarekani 40,000 pamoja na nyongeza ya
mshahara.
Okwi amekuwa
akihusishwa na habari za kuhamia Yanga na Azam FC baada ya kumaliza mkataba
wake Simba SC, lakini wakati huo huo inaelezwa amekwishafikia makubaliano na
Wekundu wa Msimbazi kuongeza mkataba.
POULSEN AFICHUA SIRI YA KUMPIGA BENCHI MSUVA
Kim Poulsen kulia na Msaidizi wake Marsh kushoto |
Akizungumza
na waandishi wa habari katika mahojiano maalum jana, Uwanja wa Mandela, Namboole,
alisema kwamba alipompa nafasi ya Kiemba amefanya kazi nzuri ambayo imemvutia
na kuamua kuendelea kumtumia kwenye kikosi cha kwanza.
“Najua Msuva
ni winga mzuri, ana kasi na anashambulia sana, lakini hata Kiemba anafanya kazi
nzuri, tena kama jana (juzi) amefunga hadi bao, kwa kweli ananivutia na
anafanya kazi yake vizuri,”alisema.
Msuva
alianza katika mechi mbili za mwanzoni za Kundi B kwenye michuano hii, dhidi ya
Sudan na Burundi, lakini baada ya hapo amemalizia benchi dakika zote 180 katika
mechi kwenye mechi mbili zilizofuata dhidi ya Somalia na Rwanda.
Hata hivyo,
Kim alisema bado Msuva anaweza akatokea benchi wakati wowote na kwenda kuongeza
nguvu katika kikosi cha Kilimanjaro Stars hasa katika hatua ngumu ambayo
michuano hii imefikia.
Stars
imefika Nusu Fainali na kesho itamenyana na wenyeji Uganda, Uwanja wa Mandela,
Namboole, kuanzia saa 12: jioni, mchezo ambao utatanguliwa na Nusu Fainali
nyingine kati ya Kenya na Zanzibar, itakayoanza saa 10:00 jioni.
Stars
ilitinga Nusu Fainali, baada ya kuifunga Rwanda mabao 2-0 juzi kwenye Uwanja wa
Lugogo mjini hapa, ambayo yalitiwa kimiani na Amri Kiemba na John Bocco.
Awali ya
hapo, Stars ilifuzu Robo Fainali kama mshindi wa pili kwenye kundi lake, nyuma
ya Burundi baada ya kujikusanyia pointi sita, yaani ikishinda mechi mbili 2-0
na Sudan na 7-0 na Somalia, wakati yenyewe ilifungwa 1-0 Mbayuwayu wa Bujumbura.
INJINI YA THE CRANES YAOMBA JEZI YA NIYONZIMA YANGA HARAKA
Oloya |
Yanga SC
inamfuatilia mchezaji huyo katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Tusker Challenge kwa ajili ya kumsajili, akazibe pengo la kiungo wake
Mnyarwanda, Haruna Niyonzima anayetakiwa na El Merreikh ya Sudan.
Akizungumza jana, Uwanja wa Mandela, Namboole baada ya kuiongoza nchi yake,
kuifunga Ethiopia mabao 2-0, Oloya alisema kwamba kama Yanga watafika Kampala na
kuzungumza naye, wakiafikiana atahamishia maisha yake Dar es Salaam.
“Nimebakiza
mkataba wa mwaka mmoja katika klabu yangu, lakini tukikubaliana naweza kuondoka
Vietnam bila masharti magumu, Yanga waje tu tuzungumze,”alisema.
Kiongozi mmoja
wa Yanga, jana alisema kwa njia ya simu jana kutoka Dar
es Salaam kwamba, wanafuatilia maendeleo ya Oloya katika michuano hiyo na iwapo
ataendelea kufanya vizuri watakuwa tayari kumsajili.
“Unajua
Haruna ana asilimia kubwa ya kuondoka, sasa lazima tupate kiungo mbadala mzuri
kama yeye na mzoefu, tumefuatilia kwa haraka haraka tumemuona huyu Oloya, ngoja
tuendelee kumuangalia,”alisema kiongozi huyo.
Oloya alizaliwa
Oktoba 22, mwaka 1992 na kabla ya kujiunga na Saigon Xuan Thanh mwaka 2010, aliichezea
KCC ya nyumbani kwao tangu mwaka 2009. Kiungo huyo alianza kuichezea Uganda
mwaka jana na sasa amekuwa tegemeo la timu hiyo.
