MASHABIKI ANAPASWA KUHESHIMU TIMU ZINGINE - LOEW.
KOCHA wa timu taifa ya
Ujerumani, Joachim Loew amewataka mashabiki wa soka wan chi hiyo
kuheshima viwango vya timu nyingine na kutotegemea makubwa kutoka kwa
timu yao ya taifa. Katika
mahojiano yake na wavuti wa Shirikisho la Soka la Ujerumani-DFB Loew
amesema kuwa anaamini mashabiki wa soka nchini humo watakuwa wamepata
somo kwa mwaka huu kuelekea katika mwaka mpya. Amesema
timu ya taifa ya Hispania imekuwa ikifanya kazi ili ishinde vikombe kwa
miaka mingi hivyo Ujerumani nayo anafikiri inaweza kufanya vizuri kama
ikiheshimu wapinzani wake kwani sio wao pekee wenye ndoto za kunyakuwa
vikombe. Kocha
huyo alimalizia kuwa ni mapema mno kwa mashabiki wa nchi hiyo
kuzungumzia michuano ya Kombe la Dunia 2014 itakayofanyika nchini Brazil
hivi sasa badala kusaidia kuandaa timu bora ambayo italileta kombe hilo
wakati ukifika.
No comments:
Post a Comment