SSENTONGO SASA AITAKA MWENYEWE SIMBA SC
Ssentongo |
MSHAMBULIAJI
wa Uganda, Robert Ssentongo amesema kwamba atakuwa tayari kujiunga na Simba SC
ya Dar es Salaam, wakiafikiana naye dau.
Ssentongo anayeng’ara katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, amewahi kuchezea Simba kwa muda tu katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, mwaka juzi mjini Kigali, Rwanda.
Lakini baada ya michuano hiyo, akatemwa na badala yake akasajiliwa kiungo Mganda mwenzake, Patrick Ochan ambaye baada ya msimu mmoja aliuzwa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
“Mimi nipo tayari Simba wakinitaka, wao wafike bei tu, ile ni timu kubwa na ninaamini nikijiunga nayo nitapata mafanikio,”alisema.
Ssentongo amewahi kucheza African Lyon ya Dar es Salaam na alipomaliza mkataba wake akachezea Simba kwa muda kabla ya kurejea Uganda.
Awali
Ssentongo aliwahi kuchukua fedha za Simba, lakini hakuja kujiunga nayo hadi
alipokuja Lyon.
NGASSA, BOCCO WAMNYIMA USINGIZI UMONY
Umony |
MSHAMBULIAJI
wa Uganda, Brian Umony amesema kwamba katika mechi mbili zilizobaki za Kombe la
Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge atajitahidi awapiku
wachezaji wa Tanzania, John Bocco na Mrisho Ngassa katika ufungaji wa mabao
kwenye michuano hiyo.
“Mimi nina
mabao matatu, wao kila mmoja ana mabao matano, sijakata tamaa, nitajitahidi
niwapiku, najua ni kazi ngumu, lakini nitajitahidi sana,”alisema mchezaji huyo
ambaye ameonyesha nia ya kujiunga na Simba SC ya Dar es Salaam.
Akiizungumzia
mechi ya Nusu Fainali dhidi yao na Tanzania Bara kesho, Umony alisema anaamini
itakuwa ngumu sana, lakini watapambana kushinda.
“Tanzania
wana timu nzuri sana, ina wazoefu ambao mimi nawajua kama Mrisho Ngassa na Juma
Kaseja, kwa kweli mchezo utakuwa mgumu, itakuwa mechi nzuri sana yenye hadhi ya
fainali,”alisema Umony.
Brian
amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na Express baada ya kumaliza mkataba wake,
Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009,
baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini kwa Umony,
ikamsajili Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
Umony
aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya
Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa
mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C.
Tayari Umony
amesema anaweza kujiunga na Simba wakiafikiana naye dau.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
John Bocco Tanzania 5
Mrisho
Ngassa Tanzania 5
Brian Umony Uganda 3
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
Chris
Nduwarugira Burundi 3
Geoffrey
Kizito Uganda 2
Robert
Ssentongo Uganda 2
Khamis Mcha Zanzibar 2
David
Ochieng Kenya 2
Clifton
Miheso Kenya 2
Dadi Birori Rwanda 2
CANNAVARO: KENYA WAUPE, TUTAWANG'OA WATAKE WASITAKE
Cannavaro |
NAHODHA wa
Zanzibar, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alikuwapo jana Uwanja wa Mandela, Namboole
akiishuhudia Kenya ikiichapa Malawi 2-0 na kutinga Fainali, lakini amesema Harambee
Stars ‘weupe tu kwao’.
Akizungumza
jana baada ya mechi hiyo, Cannavaro alisema kwamba kulingana na kiwango
kiliochoonyeshwa na Kenya katika mechi hiyo dhidi ya Malawi, wanaamini
watawafunga.
“Yaani jamaa
weupe sana, hata bao walilopata la kibahati bahati sana, mimi nakuambia sisi
hawa tunawafunga, timu yetu nzuri sana,”alisema beki huyo wa kati wa Yanga SC
ya Dar es Salaam.
Nahodha huyo
wa Yanga SC, alisema kwamba baada ya kuitoa Burundi juzi sasa anaamini Kombe la
Challenge litakwenda Zanzibar, kwani haoni timu nyingine ya kuwasumbua wao
katika mashindano haya.
Zanzibar juzi
ilikata tiketi ya kutinga Nusu Fainali baada ya kuichapa Burundi kwa penalti 6-5
kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 na sasa itacheza na mshindi
kati ya Kenya na Malawi katika Nusu Fainali.
Shujaa wa
Zanzibar juzi alikuwa ni Abdallah Othman aliyefunga penalti ya mwisho, baada ya
kipa Mwadini Ally kupangua penalti ya Abdul Fiston wa Burundi.
Manahodha wa
timu zote, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Zanzibar na Suleiman Ndikumana wa
Burundi walipoteza penalti zao juzi.
Ndikumana
alikuwa wa kwanza kwenda kupiga na mkwaju wake ukaota mbawa na kupaa juu ya
lango, wakati wenzake waliofunga mbali na Fiston kupoteza ni Steve Nzigamasabo,
Amisi Tambwe, Chris Nduwarugira, Leopold Nkurinkiye na Gael Duhatindavyi.
Upande wa
Zanzibar Heroes, Khamis Mcha ‘Vialli’ alikwenda kufunga penalti ya kwanza ya
Zanzibar, Adeyom Saleh Mohamed akafunga ya pili, Jaku Juma akafunga ya tatu,
kabla ya Cannavaro kumpelekea mikononi mkwaju wake kipa Arthur Arakaza wa
Burundi, Samir Hajji Nuhu akafunga ya tano, Aggrey Morris akafunga ya sita na
Othman kutumbukiza nyavuni ya ushindi.
BEKI STARS YAMVUNJA NGUVU OKWI
Okwi |
Akizungumza jana, Okwi alisema kwamba wachezaji wote wa safu ya ulinzi ya
Stars wana akili na nguvu za kupambana na mshambuliaji wa aina yeyote, hivyo
keso itakuwa kazi sana.
“Inahitaji
maarifa sana kuweza kupenya pale, Shomary (Kapombe) ni mchezaji mwenye akili
sana na anajituma, Yondan (Kevin), pia ana akili sana, uzoefu na anajituma.
Mimi nimemkuta pale Simba hadi anahamia Yanga (msimu huu).
Na tangu
nakuja Simba yeye ni mchezaji wa timu ya taifa, wana Kaseja (Juma) kipa mzuri
na mzoefu, tena sana, kwa hivyo ukuta wao ni mzuri sana, ila na sisi tuna safu
kali sana ya ushambuliaji, Diego (Hamisi Kiiza), Brian (Umony), Ssentongo (Robert),
Kizito (Geoffrey) na mimi, wote nadhani unajua cheche zetu.
Kwa hivyo
hiyo mechi itakuwa sana, lakini sisi kwa sababu tunacheza nyumbani, inatupa
nafasi nzuri zaidi ya kusonga mbele, yote kwa yote, mchezo utakuwa mgumu, ila
kushinda sisi lazima,”alisema Okwi.
Wakati ukuta
wa Cranes haujaruhusu hata bao moja, ukuta wa Stars umeruhusu bao moja tu
katika mechi nne, dhidi ya Burundi, tena la penalti lilofungwa na Nahodha wao,
Suleiman Ndikumana, Kilimanjaro Stars ikilala 1-0.
KIIZA: BOCCO ATAKUTANA NA UKUTA WA ZEGE
Kiiza |
Akizungumza jana, katika Uwanja wa Mandela, Namboole, Kiiza alisema kwamba
anamfahamu Bocco na kwenye Challenge ya mwaka huu anang’ara sana, lakini kesho
atakutana na ukuta wa wanaume wa shoka.
“Tunaiheshimu
Tanzania ni timu nzuri, na zaidi mfumo wao wanaocheza hivi sasa ni mzuri sana, lakini
hata sisi ni wazuri, hiyo mechi itakuwa kali sana,”alisema mshambuliaji huyo wa
klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam.
Kiiza
alisema mbali na Bocco, Tanzania Bara ina mchezaji mwingine hatari, Mrisho
Ngassa lakini wote wajue kwamba watakutana na ukuta wa Uganda, ambao katika
mechi nne haujaruhusu hata bao moja.
Uganda jana
ilifuzu kuingia Nusu Fainali ya Challenge, baada ya kuifunga Ethiopia mabao
2-0, ambayo yalitiwa kimiani na Geoffrey Kizito dakika ya nne na Robert
Ssentongo dakika ya 60.
Kwa ushindi
huo, Uganda itamenyana na Tanzania Bara katika Nusu Fainali Alhamisi usiku,
mchezo ambao utatanguliwa na Nusu Fainali nyingine kati ya Kenya na Zanzibar,
itakayoanza saa 10:00 jioni.
Kenya ilifuzu
Nusu Fainali jana, baada ya kuifunga Malawi 1-0, bao pekee la Mike Barasa dakika
ya 56.SENEGAL YAKUBALI YAISHE.
SHIRIKISHO la Soka
nchini Senegal-FSF limetangaza jijini Dakar jana kuwa hawatakata rufani
kufuatia adhabu waliyopewa na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF
kufuatia tukio la mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika 2013. Maofisa
wa FSF wamesema ingawa wamepewa nafasi ya kukata rufani kuhusiana na
uamuzi wa shirikisho hilo kuufungia Uwanja wa Leopold Sedar Senghor kwa
kipindi cha mwaka mmoja wameamua kutokupinga adhabu hiyo. Kamati
ya Nidhamu ya CAF pia imelitoza shirikisho hilo faini ya dola 100,000
ambayo inatakiwa kulipwa katika kipindi cha miaka miwili. Adhabu
hiyo imekuja kufuatia mashabiki wan chi hiyo kuvuruga mchezo wa
marudiano wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika baina ya Senegal na
Ivory Coast Octoba 13 mwaka huu katika kipindi cha pili wa Ivory wakiwa
wanaongoza kwa mabao 2-0. Tukio lilisababisha mchezo huo kusimamishwa huku baadae CAF ikiamua kuiengua Senegal na kuipa nafasi Ivory Coast kufuzu.
SIJAHUZUNISHWA NA UAMUZI WA FIFA - DROGBA.
MSHAMBULIAJI nyota wa
Ivory Coast, Didier Drogba amesema kuwa hajakasirishwa na uamuzi wa
Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kumkatalia ombi lake la kuondoka
Shanghai Shenhua kwa mkopo kwenda katika klabu yake ya zamani Chelsea
kabla ya kipindi cha dirisha la usajili kufunguliwa. Drogba
amesema hakutegemea kukubaliwa kwa ombi lake kutoka kwa shirikisho hilo
kwasababu ni kitu kisicho cha kawaida na hakukuwa na dhamana kwamba
kitakubalika. Nyota
huyo ambaye kwasasa anafanya mazoezi katika klabu yake hiyo ya zamani
kwa ajili ya kujiwenda na michuano ya Mataifa ya Afrika yakayoanza
Januari 19 mwakani amesema kukataliwa huko hakuwezi kumkosesha usingizi
kwakuwa alikuwa anajaribu. Katika
taarifa yake FIFA imesema kuwa ombi la mchezaji huyo lingewezekana kama
mkataba wake ungekuwa umeisha wakati wa dirisha la usajili bado
halijafunguliwa lakini Drogba bado ana mkataba na Shenhua mpaka 2015.
MSHINDI WA BALLON D'OR TAYARI AMESHAJULIKANA.
MENEJA wa klabu ya Real
Madrid, Jose Mourinho amedai kuwa mshidi wa tuzo ya Ballon d’Or tayari
ameshaamuliwa kwa kuwatuhumu Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kumpigia
debe nyota wa Barcelona Lionel Messi. Messi
ndio anayepewa nafasi kubwa ya kunyakuwa tuzo hiyo ya mchezaji bora
duniani kwa mara ya tatu mfululizo lakini anakabiliwa na upinzani kutoka
kwa mchezaji mwenzake kutoka Barcelona Andres Uniesta na mshambuliaji
nyota wa Madrid Cristiano Ronaldo. Kauli
hiyo ya Mourinho ilikuja wakati akiulizwa kama Ronaldo ana nafasi ya
kunyakuwa Ballon d’Or baada ya ushindi wa mabao 4-1 iliyopata Madrid
dhidi ya Ajax jana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akijibu
swali hilo Mourinho amesema kuwa wakati FIFA wakiongea na kufanya
kampeni hakuna unaloweza kufanya hivyo anadhani tuzo ya Ballon d’Or
tayari imeshatolewa.
MESSI KUVUNJA REKODI YA MULLER KATIKA MCHEZO DHIDI YA BENFICA.
USIKU WA ULAYA MANCHESTER CITY WAAGA KWA AIBU ILHALI ARSENAL NAO WAKISHIKISHWA ADABU NA OLYMPIAKOS.HABARI NA MATUKIO KATIKA PICHA .
Olympiakos iliyotokea
nyuma imefanikiwa kuichapa Arsenal mjini Piraeus, na kuwafanya washika mitutu
hao kumaliza katika nafasi ya pili katika kundi B nyuma ya Schalke.
Tomas Rosicky
alianza kufunga bao la uongozi kwa Arsenal kabla ya bao la kipindi cha pili la Giannis
Maniatis lililokuwa la kusawazisha na baadaye Kostas Mitroglou kuandika bao la
pili na la ushindi kwa wagiriki.
Kocha wa
Schalke Leonardo Jardim aliwatumia wachezaji wake ambao ni wafungaji wakubwa
katika ligi ya Ugiriki Rafik Djebbour na
Djamel Abdoun sehemu ya kiungo.
Akiwa ni
mwenye matumaini ya kufuzu, Wenger alikifanyia mabadiliko kikosi chake
kilichopoteza dhidi ya Swansea mabao 2-0 mwishoni mwa juma akimrejesha Rosicky kiungoni
pamoja na kinda wa miaka 20 Jernande Meade akicheza dakika zote za mchezo.
MANCHESTER CITY 0 VS DOTMUND 1
Manchester
City imemaliza kampeni ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa kichapo
kingine cha bao 1-0 toka Borussia
Dortmund.
Bao la
kipindi cha pili la Julian Schieber kunako dakika ya 57 lilitosha kuwaondosha katika
harakati za kusonga mbele na michuano hiyo huku wajerumani wakifurahia mchezo
ambapo walitengeneza nafasi nyingi karibu sehemu kubwa ya mchezo.
Matokeo hayo
yana maanisha kuwa kikosi cha Roberto Mancini kimemaliza michezo yake ya kundi
D kikiwa mkiani bila ushindi hata mmoja na Dortmund wakifanikiwa kusonga mbele
katika hatua ya mtoano ya michuano hiyo.
- MATOKEO MENGINE
- Din Zagreb 1 - 1 Dynamo Kiev FT
- Malaga 2 - 2 Anderlecht FT
- Montpellier 1 - 1 Schalke 04 FT
- Paris SG 2 - 1 FC Porto FT
- Real Madrid 4 - 1 Ajax FT
UEFA CHAMPIONZ LIGI: Man City waikosa hata EUROPA LIGI!
>>TIMU 13 zipo Mtoano, Bado 3 kupatikana Mechi za LEO!
>>CHELSEA nini LEO??
Mabingwa
wa England, Manchester City, jana walichapwa Bao 1-0 na Borussia
Dortmund katika Mechi ya mwisho ya Kundi D na kutupwa nje ya Ulaya huku
wenzao Arsenal wakifungwa 2-1 huko Ugiriki na Olympiacos lakini Arsenal
walikuwa tayari wameshafuzu kutoka Kundi lao kabla ya Mechi hiyo.
+++++++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumanne Desemba 4
GNK Dinamo 1 FC Dynamo Kyiv 1
Paris SaintvGermain 2 FC Porto 1
Montpellier Hérault 1 FC Schalke 1
Olympiacos FC 2 Arsenal 1
Málaga 2 RSC Anderlecht 2
AC Milan 0 FC Zenit St. Petersburg 1
Borussia Dortmund 1 Manchester City 0
Real Madrid 4 AFC Ajax 1
+++++++++++++++++++++++++++++++
Wakihitaji ushindi, hasa wakati Real
Madrid, wakiicharaza Ajax Bao 4-1 katika Mechi nyingine ya Kundi D kwa
msaada mkubwa wa Nyota wao Cristiano Ronaldo, Man City walijikuta
wakitunguliwa Bao katika Dakika ya 57 na Julian Schieber.
+++++++++++++++++++++++++++++++
TIMU ZILIZOFUZU KUCHEZA RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16:
-KUNDI A: PSG, Porto
-KUNDI B: Schalke, Arsenal
-KUNDI C: Malaga, AC Milan
-KUNDI D: Dortmund, Real Madrid
-KUNDI E: Shakhtar Donetsk
-KUNDI F: Bayern Munich, Valencia
-KUNDI G: Barcelona
-KUNDI H: Manchester United
+++++++++++++++++++++++++++++++
Man City sasa wapo nje kabisa ya
Mashindano ya Ulaya kwani nafasi ya 3 imechukuliwa na Ajax ambao
watacheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 za EUROPA LIGI.
Mechi nyingine za mwisho za Makundi E
mpaka H zinachezwa leo ambazo ndizo zitatoa Timu 3 zilizobaki
kukamilisha jumla ya Timu 16 zitakazocheza Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
+++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZA MWISHO ZA MAKUNDI:
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Jumatano Desemba 5
FC Shakhtar Donetsk v Juventus
Chelsea FC v FC Nordsjælland
LOSC Lille v Valencia CF
FC Bayern München v FC BATE Borisov
FC Barcelona v SL Benfica
Celtic FC v FC Spartak Moskva
Manchester United FC v CFR 1907 Cluj
SC Braga v Galatasaray A.S.
++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments:
Post a Comment